peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 13,599
- 22,529
Manispaa ya Moshi chini ya Sheria ndogo za (ada na ushuruj ya Mwaka 2019, Tangazo in Serikali Na. 148 la Tarehe 15/02/2019, imeainisha ada na tozo mbalimbali katika kuendesha sherehe kwenye kumbi na maeneo ya starehe.
Mchanganuo wa ada na tozo hizo ni kama ifuatavyo;
- Tshs. 60,000.00, Kibali cha kufanya sherehe
- Malipo kutoka kwa mpambaji wa sherehe Tshs. 50,000.00 Tshs. 50,000.00
- Malipo chakula na vinywaji Tshs. 30,000.00
- Mshercheshaji wa sherehe (MC) Tsh. 30,000
- Mpiga picha wa sherehe Tshs. 20,000.00
- Muziki Tshs. 20,000,00
Fedha hizi zinatakiwa kulipwa na Mwenye sherehe ndipo apatiwe kibali cha kuendesha sherehe husika. Aidha mmiliki wa Ukumbi anapaswa kuhakikisha kwamba Mwenye sherehe anakupatia nakala ya kibali kabla ya kumruhusu kutumia Ukumbi. ANGALIZO: Iwapo wakala hatakuta kibali ukumbini, sherehe itazuiwa kufanyika kuanzia muda huo.
Kwa barua hii namtambulisha kwenu ULOFAMO AUCTIONEER AND COURT BROKERS LTD, wakala atakayehusika na usimamizi wa ukiukwaji wa ada na tozo tajwa kifungu cha 3 hapo juu.