Sweya Makungu
JF-Expert Member
- Jun 11, 2023
- 479
- 556
Ikiwa Mazishi ni Ibada , Basi Usiingilie Ibada za Wafu . Waache Wafu Wawazike Wafu Wenzao..
💫💫💫💫💫
©️Mwl. Makungu m.s
0743781910
Wana Heri wafu wafao katika Bwana. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa Matendo yao yafuatana nao ( ufunuo 14:13).
Maana wafu wote wanalo tumaini ya kuwa Siku moja watatafufuliwa . Lakini ni wafu wachache walio na uhakika wa wapi wataelekea baada ya kufufuliwa.
Ni utamaduni wetu wa kuziosha maiti na kuzisafisha na kuzivalisha suti au sanda . Lkn yote hayo ni maandalizi ya kuzifukia chini ya udongo.
Nenda kaizike maiti , lkn usiingilie ibada za wafu.
Huwa tunazika maiti, lkn hatuziki wafu. Wafu hawafi. Wafu wanaishi . Pengine hujanielewa Bado . Ni hivi , huwa tunazika miili ya wafu lkn hatuwaziki wafu. tunazika mwili lkn hatuziki nafsi . Nafsi haifi.
Umepata kusoma kisa cha Lazaro na tajiri ktk Biblia? Wote wawili walikuwa wafu . Miili yao iliishazikwa zamani duniani . Lakini wanaonekana wako mahali fulani tofauti wakiwa hai wanajadiliana . Mmoja anastarehe mwingine anataabika. Miili inakufa ,maiti zinazikwa , lakini Wafu wanaishi.
Ufunuo wa Yohana 6:9 " Na alipoifungua muhuri ya tano , nikaona chini ya madhabau roho zao waliochinjwa kwaajili ya neno la Mungu , na kwaajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema , Ee Mola , Mtakatifu , Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu , Wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi ? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu , nyeupe , wakaambiwa wastarehe Bado muda mchache , hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na Ndugu zao , watakaouawa vile vile Kama wao."
Ukisoma hapo juu unapata picha gani juu ya wafu ? Kuna Wafu wapo hai wanastarehe.
Unakumbuka Yesu alitokewa na Nani pale mlimani wakati akiomba? Alitokewa na wafu, nabii Musa na nabii Elia wakazungumza nae. Kwa lugha ya kiswahili sanifu Tunasema alitokewa na mizimu( yaani watu waliowahi kuishi katika hii dunia na baadae wakafa au wakaondoka ktk hii dunia) . Mzimu wa Musa na mzimu wa Elia . Wafu hawafi , wafu wanaishi. Inayokufa ni miili..
Yule Mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ( mchawi/ mganga) anamwambia mfalme Sauli je! Ni Nani nitakayekupandishia? Naye akasema , Nipandishie Samweli ( nabii ambaye amekwishakufa na kuzikwa) . Yule mwanamke akampandisha Samwel kutoka ktk nchi ( ardhi/ kuzimu) . Nao nabii Samwel ( mzimu) na mfalme Sauli wakazungumza ..
Japo wanatheolojia wengine huwa wanasema kuwa Samwel aliyepandishwa toka kuzimu siyo Samwel . Ni pepo , jini au shetani lililojivika mwili wa Samweli. Lakini ukilisoma andiko hili ktk Biblia Hakuna mahali wala mstari wowote pameandikwa kukanusha kuwa yule alikuwa ni Samwel wa uongo, pepo , jini au shetani aliyezuka. Hili la Samwel wa uongo au wa ukweli siyo somo langu kwa leo . Leo nataka tu kukwambia kuwa * wafu wanaishi* .. Wanaishi katika dunia yao . Wanaishi katika ulimwengu wa roho. Wapo walio kuzimu na wapo waliokwisha tangulia peponi. Wanaishi maisha yao .
Kama wewe Bado mwili wako una uhai na uzima Basi usiingilie maisha ya wafu.
Lakini ktk Injili Yesu anakuja kutuonesha kitu cha tofauti kbs . Siyo tu kwamba Wafu wapo kuzimu na peponi tu , bali kuna wafu wapo duniani. Tupo nao tunaishi nao .
Yesu anamwambia mtu aliyemuomba akamzike baba yake, "waache wafu wawazike wafu wenzao" .
Huyu mtu anamuomba Yesu aende akauzike mwili wa baba yake , lkn Yesu anamwambia waache wafu wawazike wafu wenzao.
Hapa tunaona ya kuwa Kumbe Kuna Wafu wapo duniani ,wanatembea, wanaongea , wanakula , na pengine wanaongoza watu. Maana wafu waliokufa mwili wasingeweza kwenda kuuzika mwili wa mfu mwenzao .
Hii tafsiri yake ni kwamba , mwili huu wa mfu aliyetakiwa kwenda kuzikwa ulienda kuzikwa na watu wafu ambao hawajakufa mwili. Wamekufa rohoni na akilini. Nielewe vizuri hapa , hawajakufa roho Wala hawajakufa akili ,Bali wamekufa rohoni na akilini.
Miili yao ipo hai. Roho zao zipo hai . Akili zao zipo hai . Lkn Matendo yao ya mwili yanayoongozwa na roho na akili siyo Matendo yanayostahili kuwa ya mtu aliye hai rohoni ..
Wanahesabika kuwa wamekufa ktk ulimwengu wa roho..
Ikiwa mazishi ni ibada . Basi usiingilie ibada za wafu waache wafu wawazike wafu wenzao.
Kuna watu tupo nao tunaishi nso lkn waliishakufa tyr . Ni wafu . Matendo yao machafu , ya kinyama hayastahili kuwa ya Binadamu aliye hai.
Mtu akiishakufa amekufa . Ameondoka ktk ulimwengu huu .
Japo ni utamaduni, lkn Hata tukijitahidi kuuosha, kuusafisha, kuutakasa na kuuvalisha vizuri mwili wake, Haiondoi ukweli ya kuwa anakwenda kufukiwa na udongo chini ya ardhi.
Kwanini unahangaika kuwasafisha wafu ( sijasema maiti) . Unatumia gharama kubwa , muda wako na nguvu zako bure kuwasafisha wafu na unajua ya kuwa huwezi kubadilisha ukweli kuwa wanaenda kufukiwa na udongo chini ya ardhi!!??
Usiingilie ibada za wafu waache wafu wawazike wafu wenzao.
Wafu wanaelewana vizuri . Wanapata na muda Wanapiga story zao km Lazaro na tajiri. Wewe unaingilia story zao ambazo hazikuhusu. Unataka kumsafisha tajiri mfu . Mfu ni mfu tu . Haibadilishi ukweli hata Kama akitokea km mzimu wa Musa na Elia. Aliishakufa. Hayupo ktk dunia hii.
Ukihangaika kumsafisha mfu iwe ni bure au kwa gharama nawe unageuka kuwa mfu unayetembea . Wote mnakuwa wafu. Mmekufa kiroho na kiakili..
Je! Unaishi na mfu? Unafanya kazi na mfu? Unasoma na mfu ? Unaongozwa na mfu ? Unaongoza wafu?
Kuwa makini . Wafu wanaotembea wamekufa kiroho na kiakili . Ni wabaya wachafu kuliko wafu waliokufa kimwili .
Mungu JEHOVA wasamehe wafu wanaotembea maana hawajui walitendalo . Lkn wasaidie Sana wahangaikao kuwasafisha wafu maana hawajui kuwa wanageuka kuwa wafu wa kiakili . .
Ikiwa mazishi ni ibada Basi usiingilie ibada za wafu. Waache wafu wawazike wafu wenzao.
Makungu m.s
0743781910
23 April 2023