Ilikuwa mwaka 1981

Ilikuwa mwaka 1981

Mkuu wewe ulisoma Juma na Roza, Lusi na Damasi?
Screenshot_2017-01-02-07-45-20.jpg
Mkuu Juma na Roza hawa hapa nimekuletea ujikumbushe mbali.
 
Immaculata_ Bima Lee

Haloo Immaculata mama
Vipi Immaculata mama
Nakutafuta sikuoni mama
Napiga darubini sikupati mamaa
Napiga tarumbeta sikupati mamaa

Ni umbali gani ulipooo
Nipigie simu namba 26561

Hakyamungu nakupenda Immaculata natoka jandoni mama nishike mkono nipeleke mbele ya wazee

Nafanya nini nderakendr ?

Nakupendaaaa aa.................. Endelea mwenyewe

Hapo unawakuta jamaa waliotoka NGINDE Mulenga "Spoiler" gitaa la Solo, Mwanyiro "Computer" Bass Gitaa, Abdallah Gama, Rhythm Guitar wakiambatana na Shabaan Dede huku wakiwakuta wenyeji Nguli mwenyewe Jerry Nashon Dudumizi akina Roy Bashekanako, Momba "sauti ya chuma" etc

Huo ulikuwa muziki halisia wa Kitanzania na ubunifu wa hali ya juu bila kusaidiwa na Kompyuta!
Umenikumbusha mbali sana.Niliwahi sikia simulizi fulani kuhusu wimbo huu.Ni kwamba Jerry Nashon alikutana na huyo dada mrembo Imaculata huko Musoma.Inasemekana Jerry alivutiwa sana na binti huyo.Sasa akatokea siku moja akaenda nyumbani kwao huyo binti ili aweze kumwaga sera zake lakini kwa bahati mbaya hakumkuta na akaambiwa amekwenda nje ya mkoa wa Mara.Na hakukuwa na mawasiliano mengine ya kumpata huyo binti hasa ukiangalia miaka hiyo haikuwa na njia nyingi za mawasiliano kama ilivyo leo.Kwahiyo jamaa akaamua kuweka namba zake hewani ili Imaculata akisikia ampigie.Na ndani ya wimbo huu Jerry kachanganya kidogo na kijaruo kuonyesha tu hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo juu ya binti huyo.

Nyimbo nyingine alizoimba Jerry Nashon kwa hisia kali za mapenzi ni pamoja na; Sarah nyota ya uzuri,mama Shani,Pesa bado zanisumbua,Neema,VIP,Thereza,Top queen nk.
 
Hapana mwaka huo hao walikuwa hawajaja. Alikuwapo mtu anaitwa Belesa Kakere. Hao walikuja kunako 1984
Balesa Kakere aliufanyia haki wimbo wa Asia.

Asia ohoox2
Asia..
Asia wa mama umenihuzunisha..
Asia umeondoka bila ya taarifa...
Asia umeondoka bila ya kuniaga...
Duu jamani zamani ilikuwa raha sana.
 
Wakati ninaanza kusoma hivi vitabu, tulikuwa pia tunafundishwa kuingia kwenye mahandaki kama Vita ya Kagera ikiendelea.
Duh umenikumbusha mahandaki... yaani nilichimba moja la shepu ya L unaingilia na kutokea mwisho au mwanzo wa hiyo L.

Wakati wanajeshi wanarudi Songea, wengine waliponduka na kufa pale Lukumburu.

Tulijipanga barabani kuwashangilia
 
Umenikumbusha mbali sana.Niliwahi sikia simulizi fulani kuhusu wimbo huu.Ni kwamba Jerry Nashon alikutana na huyo dada mrembo Imaculata huko Musoma.Inasemekana Jerry alivutiwa sana na binti huyo.Sasa akatokea siku moja akaenda nyumbani kwao huyo binti ili aweze kumwaga sera zake lakini kwa bahati mbaya hakumkuta na akaambiwa amekwenda nje ya mkoa wa Mara.Na hakukuwa na mawasiliano mengine ya kumpata huyo binti hasa ukiangalia miaka hiyo haikuwa na njia nyingi za mawasiliano kama ilivyo leo.Kwahiyo jamaa akaamua kuweka namba zake hewani ili Imaculata akisikia ampigie.Na ndani ya wimbo huu Jerry kachanganya kidogo na kijaruo kuonyesha tu hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo juu ya binti huyo.

Nyimbo nyingine alizoimba Jerry Nashon kwa hisia kali za mapenzi ni pamoja na; Sarah nyota ya uzuri,mama Shani,Pesa bado zanisumbua,Neema,VIP,Thereza,Top queen nk.
"Ni mahali gani ulipooo, nijulishe , nipigie simu namba 26561!
 
Immaculata_ Bima Lee

Haloo Immaculata mama
Vipi Immaculata mama
Nakutafuta sikuoni mama
Napiga darubini sikupati mamaa
Napiga tarumbeta sikupati mamaa

Ni umbali gani ulipooo
Nipigie simu namba 26561

Hakyamungu nakupenda Immaculata natoka jandoni mama nishike mkono nipeleke mbele ya wazee

Nafanya nini nderakendr ?

Nakupendaaaa aa.................. Endelea mwenyewe

Hapo unawakuta jamaa waliotoka NGINDE Mulenga "Spoiler" gitaa la Solo, Mwanyiro "Computer" Bass Gitaa, Abdallah Gama, Rhythm Guitar wakiambatana na Shabaan Dede huku wakiwakuta wenyeji Nguli mwenyewe Jerry Nashon Dudumizi akina Roy Bashekanako, Momba "sauti ya chuma" etc

Huo ulikuwa muziki halisia wa Kitanzania na ubunifu wa hali ya juu bila kusaidiwa na Kompyuta!

usisahau ule wimbo maarufu , SHANGWE YA HARUSI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! , DEDE DAMU YA KUNGUNI HUYO
 
Hakika ya kale ni dhahabu.
Siyo kwamba wengi tunaopenda muziki wa enzi hizo ni wazee.La hasha.Wengine bado ni vijana tu ila tulikuwa tukiachiwa radio na baba zetu ndio sababu tukatokea kuupenda muziki huo.Kumbuka enzi hizo radio ilikuwa ni ya baba tu labda na mama kidog😵le wako ukutwe umefungua radio bila ruhusa.Enzi hizo vifaa vingi vya ndani kama fenicha,masufuria nk. vilikuwa na jina la mmiliki !
Pamoja na mazingira ya namna hiyo watu tulikuwa tunafuraha sana moyoni.Ukijua baadaye kuna kipindi cha muziki,kazi yako ni kuanika betri juani ili baadaye usikilize muziki.Binafsi kuna vipindi kama club raha leo show,ombi lako,top ten show,chaguo la msikilizaji na misakato nilikuwa sivikosi.Yote tisa,kumi ilikuwa bendi ije mkoani sasa halafu iwe inapiga uwanjani.Mji mzima unahamia hapo uwanjani.Msio na kitu mtabaki nje mpaka muda wa fungulia mbwa lakini bado tulikuwa tunaona poa tu.
 
Back
Top Bottom