Ikulu mpya na maswali

Ikulu mpya na maswali

Ni kweli tunahitaji shule sio UMEKASILIA ni UMEKASIRIKA mimi nikiona mtu anachanganya "L" na "R" basi nguvu zinaisha.

Dunia nzima ni masikini.

Hata huko ulaya masikini wapo.

Hata serikali iseme bajeti yote ipelekwe kuondoa umasikini haitatosha hata miaka 100 ijayo.

Wacha vingine vifanyike

Ni kweli tunahitaji shule sio UMEKASILIA ni UMEKASIRIKA mimi nikiona mtu anachanganya "L" na "R" basi nguvu zinaisha..
Hayo Ni Makosa ya Kiuandishi hata BBC CNN wanakosea Nenda Kwenye Point inaonekana Na Wewe Kuna Mrija unafyonza Mema ya Nchi Alaf unakuwa Mkali inabidi tule Wote Au Tujenge Nchi Yetu Sote ????
 
Kipindi Cha Kikwete Bajeti ya Chai Ikulu Ilifika Bilion Kadhaa Sasa hata Hapa Kweli Tusihoji Majizi Hayataisha Mpaka Yafukiwe Kabulini
 
Sasa kaangalie budget ya miundombinu, elimu na maji imepunguzwa? acheni gubu wewe umeanza kujenga nyumba ya kuishi au ulichimba kisima kwanza...
Tunahitaji bajeti itumike zaidi kwenye vipaumbele vya msingi na mambo ya msingi,,,,Ikulu ina faida gani kwa dunia ya sasa??,,,uchumi kwa jamii,, wananchi na nchi kiujumla haukuzwi kwa kuwa na ikulu nzuri na kubwa,,,ni ufahari wa kijinga na hulka za kijinga za viongozi,,,Viongozi inabidi wawe na maono bora ya kulijenga Taifa kwenye sekta na mambo ya msingi na sio kujenga ikulu!!!
 
Nchi inaongozwa na Mapaka👇😁😁😁
AEb8rsjc_1.png
AEb8rs.jpeg
16525976734300.jpg
ummY_jc.jpg
 
Hayo Ni Makosa ya Kiuandishi hata BBC CNN wanakosea Nenda Kwenye Point inaonekana Na Wewe Kuna Mrija unafyonza Mema ya Nchi Alaf unakuwa Mkali inabidi tule Wote Au Tujenge Nchi Yetu Sote ????
Hapana L na R ni issue kubwa Tanzania, sasa twende kwenye hoja kwanza mimi kwa bahati nzuri sio mtu anayenufaika na system kabisa wala sina hata ndugu labda yuko serikalini huo ndio ukweli lakini katika uhalisia tu, Mimi kama najenga nyumba yangu na watu wengi tu huwa wanatumia pesa nyingi kuiweka sitting room katika ubora zaidi ipendeze sababu wageni wako wakija ndio sehemu watafikia na unataka wafurahi huwezi kuwekeza pesa nyingi kwenye store kwa maana kama una Million 100 ya kujenda labda 40% kipaumbele sitting room na serikali ni hivyo hivyo huwezi kuwa na Ikulu haina hadhi kama nchi. Mtu angesema tubane matumizi kwenye manunuzi ya magari mapya kwamba gari ili ibadilishwe kuwa na criteria muhimu sio model maana ziko gari bado ziko vizuri tu lakini wanatumia vigezo vya model na kupunguza misafara mikubwa ya viongozi ziko sehemu nyingi zakubana matumizi yasiyokuwa na ulazima ila lazima tuwe na ofisi za wizara bora, Bunge bora, Mahakama, airport bora na Ikulu bora na immigration office bora sababu ni uso wa nchi ile ya kurasini haina hadhi kabisa kwa nchi yetu nadhani Dodoma inajengwa kitu chenye hadhi. Hebu angalia mahakama ya kisutu ni wakati wa ku move on, hizi nyumba zinajengwa mara moja ni kama wewe ukiamua kujenga jenga nyumba nzuri sababu hutajenga kila siku.
 
Ni upuuzi wa kiwango cha lami binafsi Kodi yangu watachukua kwa kunishurutisha daima. mpaka ccm waondoke madarakani....ameen!!
 
Tutachukua muda sana kuendelea ,viongozi ni wabinafsi sana ,hawaangalii mateso wanayoyapata waTZ kwa kuwatoza mikodi ya kufa mtu halafu hizo fedha wanaenda kuzitapakanya! Ni ujinga mnatenga kila mwaka biioni 580 kununua magari halafu baada ya mwaka viongozi wanayanunua kwa milioni 2 hadi 3 wakati bajeti moja ni 400m.


Viongozi wetu Wametoka kwenye jamii zetu.
Sisi na Viongozi wetu ni watu wa jamii moja.

Tabia za Viongozi wetu zimejengwa na zinaendelea kujengwa na sisi wenyewe kwa maana sisi ndio Jamii yenyewe.

Matendo Yao na fikra zao ni zile zile sawa Sawa na sisi wananchi. Mchawi anajulikana!
 
Kumbe wanajenga na njia ya ndege!
Nadhani eneo la ikulu yetu litakuwa kubwa kuliko hata Marekani halafu eti sisi ni masikini!
Mkuu hata ukiangalia jengo la bunge la Uingereza ni Dogo mno yaani inaweza kuingia kama Mara nne kwenye bunge letu

Wenzetu wanachoangalia ni LENGO hasa na sio muonekano wa nje

Hii nchi hii ina mambo ya kushangaza sana
 
Hivi utaelewa lini?

Nchi kama Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye maeneo yatoyoinua maisha ya watu. Sasa wewe unashangilia ikulu kuwa na ranch, kwanini hio ranchi isijengwe kwa ajili ya watu wote? Kwanini ijengwe ikulu?
Au hio pesa kwanini usikopeshe wajasiriamali kuwaongezea mitaji? Au kwanini usitumie hio pesa kuwapa punguzo la bei za umeme kwa watu wenye viwanda vidogo walioanzisha viwanda Vipya? Au unafikiri tutaumalizaje umaskini kama hatujui jinsi ya kutumia pesa ndogo tulizonazo?
Unajua kinachoendelea kwenye ule mgawo wa 4:4:2? Wananchi wa Tanzania hatujajielewa bado!
 
Back
Top Bottom