Ikulu, Dar: Rais Samia akutana na Freeman Mbowe

imekufa hiyo

Hii ndio aina ya siasa tunayoitaka Tanzania. Scientific politics. Kukubali siasa ziondoe ubinadamu wetu ni tatizo kubwa lililokuwa linatunyemelea. Safi kabisa.

Mungu wa Chato ndio muasisi wa hizo siasa mbovu.
 
Kabla ya jana alikuwa anatambua nani ndiye Rais?!
CHADEMA hajawahi kutambua kuwepo kwa serikali toka 2020- 18/2 Mbowe alipoletwa mahakani si mliimba pambio- rais rais- unajitoa ufahamu
 
Kamanda Mbowe katika utulivu wake amekutana na mama Samia Suluhu katika ikulu ya Magogoni:

Kwa hakika salamu hizi za kheri ziwafikie maadui wetu wote ndani na nchi yetu.

Hili likawe somo zaidi ya nadharia zisizokuwa na mashiko za nani kuitwa adui na nani kujiita mwenyewe kuwa ni mzalendo.

Kamanda Sirro, ACP Kingai na wenzenu zingatieni haya:

"nchi hujengwa hivi na hubomolewa kupitia njia mliyokuwa mkitupeleka."

Tambueni ni nia njema bado kufahamu alipo mtanzania mwenzetu Moses Lijenje.

Heko mama Samia, Heko Freeman Mbowe.

Nini kama maridhiano?
 
Kwa mama Kila goti litapigwa, umemuona Mbowe alivyokunja mikono kwa unyenyekevu?
 
Ni muda wa kwenda kuifanya siasa inayohitajika kukidhi malsai ya jamii... na ni muda wa kwenda kuipata KATIBA mpya.
 
Kwa vile hukukaa ndani wewe,Mbowe atapumzika kwanza kwasababu ile nia imeahirishwa tuv
Sio nia kuahirishwa bali kesi imefutwa sio kwamba imewekwa pending.

Ndo maana wameachiwa huru bila masharti youote. Kama kuachiwa kwao hiru pangeambatana na masharti kadhaa basi hapo uwezekano wa kesi kuja kuendelea ungekuwepo endapo wangekiuka masharti.

Hapo kesi imefutwa na washindi ni akina Mbowe.
 
Mbowe ni mwanasiasa yote hayo ila uso una afya.

Wale magereza waliokula chakula chao wapeni salaam
 
Sio nia kuahirishwa bali kesi imefutwa sio kwamba imewekwa pending.

Ndo maana wameachiwa huru bila masharti youote. Kama kuachiwa kwao hiru pangeambatana na masharti kadhaa basi hapo uwezekano wa kesi kuja kuendelea ungekuwepo endapo wangekiuka masharti.

Hapo kesi imefutwa na washindi ni akina Mbowe.
CPA 91 inasema pia aweza kukamatwa na kushitakiwa upya
 
CHADEMA ndio waliokuwa wa kwanza kuomba kukutana na Rais Samia ndipo msajili na Zitto wakaja na maigizo yao kupitia TCD kufunika na kuvuruga!
CHADEMA hajawahi kutambua kuwepo kwa serikali toka 2020- 18/2 Mbowe alipoletwa mahakani si mliimba pambio- rais rais- unajitoa ufahamu
 
CHADEMA ndio waliokuwa wa kwanza kuomba kukutana na Rais Samia ndipo msajili na Zitto wakaja na maigizo yao kupitia TCD kufunika na kuvuruga!
Sasa ile RAIS RAIS siku ile ilikuwa ya nani? Mbunge wa Nkasi manamtambua- acheni uchuro basi
 
Endapo kuachiwa kwake kumeambatana na masharti.
Hakuna masharti ni sheria inasema hivyo
91.-(1) Katika kesi yoyote ya jinai na katika hatua yoyote ile
kabla ya hukumu au uamuzi, kama itakavyokuwa, Mkurugenzi wa
Mashtaka anaweza kuweka nolle prosequi, aidha kwa kueleza
mahakamani au kwa kuiambia mahakama husika kwa maandishi kwa
niaba ya Jamhuri kuwa mwenendo hautaendelea; na baada ya hapo
mtuhumiwa ataachiwa mara moja kuhusiana na shtaka ambalo nolle
prosequi imewekwa na kama amepelekwa gerezani atatakiwa
kuachiwa, au kama yuko chini ya dhamana wadhamini wake
watakoma kuwa wadhamini; lakini kuachiwa huko kwa mtuhumiwa
hakutachukuliwa kama kizuizi kwa mashtaka mengine ya baadaye
dhidi yake kwa kutumia maelezo hayo hayo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom