Ilikuwa mwaka 1981

Ilikuwa mwaka 1981

Kuna mutu ilikuwa inaitwa Jerry Nashon aka Dudumizi sas ni Marehemu! Hapo nipo darasa la 4 tandika shule ya msingi, dah imenikumbusha mbaaaaaaali! Bar ya maana ilikuwa inaitwa Majaribio Bar, ipo hadi Leo!
Jerry Nashon alikulia katika kijiji kiitwacho Kigera kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma jirani na shule ya Sekondari Mara. Jerry alianza kujifunza gitaa akiwa Musoma Catholic Mission club ambayo leo ni Mwembeni secondary School. Alikuwa ana mazoea ya kwenda kwenye hiyo social club ya kanisa iliyofanya kazi nzuri sana ya kuwaunganisha vijana wenye vipaji mbalimbali. Alijiunga katika bendi ya Special Baruti Band iliyokuwa na Rashid Ruyembe mwaka 1980.
1483199320235.jpg

Jerry akiwa Magereza Jazz band amabapo alidumu kwa muda, na kisha akahamia Bima Orchestra nahatimae Vijana Jazz Band mpaka mauti yake.
 

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Sikuile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungurakarukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karukatena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitakimbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Siokama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikia,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
 
Back
Top Bottom