Tunaweza kufikia teknolojia ya kufufua wafu?

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Wakati waumini wote wa dini ya kikristo duniani wakiwa wanaazimisha sikukuu ya kufufuka Kwa bwana yesu kristo, ningependa tuiangazie tekinolojia ya ufufuko na namna ambavyo wanadamu wanajaribu kupiga hatua kuhakikisha inakuwa mikononi mwetu.

Mwaka 2011 mwanamuziki Eminem na mtayarushaji wa muziki na mwanamuziki Dr. Dre walitoa kibao kilichokwenda Kwa jina la "I need a doctor" Huku katika kiitikio wakimshirikisha mwanadada Skylar grey

Katika kiitikio mwanadada Skylar grey Kuna mistari anasema:-
"I need a doctor, call me a doctor
I need a doctor to bring me back to life"

Akimaanisha kuwa
"Nahitaji daktari, niitieni dakatari
Nahitaji daktari anirudishe tena kuwa hai/anifufue"

Sasa swali linauliza je, tutaweza kuifikia tekinolojia ya kuweza kuwafufua wafu? Hiyo ndo story yetu ya Leo.
________________________________________________

Katika wimbo huo, Dr. Dre anaonekana kuendesha gari Kwa spidi Kali sana Huku akiwa na msongo mkubwa wa mawazo Huku akiwawaza marafiki zake kina Eminem, 2pac, Eric wright, Snoop doggy, ice cube nk, msongo huo wa mawazo ukampelekea akapoteza control ya gari na kupata ajali iliyopelekea akafa

Dr. Dre akapelekwa hospitali na hatua ya kwanza ilikuwa ni kumnyoosha mifupa kupitia "equilibrium technology" akafungwa kamba kamba akiwa amelala ananing'nia.

Baada ya hapo, Dre akapelekwa na kuwekwa kwenye chupa maalumu iliyokuwa na kimiminika maalumu, akawekwa humo Kwa muda Fulani, baadae vinaonekana vidole vya mikono vikicheza cheza(hiyo ilikuwa ni alama kuwa Dre anaelekea kuaamka kutoka katika usingizi wa kifo) na baadae anatolewa kwenye chupa akiwa chini ya uangalizi wa madaktari kitandani, Dre anafumbua macho na kuwa hai Kisha anavikwa "exoskeletons" za chuma na kufundishwa upya kujongea kupitia mifumo ya computer mpaka ana adapt na kuweza kutembea mwenyewe na kufanya mazoezi ili kuuweka mwili sawa.

Katika huo wimbo, ujumbe mahususi ni kuonesha tekinolojia ya kuweza kuwafufua wafu

Katika bailojia tunaambiwa kuwa "cell" ndo kiini Cha msingi Cha uhai" viumbe hai wote wameundwa Kwa cell(s) aidha cell Moja (mfano bacteria ) au cell zaidi ya Moja mfano binadam

Sasa ili kiumbe kiwe hai maana yake cell yake/cells zake lazima ziwe zinafanya kazi, hari kadhalika ili kiumbe kihesabike kuwa kimekufa maana yake cell yake /cells zake ziwe hazifanyi kazi.

Kumbe kiumbe chochote mfu, maana yake cells zake zote zimekufa/zimesimama kufanya kazi

Sasa ili kiumbe kiweze kufufuliwa lazima hizi cells zilizokufa /kusimama kufanya kazi lazima zote ziamshwe. Ili tuende sawa nitatumia mfano wa mwanadam mathalani Dr. Dre, maana yake mpaka Dre akafufuka kutoka usingizi wa mauti ni kwamba cells zake zote ziliamshwa na kuanza kufanya kazi upya.

Ila tunafahamu mwanadamu akishakufa anaanza kuoza, wanaomuozesha ni viumbe wadogo wadogo mathalani bacteria, hivyo basi kabla hatujafikia hatua ya kumfufua mtu, lazima tuzuie kwanza asiweze kuoza, katika video, Dr. Dre aliwekwa kwenye mtungi wenye kimiminika maalumu, kimiminika kile kinaitwa "liquid nitrogen" na kunakuwa na mazingira yenye baridi Kali sana ndani yake kukaribia takribani nyuzi za centigrade -196°C(ila nyuzi hizo hazifikiwi sababu katika nyuzi hizo liquid nitrogen hubadilika na kuwa katika hari ya yabisi) katika mazingira hayo hakuna bacteria yeyote anaweza kustahimiri hivyo mwili unabaki salama bila kuoza Kwa muda mrefu sana, uhifadhi huo wa miili katika mazingira ya baridi Kali kama hiyo kitaalam huitwa "cryonics" na inatumika liquid nitrogen sababu freezing point yake iko chini sana, pia hutumika hata katika mafriji, nitrogen katika mazingira ya kawaida huwa katika hari ya gesi, ila ikipoozwa sana hubadilika na kuwa kimiminika(infact gas zote zikipoozwa hubadilika na kuwa kimiminika na kama ukipooza zaidi hubadilika na kuwa katika hari ya yabisi).

Ila katika mazingira hayo ya baridi Kali (licha ya kwamba tunazuia mwili kuoza) ila baridi hili Kali hupelekea viungo vya mwili kama organs mbali mbali kupata uharibifu Kwa kuunda nyufa hivyo ufanisi wa ufanyaji kazi unakuwa umeharibika hivyo basi hapo itahitajika tekinolojia ya kuweza kuhifadhi mwili bila ya hitilafu yoyote kutokea. Hiyo ni changamoto kubwa sana.

Lakini pia mwili unapokuwa humo ndani ya chupa hiyo Kwa muda mrefu basi hutokea kitu kinachoitwa "vitrification" Yani kimiminika kinaweza kupenya sehemu za ndani za mwili na kuleta uharibifu hasa kwenye ubongo na kuua "neural circuits" za ubongo hivyo basi changamoto nyingine ni kupambana kuipata tekinolojia ya kuzuia vitrification.

Ila katika miaka ya 1990 wataalam wa cryonics (cryobiologists ) bwana Gregory Fahy na Brian wowk walifanikiwa kuhifadhi ubongo wa panya Kwa kutumia tekinolojia hiyo hiyo ya cryonics na ubongo haukupata hitilafu yoyote walichokifanya ni kuzuia namna ambavyo cells za ubongo zingeweza kupoteza maji (dehydration) Kwa kuratibu mchanganyiko wa liquid nitrogen uwe katika uwiano stahiki, na kuratibu jotoridi Kwa takribani nyuzi -135°C hiyo ilikuwa ni hatua kubwa.

Ila changamoto Bado ipo katika upande wa kufufua kiumbe Sasa kirudi kuwa hai tena, hapa ndipo penye ugumu na wanayansi wapo wanaumiza kichwa namna gani wata reverse mchakato wa kifo na kurudi kuwa uhai, ila pia itahitajika tissues kadha wa kadha kuzalishwa upya sababu ya life span zao nk

Katika kulitatua hilo, wanasayansi wanaifikiria tekinolojia ya "Nanotechnology" kuwa huenda ikawa ndo mwarobaini wa kuwezesha hilo(kuwafufua viumbe hai) ila tekinolojia hii ya Nanotechnology ndo ipi? Hiyo ni story itakayofatia.

Ila mpaka kufikia mwaka 2014 tayari nchini marekani miili takribani 250 ya wafu ilikuwa imehifadhiwa katika hizo chupa maalumu ikisubiri igunduliwe tekinolojia ya kuwafufua wafu ili ifufuliwe.

Mpaka kufikia mwaka 2016, kulikuwa na maabara nne tu za kuhifadhia miili ya wafu ikisubiri ugunduzi wa hiyo tekinolojia, maabara tatu zikiwa nchini marekani, na maabara Moja ikiwa nchini urusi. Huku watu takribani 1500 (Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016) wakiwa wamejiandikisha na kufanya malipo ya kuhifadhi miili Yao pindi watakapokufa.

Nini maoni yako? Je tutaweza kuipata tekinolojia ya kuweza kuwafufua wafu?
FB_IMG_1681120908458.jpg
 
Moja ya Tecnolojia ambazo haziwezekani kuwepo , hata matajiri mbali mbali ambao hufinance ugunduzi wa technology mbali mbali washaachana na hyo hasara
 
Nimeikumbuka ile movie ya Dr Einstein...yeye alifufua mtu wake ila huyo huyo mtu ndiyo akamuua dr na mkewe
 
Je, ungepata ofa ya kuhifadhi mwili wako pindi utakapokufa ungekubali?

FB_IMG_1681120908458.jpg
 
Haitowahi kuja kutokea hata siku moja hii coment yangu iwekwe hapa vizazi na vizazi ije ione kuwa haitowahi kutokea hio kitu ukifa ndo umekwenda mkuu
 
Kufufua maana kifo kinaweza kusababishwa na ajali kama ya sunami n.k
Kwani hamtaki kujua yaliyoko huko?
Au hamna kingine ni haya tunayoyaona kwa macho na darubini tu?
Unamrudisha mtu anajiua tena maana bora huko alikokuwa!!
 
Upo wakati itawezekana na japo itakuwa Ni kwa aina fulani ya vifo kama ajari ,mishituko na vifo mbalimbali vifananavyo na hivyo!

Ugumu utabaki kwenye uzee na magonjwa.

Nawambia kwa sababu nafahamu.
 
Ni Bwana Yesu au Yesu Kristo na siyo bwana yesu kristo
Teknolojia ya kufufua wafu is as old as 2000 years ago na muasisi wake ni Bwana Yesu.
 
Back
Top Bottom