WanaJF, mimi niko nje lakini najitahidi kukaa karibu na mikoa yote ya Tanzania kupitia mitandao mbali mbali kama hii, najaribu kuifutilia breaking news toka kwenu na vyanzo vingine vya habari. karibu wiki nzima nimejaribu kuhoji watu mbali mbali katika mikoa ya mbeya(kuna marafiki), Dodoma(kuna marafiki), Shinyanga [Kahama na Kishapu(Home)], mwanza(Nilisoma), Tabora (nilisoma), Dar es salaam ( ninakofanya kazi), Arusha (nimefanya kazi), na Manyara( nimefanya kazi). Watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea ndo maana wenye vijarida vyenye vituko wanauza, haviitaji kufikiria sana ni kucheka tu na kusisimuka basi.
Kote huko nilikuwa naulizia jinsi Chadema ilivyojipanga au upinzani ulivyo nanguvu, cha kusikitisha mkoa wangu (Shinyanga) wanasema wanataka chama cha Nyerere. Iliniuma sana lakini nitafanyeje! nikabaki kutafuta sababu tu, ambayo nimeona niiweke hapa! CCM imefanikiwa kukaa muda mrefu kwa kuwanyima watu elimu bora, inawapa watu elimu ya kuendeleza umasikini badala ya kuwaondelea umaskini.
Inauma sana kuona mkoa kama shinyanga unakuwa ni kama jimbo la CCM vile. kwa hiyo chadema au vyama vya upinzani tuna kazi, ilani najua itasaidia kwa wajanja wachache, lakini kwenye mikoa kama shinyanga nadhani kuna haja ya kuwafanyia utafiti kabla ya kampeni ili kuweza kuwapa upeo.
Hiyo ni shinyanga, lakini kuna maeneo kibao,mikoa mingi ya namna ambayo ni kama majimbo ya ccm watu hawaelewei, wanatishiwa vita kama vya rwanda, wanaohongwa, wanaokamatwa na kubambikwa kesi yaani ni uonevu kwenda mbele. Lakini yanawezekana, maisha bila ccm yanawezekana kabisa. TWENDE KAZI chadema.