Ilikuwa mwaka 1981

Ilikuwa mwaka 1981

Baada ya huo ulikuwa "njiwa peleka salamu" JKT taarabu.
Kuna wimbo wa..
Kifo cha mma naliaa, kimetia uchunguu.. mama enheeee mama enheeee, kilio umechiaaa... nilikuwa napiga marimba na wakati mwingine kinanda kwenye kikundi cha sanaa cha shule
 
Kuna wimbo wa..
Kifo cha mma naliaa, kimetia uchunguu.. mama enheeee mama enheeee, kilio umechiaaa... nilikuwa napiga marimba na wakati mwingine kinanda kwenye kikundi cha sanaa cha shule
huo siukumbuki ninakumbuka tu mchana kipindi cha peleka salamu RTD, kipindi cha mama na mwana.
 
Hapo sasa nilikuwa Phlips EA tunatengeneza radio kwa ajili ya vita ya Uganda inaishia na ukombozi.

Nakumbuka Jamhuri Jazz na nyimbo za Pamela Atomic Jazz na Tanzania yetu Zahir Ali na Joka Iddi Amin Western Jazz na Jela ya Mapenzi. Dar Jazz Moro jazz etc etc wacha tu

Tulitangaziwa miezi 18 ya kufunga mkanda na Mwl Nyerere Ingawa hadi leo bado tunafunga mikanda.

SI UCHOCHEZI NI KWELI
 
Philips, ndiyo yenyeweee.. sauti safi sauti kubwaaa.... philips
 
Kulikua na kipindi RTD kinaitwa Ngoma zetu asilia kiliendeshwa na Bujaga Izengo Kadago, halafu kipindi cha Mbiu ya mikoa unakutana na mtangazaji mahiri kabisa Michael Katembo.
 
Naikumbuka sana RTD

Dah! enzi za kuunganisha betri ili uweze kusikiliza redio, nakumbuka zaidi 'club raha leo show' mtu akitambulishwa anapiga chombo chake kidogo au anaimba kidogo basi anashangiliwa na umati
 
Kajukuu katakorithi kipaji changu mtaomba wazazi wake waniachie nimlee ili nikinoe vizuri kipaji chake...

Mi sipendagi ujinga wa kupoteza vipaji maalum na adimu LOL
Hahahahahah huhitaji kunoa huwa ni mara mbili ya muhusika pale atapokwambia "sio hivyo babu"
 
Naikumbuka sana RTD

Dah! enzi za kuunganisha betri ili uweze kusikiliza redio, nakumbuka zaidi 'club raha leo show' mtu akitambulishwa anapiga chombo chake kidogo au anaimba kidogo basi anashangiliwa na umati
Ili radio iongee hadi ipigwe kibao ndio itaongea yaani ikinyamaza tu inapigwa
 
Toto disco Msasani Club, bila Madonna Holiday hatujatendewa haki.
Sisi tulikuwa tunakwenda gogo disco Africana sasa ikawa tukiingia hatutoki hata tuitwe vipi hatutoki wakaona isiwe shida siku hiyo tumejiandaa hatuitwi ikabidi tukawastue tulipewa jibu moja.... nendeni msasani kwa miguu M bembelezwe Nyie kina nani?
 
Hahahaaa! Zile radio nyuma zina kama "plywood" laini na ina matundu tundu halafu imeandikwa Dudu proof
Umenikumbusha hizo mama alikuwa nazo mbili kusafiri kaka akahonga moja afanye nini na hela hana mwenyewe karudi haipo alipoulizwa akaona isiwe shida akaenda kumnunulia birika la chai bi mkubwa acha aangue kilio kila akiliona lile birika utasikia wallahi matumbo haya
 
Na umeliweka kwenye wanga... mgongoni kuna malinda ya mraba, na mabegani pia....

Kuna wakati BLUEE ILIKUWA INAHUSIKA
Ukikosa "Bluu" unatumia dawa flani ya vidonda ina rangi ya bluu inaitwa Jivii 😀😀
 
Back
Top Bottom