Ikulu Dar: Rais Yoweri Museveni na Rais Samia Suluhu washuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

========

Shughuli inaanza kwa nyimbo za Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki. Gerson Msigwa anaanza kwa kutoa ufafanuzi wa wingi wa mikataba inayosainiwa kwenye bomba hilo.

Msigwa amefafanua mkataba wa leo ni makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na kampuni itakayotekeleza mradi, amesema miradi mikubwa kama huu wa mafuta unaohusisha zaidi ya pande moja huambatana na utiaji saini wa mikataba kadha kadha hivyo hakuna kujirudia kwa utiaji saini wa mikataba.

Mkataba wa bomba la mafuta umetiwa saini na waziri wa nishati, Medard Kalemani shuhuda akiwa mwanasheria mkuu wa Tanzania, Prof. Kilangi na kwa upande wa kampuni ya EACOPP ni mkuregunzi mkuu wa kampuni hiyo, Martin John na atashuhudiwa na rais wa utafiti na uzalishaji wa Total Afrika, Nicholaus Teraz.





Rais Samia Suluhu Hassan
“Rais Museveni sio Mgeni Tanzania, ameishi hapa, amepata Elimu yake ya Chuo Kikuu hapa na hata baadhi ya Watoto wake amepatia hapa kwahiyo huyu ni nusu Mtanzania na nusu Mganda, tunamkaribisha sana”

“Hayati Magufuli na Museveni walianza mchakato wa mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima - Tanga na Mimi nimekuja kuuendeleza, mradi huu una faida nyingi ikiwemo pia kuwapatia ajira Wananchi wetu”

“Nakushukuru Rais Museveni kwa kuja licha ya changamoto ya Corona, asante nilikuwa na wasiwasi ila umenithibitishia nyumbani ni nyumbani,najua umekuja kutokana na uzito wa mradi huu wa bomba la mafuta, Watanzania wamesikia maneno kwa miaka 5 tuache maneno tukatekeleze”

“Kuna mambo yanashangaza kulikuwa na sheria wote tusajili laini tuweke vidole ili Mtu akifanya utapeli ajulikane lakini utapeli wa mtandao unaendelea na Watu hawafikishwi Mahakamani, sasa ule usajili ulikuwa kiini macho au nini!? Maana wote tumesajili na majina yapo.

Yoweri Museveni
“Mimi naelewa kiswahili lakini nimesafiri na Wazungu weusi nilionao hapa kutoka Uganda wanajifanya hawaelewi Kiswahili na masikio yanawauma kwa vitu walivyoweka masikioni”

“Sekta muhimu nne ni Kilimo ambacho utapata chakula na utajiri, sekta ya pili ni viwanda, sekta ya tatu ni service (huduma), sekta ya nne ni ICT, sekta hizi zinataka miundombinu kama barabara, umeme, nishati na hizi sekta zote haziwezi kuendelea bila soko”

“Wananchi wa Uganda na Tanzania wasilewe na sekta ya mafuta na gesi wakasahau sekta nyingine kama kilimo, ICT, viwanda n.k, kwasababu mafuta yanaisha lakini kilimo, utalii vinaendelea kwahiyo tutumie rasilimali zenye ukomo kuendeleza rasilimali endelevu”

========

Pia soma

IMG_20210520_172620_535.jpg
IMG_20210520_172624_888.jpg
IMG_20210520_172628_585.jpg
IMG_20210520_172630_635.jpg
IMG_20210520_172633_989.jpg
IMG_20210520_172638_884.jpg
IMG_20210520_172642_965.jpg
IMG_20210520_172706_098.jpg

IMG_20210520_172716_946.jpg


IMG_20210520_172733_200.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku 1 hapa nchini kwa Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini Mhe. Rais Museveni na Mhe. Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni za uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement) utakaofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

1621486689671.png
 
Rais wa #Uganda, Yoweri Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku moja leo Mei 20, 2021 kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan

Akiwa Nchini, Rais Museveni na Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa Mikataba ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Bandari ya Tanga, kati ya Serikali ya #Tanzania na Kampuni za Uwekezaji katika mradi huo (Host Government Agreement)

MY TAKE:

Hii Mikata kuhusiana na hili bomba ipo Mingapi na tutamaliza kuisaini lini ili bomba lianze kujengwa?
 
Mambo ya ujenzi bomba la mafuta kutoka Ohima Kwa M7 yanaendelea!

Hongereni viongozi wetu Kwa kudumusha ushirikiano wa kiuchumi Kwa nchi zetu hizi!
 
Magufuli alisaini Mara mbili Uganda na Mara mbili Tanzania moja chato na moja dar es salaam samia hii itakua Mara ya pili moja Uganda na hii sasa Tanzania, inaonyesha hizi nchi haziaminiani.
Yawezekqna ile ya JPM imetoka, kama ataingia rais mwingine nae atasaini.
Ila mama awe mwangalifu asiingizwe cha kike
 
Back
Top Bottom