Uhai, kifo, mwili na roho

Jan 9, 2024
3
5
Uhai ninini?🤔

Uhai ni muunganiko wa mwili na roho

Hivi viwili kimoja kikiwa kinaonekana na kingine kikiwa hakionekani, ungano lao kwa usahihi wake ndio huleta kitu kinaitwa UHAI

2. Kifo ni nini? 🤔

Kifo ni hali ya kukoma kwa uhai

Kivipi? 😳

Roho inapojitenga na kile kiunganishi
kingine kinachoitwa mwili ndio kifo
hutokea

Kifo na mauti ni kitu kimoja na ni
kile kile

3. Mwili ni nini? 🤔

Mwili ni kibebeo, ni jumba ni kasha tu yaani 😁

Na ndio roho huja na kukaa ili kukamilisha tendo la uhai

Na hivi viwili vikiwa pamoja
ndio hutengeneza kitu kinaitwa nafsi au utambulisho

4. Roho ni nini? 🤔

Roho ni nishati Roho haionekani, haina
umbo, haina sura, haina harufu

Hivyo vyote ni vya mwili Lakini ili viweze kufanya kazi vinahitaji roho

Roho pamoja na kuwa ni nishati lakini katika ndani ya mwili ni nishati yenye pumzi

Hapa lazima tuelewane kuna nishati
hazina pumzi

Sasa tusonge mbele Je kinachokufa ni
mwili, ni (nafsi) au ni roho? 🤔

Kwa tafsiri iliyozoeleka ya kibinadamu kinachokufa ni mwili

Kwanini mwili? 🤔

Kwakuwa ndio kinachoonekana ndio visible Ndio kilichoundwa ama kuumbwa

Kila kilichoumbwa huwa na kikomo ama ukomo wa kukua

Roho ni pumzi na ni nishati tu

Nishati wala pumzi havifi vilikuwepo vipo na vitakuwepo milele

Lakini kwa usahihi kinachokufa ni NAFSI yaani utambulisho wako wewe

Na ndio maana tunaambiwa kila nafsi itaonja MAUTI

Haisemwi mwili wala roho bali nafsi kwahiyo hata tunapofanya ibada na chochote kinachohusika na wafu tunadili na nafsi na sio mwili wala roho

Najua fika utasema mbona kuna roho mfu? 😳

Kiuhalisia hakuna roho mfu

Ufu wa roho ni ile hali ya mwili kutengana na roho na hapo ndio tunapata tafsiri mbili moja
ikiwa sahihi na nyingine ikiwa sio sahihi

Sahihi ni mwili mfu kwa kuwa baada ya kutengana na roho wenyewe huendelea kuharibika kuoza na hatimaye kupotea milele

Kinachobaki ni nafsi utambulisho ambao haupo tena bali historia yake tu

Roho hubaki ikisubiri kiama ama kuingia kwenye utaratibu mwingine ama kugeuka mzimu
 
Back
Top Bottom