Ikulu mpya na maswali

Ikulu mpya na maswali

Kwa kweli wakati Mama anasema wanajenga Samia complex nilishtuka, nikajikuta nimenyong’onyea sana! Bora hata asingesema kwenye public!
Kiufupi mabilioni yetu yanatafutiwa njia za kuyapiga na watu wachache!
Hiyo ikulu hata bajeti yake hawataki kuiweka wazi!!!
Wangeianika tuone maajabu!!
Mawazo ya kimasikini hayo.
 
Je, kuna ulazima wa yafuatayo au ni kupoteza pesa za walipa kodi?
  1. Kujenga Njia ya Kuruka Ndege Ikulu.
  2. Ujenzi wa Viwanja vya Golf.
  3. Ujenzi wa Complex ya watu 2000-3000
NB: Kama wanatimiliza Ndoto ya Nyerere kwanini Complex isiitwe Nyerere Complex au iitwe aliyeanzisha Ujenzi Magufuli Complex. Kwanini iitwe Samia Complex?

Je, Watanzania tuna kodi kiasi hicho kujenga Ikulu ya namna hiyo? Kuna ulazima gani?

Je, nani mnufaika wa hayo yote?

Kwanini hizo pesa zisiende kwenye elimu ya awali na msingi maana huko ndo chanzo cha madudu ya huku juu?
Wajenge viwanda, Hospitali n, shule na masoko hapo ikulu.
 
Jana Samia kaongea kuwa Ikulu bado kuna mambo yanafanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya kurukia Ndege

Ndege zenyewe zipi? Uwanja complicated wa msalato nao unasubiri, ni hizihizi kodi zetu au?

Well
Vipaumbele vya nchi yetu miaka ya karibuni ni vipi? Elimu ujinga na maradhi vimeisha?

Maana enzi za Mzee Mkapa kila mwisho wa mwezi tulikua tunakumbushwa na kupewa updates where are we heading to…
 
Wajenge viwanda, Hospitali n, shule na masoko hapo ikulu.
Matumizi mabaya ya ardhi na kodi yetu.
Ipo siku atajitokeza mtu atapunguza eneo na kujiuzia
 
Ndege zenyewe zipi? Uwanja complicated wa msalato nao unasubiri, ni hizihizi kodi zetu au?

Well
Vipaumbele vya nchi yetu miaka ya karibuni ni vipi? Elimu ujinga na maradhi vimeisha?

Maana enzi za Mkee Mkapa kila mwisho wa mwezi tulikua tunakumbushwa na kupewa updates where are we heading to…
Hii nchi haina viapumbele
 
Je, kuna ulazima wa yafuatayo au ni kupoteza pesa za walipa kodi?
  1. Kujenga Njia ya Kuruka Ndege Ikulu.
  2. Ujenzi wa Viwanja vya Golf.
  3. Ujenzi wa Complex ya watu 2000-3000
NB: Kama wanatimiliza Ndoto ya Nyerere kwanini Complex isiitwe Nyerere Complex au iitwe aliyeanzisha Ujenzi Magufuli Complex. Kwanini iitwe Samia Complex?

Je, Watanzania tuna kodi kiasi hicho kujenga Ikulu ya namna hiyo? Kuna ulazima gani?

Je, nani mnufaika wa hayo yote?

Kwanini hizo pesa zisiende kwenye elimu ya awali na msingi maana huko ndo chanzo cha madudu ya huku juu?
Uwivu huoo hamtaki na sisi viongozi wenu tuanze kujifunza na kucheza golf ikulu..
Mibongo inawivu sana na roho ya kimasikini
 
Usiposema samia complex utahalishaje upigaji wa fedha? Yaani hapo upigaji umehalishwa. Ni mwendo wa kula tu.

Huyu mama kwakweli anawaangusha sana wanawake wenzie kiuongozi.
CCM wenzio hao
 
Kila mtu anataka jina lake liwepo hapo tena kwa kujipigia chepuo mwenyewe mara Zanzibar mara Nungwi golf courts.

Hivi mfano Nyerere aliacha vitu gani vikiitwa kwa jina lake alipokuwa madarakani? Barabara?

Vingi vimepewa jina lake na watu Baki akiwa mstaafu au marehemu.

JNIA yenyewe aliiacha ikiitwa DIA hadi 2005.

BTW:Eneo lenyewe wamehodhi kubwa mno ekari 8,473 zote za nini si heri wangewapa vijana wa maigizo ya kilimo ya BBT ya Bashe.
 
Ukiona mtu yoyote katia neno kwanini pesa hizo zisiende kwenye elimu ujue mwisho wake wa kufikiri umeishia hapo. Ngoja nikujibu kwa urahisi tu, Ikulu ya nchi ni hazina ya nchi na itabaki hata vizazi vinayokuja ni muhimu kuwa na sehemu bora ya kufanya shughuli za serikali wala sio kupoteza pesa kwa mawazo yako maana ni kama kusema budget ya nchi 100% iende kwenye shule tu huu ni ujinga kila kitu kinapangwa kwa budget na elimu ina budget yake. Ukisema kodi kwani uliambiwa kodi yako inaongezake kulipia ujenzi? acheni gubu hata wewe unaweza kumuita mtoto wako Magufuli. Stand Magufuli, Mji wa serikali Magufuli na mpaka ikulu Magufuli imekuwa nini tena, Nyerere jina lake liko kila sehemu mimi naona tubadilishe nchi jina tu kutoka Repuclic of Tanzania to Republic of Nyerere au Magufuli

Ikulu = hazina ya nchi?
Wenzetu hua mnatumia ubongo upi kutoa arguments kama hizi? Muulize Mzee Kagame Ikulu iko wapi? Unadhani hawezi kujenga ikulu ya maonyesho?
 
Kila mtu anataka jina lake liwepo hapo tena kwa kujipigia chepuo mwenyewe mara Zanzibar mara Nungwi golf courts.

Hivi mfano Nyerere aliacha vitu gani vikiitwa kwa jina lake alipokuwa madarakani? Barabara?

Vingi vimepewa jina lake na watu Baki akiwa mstaafu au marehemu.

JNIA yenyewe aliiacha ikiitwa DIA hadi 2005.

BTW:Eneo lenyewe wamehodhi kubwa mno ekari 8,473 zote za nini si heri wangewapa vijana wa maigizo ya kilimo ya BBT ya Bashe.
Uliambiwa kuna uhaba wa maeneo ya kulima?
 
Kwa nini iitwe majina yao kwanza huu ujinga wa kuita majina yao kila sehemu nao uangaliwe..na waite hata Tanzania complex au kodi zetu complex
 
Hatari sana what for? Wangeweka tu kiwanja cha helicopter ingekuwa poa tu. Afrika tuna shida mahala viongozi wanataka kufanya mambo kama donor country tena unakuta donor country hata hawafanyi hivyo. Just imagine ni pesa kiasi gani itatumika kuitunza hiyo complex kwa kila mwezi?
Kuna Ikulu duniani yenye uwanja wa ndege au wana taka wawe wa kwanza
 
Kifurushi cha bima ya watoto yenyewe wameshindwa. Kisha mmama mtu mzima wanayemuita rais anashangilia kujengwa kiwanja kwa golf sababu anajua wajukuu zake watatibiwa ulaya.

Na westerners hua wanafurahi sana wakizikopa nchi za africa alafu wakaona zinafanya mambo kama haya hua wanaongeza na rate za mikopo kabisa ili tukope kwa wingi wazidi kumiliki nchi.
 
Ikulu = hazina ya nchi?
Wenzetu hua mnatumia ubongo upi kutoa arguments kama hizi? Muulize Mzee Kagame Ikulu iko wapi? Unadhani hawezi kujenga ikulu ya maonyesho?
Sasa wewe na akili zako zote unatufananisha na kile ki mkoa Rwanda? kweli tunawatu akili zao zina changamoto, leo hii sisi wakutuweka kundi moja na Rwanda ya Kagame kwa lipi haswa? Hii Tanzania na EA mtu wa kushindina naye ni Kenya. Halafu toka lini nchi tukaweka vipaumbele vyetu kwa kuangalia Kagame anafanya nini. Usitukoshee heshima kama nchi kutufananisha na nchi kama wilaya yetu. Hata kama unachuki zako na Mama Samia uko umeenda mbali. Nchi yoyote ni lazima uwe na airport nzuri, Immigration nzuri, ofisi za serikali nzuri na ikulu nzuri ndio sura ya nchi mengine yatakuja.
 
Back
Top Bottom