Ikulu, Chamwino: Rais Magufuli ateua Baraza la Mawaziri lenye Wizara 23. Aunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Kuna nini kimetokea kwa Dk Ashatu kijaji? huyu ni msomi mzuri wa Uchumi na ingekuwa bora kuungana na Dk mango katika wizara ya fedha, yaani unachagua akina katambi unamuacha Dk Ashatu? sioni logic.
 
uwaziri sio sadaka/zawadi bali ni mzigo/majukumu mazito ya kuwatumikia watanzania zaidi ya 60million, ukitazama kwa jicho hilo sidhani kama utashangilia wala aliye kosa kamwe hawezi kulalamila, ukimuona mtu analalamika kwa kukosa uteuzi wa uwaziri basi jua kuwa huyo alikuwa na malengo binafsi ya kujinufaisha yeye sio watanzania na ukimuona yeyote anashangilia kwa kupata uteuzi basi ujue kuwa huyo haendi kuwatumikia watanzania zaidi ya tumbo lake na ndugu,
Wewe unaandika ujinga hapa kama hupo Tanzania ambako ili mtu apate Uwaziri unaodai ni mzigo, anatoa rushwa kwa wajumbe wa Chama chake ili wampendekeze agombee Ubunge.

Akisha pendekezwa anatoa rushwa kubwa zaidi kwa wapiga kura ili wamchague kuwa Mbunge wao kwa mategemeo kuwa akisha pata nafasi hiyo, Uwaziri unakuwa karibu nae kwa sababu Waziri lazima awe Mbunge.

Pesa anazotumia kutoa rushwa anazipata kwa kuuza mali yoyote ya familia yake akijua kuwa asipochaguliwa itakuwa kilio na kusaga meno familia nzimà kwa miaka mingi lakini ubunge mtamu na Uwaziri mtamu zaidi.

Akichaguliwa kuwa Mbunge tu anakopa pesa ya kutosha, atarudisha akiapishwa, atakwenda na bulungutu la hizo fedha kwa mganga mashuhuri ili kwa gharama yoyote amtengenezee dawa ateuliwe kuwa Waziri.

Baada ya kumalizana na mganga akingoja uteuzi, ataanza kumsifia, kumtukuza na kulamba miguu ya anayeteua akifanya yote haya ili apate UWAZIRI. Wewe mjinga unasema eti ili awatumikie wananchi!
 
Kwani lazima wawepo?

Makabila 126 yataingiaje kwenye cabinet ya watu 30 or 40?

Msijikweze sana maana inawezekana kuna Makabila tangu uhuru hayajawahi kutoa walau Naibu Waziri

Ukiondoa Jakaya kuna Mkwere kishawahi kuwa Waziri au Naibu waziri tangu uhuru? Mbona tupo kimya tu
Prof.Ibrahim Msabaha,Shukuru Kawambwa,n.k.
 
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kuhusu Uteuzi uliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo tarehe 05 Desemba 2020



========
Rais Magufuli pia amewateua kuwa Wabunge Dkt. Dorothy Gwajima(Alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Afya) na Dkt. Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi).

Pia Rais Magufuli ameunda Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Orodha ya Mawaziri kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi.

1. Wizara ya Maji - Juma Aweso

2. Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo - Innocent Bashungwa

3. Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu - Jenister Mhagama

4. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Dkt. Doroth Gwajima

5. Wizara ya Uwekezaji ofisi ya Rais - Profesa Mkumbo Kitila

6. Wizara ya Katiba na Sheria - Dkt. Mwigulu Nchemba

7. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Profesa Joyce Ndalichako

8. Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Mashimba Mashauri Ndaki

9. Wizara ya Maliasili na Utalii - Dkt. Ndumbalo Damas

10. Ofisi ya Rais TAMISEMI -Suleiman Jaffo

11. Wizara ya Madini - Dotto Biteko

12. Wizara ya Nishati - Dkt. Medard Kalemani

13. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho

14. Wizara ya Kilimo - Profesa Adolph Mkenda.

15. Wizara Viwanda na Biashara - Mwambie Geofrey Idelphonce

16.Wizara ya Mambo ya Ndani - George Simbachawene

17. Wizara ya Muungano na Mazingira - Ummy Mwalimu

18. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari - Dkt Faustine Ndugulile

19. Wizara ya Fedha na Mipango - Dkt. Philip Mpango

20.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Profesa Paramagamba Kabudi

21. Wizara ya Ardhi na Makazi -William Lukuvi

22. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Elias John Kwandikwa

23. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Capt Mstaafu George Mkuchika


Manaibu Waziri

1. Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka

2. Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula

3. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi

4. Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi

5. Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis

6. Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar

7. TAMISEMI- Dk Festo Ndugange

8. Wizara ya Nishati- Stephen Byabato

9. Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi

10. Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew

11. Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul

12. Wizara ya Madini- Ndulane Kumba

13. Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya

14. Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga

15. Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi

16. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Abdallah Ulega

17. Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara

18. Wizara ya Mambo ya Nje- William Olenasha

19. Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja

20. Ofisi ya rais TAMISEMI- David Silinde

21. Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe

22. Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel

23. Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo

View attachment 1642517
View attachment 1642518
View attachment 1642519
View attachment 1642520

Well noted
 
Back
Top Bottom