Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,904
- 129,047
Huwezi zuia analysis ya matukio yaani hata ukijikwaa mbele ya kijiwe lazima watu waongelee hilo. Acha wapiga kura wajadili sababu viongozi wakijua kuwa wanaangaliwa hadi na sisimizi wapo watakaobadili nyendo na utendaji wao. . .
Mijadala iendelee bila kashfa, matusi wala kejeli
Bora umemwambia huyo, hapa jukwaani kuna kundi liko hapa kuhakikisha eti kila anachofanya Magufuli anasifiwa na usiposifia basi wewe sio mzalendo!! Nikasema sidhani kama kusifia tu ndio kumjenga tena unaweza kukuta sisi tunaomponda kwa kiwango kikubwa ndio tunamfanya awe bora maana ili kutukata ngebe inabidi afanye kweli. Nakumbuka Obama aliwahi kusema kwenye kuitumikia America atasikiliza watu wake na hasa wale wapinzani wake maana wale ndio watampa ukweli bila kujipendekeza. Ila wengi wa hawa wanaosema asifiwe wanafikia hatua ya kutishia eti yeye sio kama JK na kwamba akikashifiwa atakuwa dictator!! Akiwa na dictator kwa kufanya chini ya kiwango ndio atazidi kutufanya ile asiimia 40 ya upinzani kupanda kuwa 50+. Yeye afanye kwa ubora wake sifa zinakuja automatically na sio kwa kulazimisha.