Ila hivi vyeo hivi! Ishi na watu vizuri tu. Leo Gambo ni mwananchi wa kawaida kama wewe

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,995
2,000
Nimekaa nikatafakari sana, zile Salute, protocals, mashabiki, misafara, ving'ora, amri leo vyote vimezimika gafla kama mshumaa, hawezi kuamrisha tena, hawezi kutoa maagizo kwa yeyote zaidi ya familia yake, hana wa kumgombeza tena, kwa ufupi Gambo hapo alipo ni mwananchi wa kawaida kabisa kama ulivyo wewe msomaji wa Thread hii, hana previlage tena, vipaumbele vimetoweka gafla.

Hapa nimekuja kuamini, busara, utu, ukarimu, hekima, heshima ni vitu vya muhimu sana kwa yeyote yule atakaye pata mamlaka

Mamlaka ni ya muda tu ..Ishi na watu vizuri.
 

livafan

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,640
2,000
Ulikuwa hujui kuwa yeye ni mwanainchi, itakuwa alikuwa mkimbizi kimbindi akiwa rais wa mkoa !
 

nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,913
2,000
Mimi sisi kama gambo.Sijawahi kutenda,kufikiri wala kujikweza.Nitakuwaje kama yeye? Bado wawili na kibosile wao(alikuwepo Bokassa,Mobutu,Saddam,n.k)
 

pasi padinde

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
248
500
Awe mjasikiamali wa kilimo

Au awe ustaadh afundishe madrasa
Itamsaidia. Au awe mwanachama invisible wa vyama vya upinzani awasaidie mbinu ili wawe wanampa mpunga kimya kimya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom