Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana... Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza......
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili... Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya... Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake... Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa... Naye akajibiwa kuwa.. Hatasubiri afanye hivyo... Watamfuata huko huko juu.....

Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika... (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa. ..
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya... Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi... Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo... Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji...

Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?!?
Je ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini.. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo... Naamini siku moja ukweli utajulikana
RIP Agnes!
@mshana jr kifo ni haki ya kila mtu.
Hata mm na ww hatujui tutakufa kwa njia ipi,,..
Hakuna sababu ya kujadili mauti yanapomfika mtu.
Kumbuka kwamba kila binadamu atakufa kwa njia aliyopangiwa na muumba wake..
R. I. P Agnes
 
Mkuu Mshana Jr bandiko lako linasomeka vizuri sana, umaarufa huja aidha kwa kusifiwa ubaya ama uzuri, hata ukiwa jambazi sugu pia utapata umaarufu. Zamani kidogo wakati naenda masomoni South Africa nilipanda ndege moja na huyu dada, yeye alikuwa siti ya mbele yangu na jamaa mmoja hivi ambae sura yake huwezi kumtazama mara mbili ingawa jamaa alikuwa amesheheni vito vya thamani mno mwilini mwake. "Agness au sie"?.. "ndio mwenyewe, za wapi mwenzangu?" "masomoni south" "poa tupo pamoja safari iwe njema". Mimi... safari njema my dada. Nilipata mashaka sana na jamaa aliekaaa nae. Baada ya hapo ikawa skendo kwenye skendo. Kwa kweli tokea siku kila nikimuona kwenye media basi najisikia huruma sana nilijua maisha anayochagua kuishi sio kabisa wanaoishi south africa wanajua vizuri haya mambo. Sasa hapa ukiunganisha dots za wakina chifupa, aliekuwa mkurugenzi wa TBS akafia Tanga, na wengineo. Nakubaliana na wewe kifo kipo lakini kinakuwa na sababu.
 
Habari wana jamii, nimesikitishwa sana na kifo cha Video quen maarufu Agnes Gelard almaarufu Masogange, Pia nimesikitishwa hasa na watanzania tulivyo kuwa hatuna utu yaaninkuna watu wanmpost Agnes mitandaoni huku wakitoa na maneno ya kashfa ambayo hayafai kumtole Maiti kingine ambacho nashindwa kuelewa na nimesikitishwa zaidi ni jinsi picha ambazo watanzania wanatumia kumpost humo mitandaoni marehemu Masogange yaani ni picha chafu ambazo hazina maadili kwa umma nnacho kishangaa ni jee Masogange hana picha nzuri za staha ambazo watu wanaweza kuzitumia kuposti mitandaoni kushow apreciation? au ndio muendelezo wa kumzihaki marehemu?.

Kitu kingine ni hili swala la watu wanaohoji na kuhusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani, yaani watu wanaamini Masogange hajafa bure yaani kuna watu wanahusika katika kifo chake, yaani kwa maana hiyo watu wanapuuza taharifa zilizotolewa hospitali kuwa marehemu alilazwa kwa siku nne kwa maradhi ya Pumu pamoja na upungufu wa damu,Nadhani wengi tunajuwa pumu likikubana unakuwa katika hali gani. Mimi mwenyewe nimeshawahi kuumwa Pumu mara kadhaa katika umri wangu kwa hiyo na declare interest Pumu ni ugonjwa hatari sana pale linapokuamulia kukushika haswa maana linahusiana moja kwa moja na mfumo wa upumuaji,Pia tunajuwa madhara ya upungufu wa damu lakini pia tujuwe kuwa Masogange hakupelekwa hospitali bali hospitali alikwenda yeye mwenyewe baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa pumu.

Naumia sana nnapo waona watu niliyokuwa nawaheshimu kama Mshana Jr naye ni miongoni mwa watu wanaohusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani kupitia post zake tofauti zilizopo humu jukwaani.

Nnacho kiona hawa watu wote wanaokihusisha kifo cha masogange na kufanyiwa njama na watu flani naona ni upungufu wa akili pamoja na ukosefu wa kazi za kufanya kutokana na fikira zao finyu.

Masogange kafa kama Mwenyezi Mungu alivyotuambia katika Qur'an "Qullinafsi Dhaaikatul Mauti" Kila nafsi yenye uhai au yenye roho itaonja umauti. Kikubwa niwahusiye nafsi zenu wana jukwaa pamoja na kuihusia nafsi yangu jamani tumcheni Mola wetu haya maisha ya duniani ni mafupi mno huyo Masogange kafa nadhani hata miaka 35 hajafikisha leo yeye Masogange kesho ni mimi au wewe unaesoma uzi huu, jee umejiandaaje na siku yako ya kufa jee umejiandaaje na safari yako ya mwisho ya kurudi kwa Mola wako. Tuacheni kuchukulia matatizo ya watu wengine na kuyahusisha na masuala ya kisiasa. Kuna watu walinishangaza zaidi eti wanahitaji Postmoterm ya kifo cha Masogange wakati wanajuwa fika kama marehemu alikuwa anaumwa Pumu, jee wangapi hawajuwi kama pumu linauwa? nadhani wote tunajuwa kuwa Pumu linauwa na ndilo lililosababisha kifa cha mpendwa wetu Masogange.

Mwisho nitowe ushauri kwa wadada wote watakao soma uzi huu, tuangalie sana picha tunazozipost kwenye mitandao yetu ya kijamii zinaweza kuja kukuharibia sifa zako hapo baadaye maana picha zako zinaishi wewe mwenyewe hauishi muda mrefu. Agnes Masogange awe funzo kwenu maana R.I.P zote anazopewa ukianga photo attachment moyo razima uume hii nikutokana ndio picha nyingi alizokuwa nazo labda kwenye akaunti zake za social media. Lakini hata kama mtu alikuwa na matendo mabaya kwa wewe hnavyohisi sio vizuri kutoa aibu zake hadharani maana kwa sisi waislamu Mtume Muhammadi S.A.W anasema msithubutu kutoa aibu za maiti zenu hilo sio jambo jema kabisa.

Mwisho kabisa nasikitika Marehemu Masogange kaondoka hali yakuwa ndoto zangu hazijakamilika hata kidogo. Hakuna anayebisha Marehemu alikuwa ni mrembo haswa na mimi ni miongoni mwa wanaume wachache sana tuliyofanikiwa kuuona uzuri wa Masogange na nilikuwa nipo kwenye process za kutaka kwenda kwao na kupeleka barua ya uchumba. sio siri nimesikitika sana basi japo hata ningepata japo hata salamu yake tu kabla hajafa ili atleast ndoto yangu ifikie japo hata robo.

All in all Mungu ailaze roho ya marehemu Agness mahali pema peponi na Mwenyezi Mungu ampe kauli thabiti marehemu.
 
Ila watanzania tuna akili za kujua wenyewe kwahiyo wewe hapa unaongelea nini? Kwani wewe na hao unaowashangaa mnatofautiana nini?
 
Kila nafsi itaonja umauti, iwe mimi, Wewe, na mwingine huu ni ukweli mchungu ambao binadamu wengi hawapendi kuusikia. Ndio maana siku zote panapotokea umauti watu hawakosi sababu .

Siku yako ikifika hata mtu akitua kidole cha macho unaondokaa. Tufanye yoteee ila Iko siku tutakua ni Mauti Kama Agnes na wengineo waliotangulia.

Kifo ni moja ya ibada Kwa tuliopo Hai tupate kujifunza na kukubali kwamba kifo kipo hakikwepeki na ndipo watu Kwa kipindi hiki neno Mungu litatamalaki midomoni mwa watu. Hujui Kwa kupitia kifo cha Agness Wangapi watazaliwa upya kiroho .

Tufanyeee yote ila tukumbuke kuna kufaa hata Ukiwa MA Pesa kiasi gani, hate Ukiwa na nguvu kiasi gani utaondoka. Na Kama siku yako haijafika Hutokufa abadani.

Fact. Ila mwishoni umevuruga kabisa....kwenye black!
 
Mkuu unataraji chochote kipya katika ripoti ya post mortem..

Mkuu hiv ndugu zako wakikupeleka hospital, daktar akasema una pneumonia ukalazwa baada ya siku 2 ukifariki nduguzo watadai chanzo ni nin!!?

Sasa katika hili mbona kila mmoja anakuja na lake, mpaka sasa zishakuja sababu 4 tofauti
Ndugu wakihisi kuna foul play wanaweza kuomba ufanyike uchunguzi.

Sasa kama hawana shaka na hata askari wakiwa hawana shaka kunakua hakuna sababu ya uchunguzi kufanywa.

Tutabaki online community kukisia sababu ya kifo.
 
Habari wana jamii, nimesikitishwa sana na kifo cha Video quen maarufu Agnes Gelard almaarufu Masogange, Pia nimesikitishwa hasa na watanzania tulivyo kuwa hatuna utu yaaninkuna watu wanmpost Agnes mitandaoni huku wakitoa na maneno ya kashfa ambayo hayafai kumtole Maiti kingine ambacho nashindwa kuelewa na nimesikitishwa zaidi ni jinsi picha ambazo watanzania wanatumia kumpost humo mitandaoni marehemu Masogange yaani ni picha chafu ambazo hazina maadili kwa umma nnacho kishangaa ni jee Masogange hana picha nzuri za staha ambazo watu wanaweza kuzitumia kuposti mitandaoni kushow apreciation? au ndio muendelezo wa kumzihaki marehemu?.

Kitu kingine ni hili swala la watu wanaohoji na kuhusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani, yaani watu wanaamini Masogange hajafa bure yaani kuna watu wanahusika katika kifo chake, yaani kwa maana hiyo watu wanapuuza taharifa zilizotolewa hospitali kuwa marehemu alilazwa kwa siku nne kwa maradhi ya Pumu pamoja na upungufu wa damu,Nadhani wengi tunajuwa pumu likikubana unakuwa katika hali gani. Mimi mwenyewe nimeshawahi kuumwa Pumu mara kadhaa katika umri wangu kwa hiyo na declare interest Pumu ni ugonjwa hatari sana pale linapokuamulia kukushika haswa maana linahusiana moja kwa moja na mfumo wa upumuaji,Pia tunajuwa madhara ya upungufu wa damu lakini pia tujuwe kuwa Masogange hakupelekwa hospitali bali hospitali alikwenda yeye mwenyewe baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa pumu.

Naumia sana nnapo waona watu niliyokuwa nawaheshimu kama Mshana Jr naye ni miongoni mwa watu wanaohusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani kupitia post zake tofauti zilizopo humu jukwaani.

Nnacho kiona hawa watu wote wanaokihusisha kifo cha masogange na kufanyiwa njama na watu flani naona ni upungufu wa akili pamoja na ukosefu wa kazi za kufanya kutokana na fikira zao finyu.

Masogange kafa kama Mwenyezi Mungu alivyotuambia katika Qur'an "Qullinafsi Dhaaikatul Mauti" Kila nafsi yenye uhai au yenye roho itaonja umauti. Kikubwa niwahusiye nafsi zenu wana jukwaa pamoja na kuihusia nafsi yangu jamani tumcheni Mola wetu haya maisha ya duniani ni mafupi mno huyo Masogange kafa nadhani hata miaka 35 hajafikisha leo yeye Masogange kesho ni mimi au wewe unaesoma uzi huu, jee umejiandaaje na siku yako ya kufa jee umejiandaaje na safari yako ya mwisho ya kurudi kwa Mola wako. Tuacheni kuchukulia matatizo ya watu wengine na kuyahusisha na masuala ya kisiasa. Kuna watu walinishangaza zaidi eti wanahitaji Postmoterm ya kifo cha Masogange wakati wanajuwa fika kama marehemu alikuwa anaumwa Pumu, jee wangapi hawajuwi kama pumu linauwa? nadhani wote tunajuwa kuwa Pumu linauwa na ndilo lililosababisha kifa cha mpendwa wetu Masogange.

Mwisho nitowe ushauri kwa wadada wote watakao soma uzi huu, tuangalie sana picha tunazozipost kwenye mitandao yetu ya kijamii zinaweza kuja kukuharibia sifa zako hapo baadaye maana picha zako zinaishi wewe mwenyewe hauishi muda mrefu. Agnes Masogange awe funzo kwenu maana R.I.P zote anazopewa ukianga photo attachment moyo razima uume hii nikutokana ndio picha nyingi alizokuwa nazo labda kwenye akaunti zake za social media. Lakini hata kama mtu alikuwa na matendo mabaya kwa wewe hnavyohisi sio vizuri kutoa aibu zake hadharani maana kwa sisi waislamu Mtume Muhammadi S.A.W anasema msithubutu kutoa aibu za maiti zenu hilo sio jambo jema kabisa.

Mwisho kabisa nasikitika Marehemu Masogange kaondoka hali yakuwa ndoto zangu hazijakamilika hata kidogo. Hakuna anayebisha Marehemu alikuwa ni mrembo haswa na mimi ni miongoni mwa wanaume wachache sana tuliyofanikiwa kuuona uzuri wa Masogange na nilikuwa nipo kwenye process za kutaka kwenda kwao na kupeleka barua ya uchumba. sio siri nimesikitika sana basi japo hata ningepata japo hata salamu yake tu kabla hajafa ili atleast ndoto yangu ifikie japo hata robo.

All in all Mungu ailaze roho ya marehemu Agness mahali pema peponi na Mwenyezi Mungu ampe kauli thabiti marehemu.

kaka umeandika maneno mazuri lakini umekosea kusema kama wewe ni mmoja wapo umeona uzuri wake kwanza ulitakiwa usiseme maana umetoa aibu yake kwamba ulikuwa nae. pili unasema wewe ni muislam lakini huujui uislam dini imekataza kuzini na kujitangaza kwa kuzini
 
mkuu sijasema nimedhini nadhani umesoma hadi mwisho lakini hukunielewa nimesema kuwa nimeuona uzuri wake nadhani uzuri huo hata wewe kama una macho mazuri unaweza kuuona na nimekili kabisa kuwa nilikuwa nipo kwenye process za kuandaa barua ili ipelekwe kwa wazazi wake ili kuwa mchumba wa marehemu na ndio maana nikasema nahudhunika Agnes kaondoka sijapata hata salamu yake mkuu
 
RIP Agnes..
Njemba na vigogo wanaojulikana wamekutumia mpaka wakaamuwa hawakakuhitaji tena, ila malipo ni hapa hapa duniani, usijali, tutakuhadithia tukija ulipotangulia..

Msanii wa filamu Tanzania, Agnes Gerald 'Masogange' alikamatwa na dawa za kulevya Afrika Kusini hivi karibuni.
ziro99blog: MAJINA NA PICHA ZA WAUZA DAWA ZA KULEVYA SASA KUCHAPISHWA MAGAZETINI...

Agnes Masogange afunguka maisha yake ya jela yalivyokuwa via YouTube
agnes.JPG
mednewcatch.jpg
wp-1497543587197.jpg
Masogange-1-1.png
f6f8b2de90c711e3816c12045ea5e329_8-1.jpg
masogange (4).jpg
Agnes-Masogange16.jpg
masogange.jpg
MASOGANGE 4.jpg
mwakyembe.jpg
 
Attachments

  • masogange (4).jpg
    masogange (4).jpg
    37.8 KB · Views: 75
Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana... Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza......
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili... Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya... Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake... Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa... Naye akajibiwa kuwa.. Hatasubiri afanye hivyo... Watamfuata huko huko juu.....

Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika... (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa. ..
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya... Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi... Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo... Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji...

Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?!?
Je ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini.. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo... Naamini siku moja ukweli utajulikana
RIP Agnes!
Msshana umefikiria na kufikirisha vema kama ambavyo ninafikiri mimi kulingana na namna haya makundi ya dawa wanavyotekelezaga mipango yao...wako very bright sana
 
RIP Agnes..
Njemba na vigogo wanaojulikana wamekutumia mpaka wakaamuwa hawakakuhitaji tena, ila malipo ni hapa hapa duniani, usijali, tutakuhadithia tukija ulipotangulia..

Msanii wa filamu Tanzania, Agnes Gerald 'Masogange' alikamatwa na dawa za kulevya Afrika Kusini hivi karibuni.
ziro99blog: MAJINA NA PICHA ZA WAUZA DAWA ZA KULEVYA SASA KUCHAPISHWA MAGAZETINI...

Agnes Masogange afunguka maisha yake ya jela yalivyokuwa via YouTube
View attachment 752302 View attachment 752305 View attachment 752306 View attachment 752307 View attachment 752309 View attachment 752310 View attachment 752311 View attachment 752312 View attachment 752313 View attachment 752316
mkuu hizi picha ulizo attach kwenye huu uzi wako ni hatari aiseeee
 
Back
Top Bottom