Miiko ya wafu na kaburi

Waterbender

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
6,826
8,676
Habari za muda sisi waafrica tuna miiko ya mambo na vitu mbali mbali, 2010 mpaka sasa miiko imekuwa ikipuuziwa tu na wengine wakisema ni mambo ya kizamani ebu tuone, moja wapo ya miiko hiyo ni hii, lakin kutoka kwa source nilipo ipata iko zaidi ya mia tisa🤔lakin naweka michache tu na wengine wataongezea .

KARIBUNI TUJADILI WAFU😀😀😀

1. Kaburi lilisale wazi, likilala wazi, basi mwanafamilia mwingine katika familia ya marehemu atafariki ndani ya mwaka huo huo. Kaburi lizikwe siku liliyo chimbwa.

2. Vifaa vilivyo tumika kuchimba kaburi, vinatakiwa vibakie kaburini kwa siku nyingine saba. Kuvipeleka nyumbani vifaa hivyo siku hiyo hiyo au kabla ya siku saba, ni nuksi kubwa sana.

3. Kuondoka makaburini kabla kaburi lote halijafukiwa, kutasababisha msiba kwenye familia yako wewe uliye ondoka kabla watu hawajamaliza kuzika. Mvua ikinyesha kwenye kaburi ambalo bado halijafukiwa, ni ishara mbaya sana kwa familia ya wafiwa. Ili kuepukana na nuksi hiyo, inabidi kuwe na mtaalamu wa kuzuia mvua.

4. Ni nuksi kubwa sana kusonta kaburi
5. Ni nuksi kubwa sana kurukia kwenye kaburi
6. Ni nuksi kutembelea makaburini baada ya jua kuzama
7. Wafiwa wasiondoke nyumbani wala kujichanganya mtaani na watu wengine, hadi matanga yatakapo inuliwa. Kwa mfano watu wengine, unakuta mtu amefiwa, lakini kabla hata matanga hayajainuliwa, anakwenda bar kunywa na kurudi msibani. Hayo ni makosa makubwa sana.

8. Wafiwa wote wakuu, yaani ndugu wa karibu wa marehemu, wasioge hadi baada ya siku tatu, ambayo ndio siku ya kuanua matanga, na maji watakayo oga yawe maji ya moto.

9. Wafiwa wasishiriki ngono hadi matanga yatakapo inuliwa.

10. Waombolezaji msibani, wasiongee kwa nguvu wala kucheka kwa nguvu. Ni makosa makubwa sana kufanya hivyo.

11. Endapo mtu anae karibia kukata roho, atakun’gata, basi na wewe utamfuata baada ya muda mfupi. Ili kujiepusha na kifo cha namna hiyo, basi unatakiwa na wewe umng’ate katika sehemu ile ile aliyo kun’gata.
12. Kama kiongozi wa familia atafariki dunia, basi mnatakiwa kusimamisha saa kubwa ya ukutani inayo kaa sebuleni, vinginevyo wanafamilia walio baki nao watamfuata ndani ya kipindi kichache, vitatokea vifo mfululizo vya wanafamilia.
13. Baada ya kuuosha mwili wa marehemu, na kuuvisha nguo zake, unatakiwa kuweka punje moja ya chumvi kwenye kifua cha marehemu ili kuwafukuza roho na majini wabaya.
14. Kama marehemu atakuwa akiwa ameacha macho wazi , hiyo ni ishara mbaya sana. Maana yake ni kwamba,anatafuta watu ( ndugu zake ) wa kwenda nae kaburini. Kujiepusha na hilo, funikeni macho yake kwa kutumia sarafu .
15. Usifagie chumba cha marehemu kabla marehemu hajatolewa. Endapo utafanya hivyo, basi amini nakwambia wewe ndie utakae mfuata marehemu.
16. Msitoe shuka wala nguo yoyote iliyopo kwenye kitanda alicho kilalia marehemu, na ambacho umauti ulimkuta. Endapo mtakiuka hilo, basi mwanafamilia mwingine atafariki ndani ya mwaka huo huo.
17. Endapo Kundi la wanandugu, jamaa na marafiki, mtaenda kuuchukua mwili wa marehemu halafu ghafla mkaona anatoa damu kwenye tundu za pua, basi mjue kuwa marehemu amekufa kwa mkono wa mtu, na aliye husika na kumuua, yu miongoni mwenu,ndani ya chumba hicho hicho.
18. Kwa mara nyingine tena narudia, mwili wa marehemu unapotolewa kwenye jengo lolote lile, iwe nyumbani, kanisani, au msikitini ni lazima miguu ndio itangulie kutoka na sio kichwa, vinginevyo roho au mzimu wa marehemu huyo, utatazama katika jengo hilo na kumuita mtu mwingine wa kufuatana nae.
19. Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.
20. Ukiugusa mwili wa marehemu, utakuwa na uhakika kwamba, roho ya marehemu haitakusumbua. Na endapo utaugusa mwili wa marehemu usoni, hutoota ndoto mbaya kuhusu marehemu huyo.
21. Usipeleke mwili malaloni kwa kutumia gari lako binafsi. Ni nuksi kubwa sana kufanya hivyo. Mwili wa marehemu unapelekwa malaloni kwa kutumia gari maalumu.
22. Endapo mtasafirisha mwili wa marehemu kwa basi, kichwa kitazame anapotoka na miguu itazame anapoelekea.
23. Usi hesabu magari kwenye maziko (makaburini), ukifanya hivyo unakuwa unahesabu siku zako mwenyewe za kuishi.
24. Kuwa muangalifu usione taswira yako kwenye gari lililo beba mwili wa marehemu, vinginevyo wewe ndio utakae fuatia kubebwa kwenye gari hilo.
25. Usiende na mtoto mchanga kwenye msiba, vinginevyo atakufa kabla hajatimiza mwaka mmoja.
26. Ni nuksi kubwa sana kutangulia makaburini ( kwenye maziko) au kupita bila kushiriki kwenye maziko . Kama utafanya hivyo, utakufa ndani ya muda si mrefu.
27. Kama paka mweusi atakatisha mbele wakati wa maziko (makaburini ) mwanafamilia mmoja katika familia ya marehemu atakufa ndani ya siku tatu.
huyo mwingine atapata nafuu kubwa.
28. Kuna ndege mmoja anapatikana porini ( SIMTAJI KWA SABABU ZA KIMIIKO), ukichukua nyoya la huyo ndege halafu ukaliweka kwenye mto wa kitanda anacho lalia mgonjwa, basi mgonjwa huyo atakufa wala hatopona. Nyoya hilo hilo likiwekwa kwenye kitanda anacholalia mtoto mdogo, litamzuia mtoto huyo kukua.
29. Kitanda anacho lalia mgonjwa mahututi, kitazame mashariki na magharibi, na kamwe sio kaskazini na kusini. Kichwa kiangalie magharibi na miguu itazame mashariki.
30. Jina la mwisho kutajwa na marehemu wakati anakaribia kukata roho, litakuwa jina la mtu atakae fuatia kufa baada ya marehemu.
graves-660x400.jpg
cemetery-989920__340-660x330.jpg
 
Wafiwa wote wakuu, yaani ndugu wa karibu wa marehemu, wasioge hadi baada ya siku tatu, ambayo ndio siku ya kuanua matanga, na maji watakayo oga yawe maji ya moto.

.Wafiwa wasishiriki ngono hadi matanga yatakapo inuliwa.

. Waombolezaji msibani, wasiongee kwa nguvu wala kucheka kwa nguvu. Ni makosa makubwa sana kufanya hivyo.
 
Wafiwa wote wakuu, yaani ndugu wa karibu wa marehemu, wasioge hadi baada ya siku tatu, ambayo ndio siku ya kuanua matanga, na maji watakayo oga yawe maji ya moto.

.Wafiwa wasishiriki ngono hadi matanga yatakapo inuliwa.

. Waombolezaji msibani, wasiongee kwa nguvu wala kucheka kwa nguvu. Ni makosa makubwa sana kufanya hivyo.
Nahisi hii ya kuongea sana msibani haiwahusu wachaga. Kwanza vikao vyao vya misiba ni kama vya harusi wakimaliza kuzima kama hakuna kilichotokea
 
Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.

Hilo limeshawatokea wengi mno hasa watani zangu
hili hata mm nimelishuudia mtoto wa kiume wa kwanza alifarik kipind wana peleka maiti musoma na marehum alitaka azikwe kwake dodoma, msafara ulizindikizwa na gari za jezi lakin ukala mzinga nzega
 
Back
Top Bottom