IGP, Kama unataka kuwakamata wauaji Pwani...

IGP, Kama unataka kuwakamata wauaji Pwani...

kwa kifupi na kwa kusummirize kibiti panahitaji intelijensia ya kujiingiza katikati ya jamii (Collaborationa trick) ndipo ujue chanzo nini na ni watu gani, ndipo upande tactics za kuwakamata...mkitumia tu nguvu wale watu watawashinda.
Collaboration sio kwa kule maana wanakijiji huwa wanajuana wote hata akija mtu mpya wanamjua na inavyoonekana ni kama wanawalinda waharifu hivyo ni ngumu kujichanganya zaid unaweza jikuta unakuwa target bure, kule Jeshi liingie msituni usiku lipige kambi
 
Ni kweli na hao wala hawahitaji mbwembwe za polisi weeeengi kwenye eneo......wala statement za vitisho eti tutawaua wote au jeshi la polisi litawakamata wote......unapokuwa unaongea na watu ukute na hao viongozi wao wapo palepale.......so katika ulimwengu huu wa kigaidi ni lazima kuwa makini sana na uhalifu na izingatiwe kwamba mahala popote duniani kwa sasa panapokuwa na rais mkristo haya mambo huwa yanatokea......hivi unafhani boko haram walishindwa Nigeria?... Alipoingia buhari tu wametulia.....vita kama hiyo ni ngumu sana maana ni ya mtandao usikute hata ndani ya jeshi la polisi wanamtandao wamo wapo.......ushauri wangu ni kwamba igp siro atulie.........ajitathimini jeshi lake......halafu ateue watu wachache sana watakaokuwa wanaoperate extraordinary..... Bila kulipot kwa mtu yeyote isipokuwa yeye tu......na wasiongeeongee sana na pia wachunguzwe sana wao wenyewe......wakifanya hivyo naamini watafanikiwa ila staili hii ya matangazo na mabunduki mengi haitasaidia lile eneo......Mungu ibariki Tanzania
Mkuu sijuwi wakati mwingine kama hujuwi kitu bora ukanyamaza mambo ya boko haramu ni mambo makubwa sana sana wale wamewekwa pale na mataifa makubwa kwa malengo yao sawa na ilivyo Alishababu apo somalia !!
Tutapata shidah sana Africa kwasababu huwa hatujuwi nini huwa kinatuangamiza asilimia 80 tumelogwa na nchi za magharibi na mafanikio ya uchawi wao ni jinsi ubongo wako unapo fikiri kwa kwenda chini badala yakwenda juu!!!
 
Mkuu fafanua, unasema haya mambo hutokea panapokuwa na RAIS MKRISTO. Hivi kumbe rais mkristo hapendwi na wasio wakristo? Somalia hata sambusa marufuku kupika ila alshabab wapo. Kumbe suluhisho ni kuchagua rais wa dini gani???
Mkuu utapata taabu bure hawa watu wa aina hiyo wamelogwa na wtu wa magharibi utapata shida kweli huyo pengine ata bendera ya Israel atakuwa anaweka juu ya mto wake wa kitanda akiamini shetani haisogelei!!!
 
Na hao wahalifu wameshakuwa wenyeji sana pande hizo. Kwa hiyo akiingia mgeni yeyote atafuatiliwa kwa makini sana.
Kuna mbinu nyingi sana za kupandikiza intelligensia pasipo kujulikana na MTU au kitu chochote
 
Umetoa mfano mwenyewe wa kuhusisha imani na mauaji kama ilivyokuwa huko Geita ulikotaja.

Kwa muda mrefu mauaji ya imani za kishirikina yamesumbua sana serikali na bado yanaendelea kuisumbua .Kwa hiyo kukaa na kuamini kuwa mauaji yanayoendelea sio ya imani kama za kishirikina ni kujidanganya.

Huenda hao watu wenye imani za kishirikina wameamua kutafuta viungo vya wenyeviti wa serikali za mitaa baada ya kudhibitiwa na serikali kwenye mauaji ya kuchuna ngozi,kuua albino n.k
Kwa hiyo pia inawezekana wale washirikina waliokua wanaua albino huenda ndio hao hao wamehamia Kibiti na Rufiji kwa imani zile zile za kutoa damu za watu.
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Nakubaliana na uchambuzi wako na nafurahi kwamba kuna watu wanaweza kuuchambua uhalifu na kutengeneza profile ya mhalifu kwa kiasi cha kuridhisha kiasi hiki. Inanikumbusha series ya 'Criminal Minds'.

Nami niongezee machache:
  • Polisi wajaribu kuchambua namba za simu zinazotumika kati ya Dar na Kibiti,Ikwiriri na Rufiji. Let's hope watakuwa na software ya kuwawezesha kuchambua taarifa hizo. Kama hawana ni vizuri wakatafuta nguli wa IT kwa ajili ya kuanalyze taarifa za mitandao ya simu kwa watu wanaosafiri mara kwa mara kati ya Dar na miji hiyo.
  • Sishauri JWTZ wahusishwe ktk hatua ya sasa. Polisi wana nafasi nzuri zaidi ya kusitisha mauaji haya kuliko JWTZ. Tatizo lililopo ni intelijensia. Serikali haijaweza kubaini kwa kina wahalifu ni kina nani, wana ajenda gani, na anagharamia uhalifu wao, wako wapi na nani anawaunga mkono. Ni jeshi la polisi na usalama wa taifa wanaoweza kupata taarifa za uhakika kuhusiana na jambo hilo kwa sababu ya mafunzo yao, uzoefu na ukaribu na jamii.
  • Serikali imefanya vyema kutolihusisha jambo hili na dini. Dini ndio udhaifu wetu kama taifa. Haijalishi kama ni kweli dini inatumika au la.
  • Watu wa Kibiti, Ikwiriri na Rufiji watumie hata mtandao kama hapa JF kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili tuweze kumaliza tatizo hili.
Kudos Technology
umeandika ya maana. kumbe watu mpo...
 
Upelelezibwa kujiingiza katika jamii ndio njia sahihi.
La kuzingati.
Wapelelezi wawe raia wa hukohuko na wasifahamike kuwa wanafanya kazi hiyo.
Mgambo wanaweza kutumika pia
Au mbinu ya kutumia wafanyakazi wa kuajiriwa, hapa watu wanaweza kuajiriwa kwenye idara za huko na wakaonekana kama wafanyakazi wakawaida kama walimu wa Primary na Sekondari ni wazuri zaidi kutumika.
Wawe wanao fiti katika maswala yote ya kijamii kama katika imani, michezo, tamaduni nk.
Wazee wa maeneo husika washirikishwe wanajua tabia za watu wengi wa eneo husika vizuri.
Wafanyakazi wanawake kama wale wanaouza Baa za vilevi huwa wanajua habari nyingi za kihalifu za maeneo yao, ni vizuri nao wakashirikishwa.

Mnaojua uhalifu wa huko hasa ninyi raia wema wa huko, ndio haswaa tunaowategemea kuweza kulitatua hili tatizo.
Isaidieni basi nchi yenu kwa kutoa taarifa za hao wahalifu kwani mnaishi nao na wengine mnawajua.
Wanakibiti onyesheni uzalendo jambo hili likomeshwe.
Mnakubalije kufa huku mmemkumbatia adui ?
Anzeni kazi sasa
Saa ya Ukombozi ni Sasa.
Hahahaha unataja mbinu tena mkuu?kama wapo humu si wanakuwa wameshajua?
 
Mkuu wewe nadhani una information nyingi sana kuhusu hili swala, kwann usiende polisi ukatoa hizi taarifa
 
Ni kweli kuna kila dalili ya suala la kiimani nyuma ya hawa wauaji.

Serikali isipojipanga mapema hawa watu wataleta madhara makubwa sana na sioni dalili ya hawa watu kusarenda bila mikakati mikubwa sana.
Wanaonekana kwa kweli wamejaa huko Ikwiriri na nchi nzima kuanzia vijijini mpaka mijini. Kwa sasa kuna makundi yanayojifanya yanaimani sana za kidini na hayajali uhai wa wale wasiowaunga mkono.

Serikali itumie mfumo wa ulinzi wa Rwanda au Israel.
Ambapo jeshi linatumika sana kupata information na pia linashirikiana na polisi kulinda usalama wa nchi.

Tanzania tuna majeshi mengi sana lakini cha ajabu watu wa chache wanapora silaha na wanajificha porini na silaha zinatumika kuangamiza maisha ya watu.

Tujiulize kwa nini migambo hawaajiriwi na vijiji kama walinzi kama enzi za awamu ya kwanza ya Mwalimu.

Rwanda polisi na Jeshi wanashirikiana kwenye ulinzi kwa kupeana muda.
Mchana polisi wanafanya kazi na usiku Jeshi linaingia mtaani. Nchi inakua shwari kabisa.

Nchi zote ambazo zina watu wenye imani za kuua ua watu kwa ajili ya kujenga hofu zinazibitiwa kwa mfumo wa ulinzi unaofanana na ule wa Rwanda, Israel,Libya enzi za Gadaff na Iraq enzi za Sadam Husein.
Ni mfumo wa jeshi kuzibiti maeneo wakati wa usiku na kutumia zana kubwa na za kisasa kuwatafuta wahalifu.

Pia mara nyingine mauaji kama hayo wanasiasa hua hawakai siriasi kuyatokomeza kwani ni moja ya matukio ya kuhamisha watu kwenye mijadala mipana ya kuzungumzia umaskini wao na haki zao. Wanabaki wakijawa na hofu kubwa.

Lakini ninaamini kuwa bado hatujaamua kukaa na kufikiri vya kutosha namna ya kuwatokomeza hao majangili wenye viashiria vya kigaidi.

Siamini kuwa hatuna ndege za kijeshi zenye uwezo wa kutafiti na kujua kambi zao zilipo. Hao watu kwa vyovyote wanafanya mafunzo ya kijeshi.

Kwa kweli inabidi amiri jeshi mkuu abadili mfumo wa ulinzi ili doria zifanywe na majeshi yote kwa kubadilishana muda wa kazi kwa sababu polisi wakati mwingine uchache wao unawafanya wawe wanazidiwa maarifa kutokana na kufanya kazi wakiwa wamechoka. Mchana kutwa wanakimbizana na vibaka, wafungwa mahakamani na doria mabarabarani ,mara kukamata mabodaboda n.k. then wanafanya doria tena usiku. Ni wazi kuwa watakuwa wamechoka kiakili na kimwili.
Lakini kama wangekua wanasaidiana wanajeshi na kigambo wakati wa usiku ulinzi ungekua ni jukumu la wanajeshi. Polisi wangekuwa wanavua uniform na kuingia mtaani jioni kusaka taarifa za uhalifu.

Ni muda mrefu tangu hawa wauji wameanza lakini bado hawajakata tamaa mana inaonekana mizizi yake haijawahi kuguswa.

Na hili la kutangaza zawadi nalo pia sio ishu mana kuna watu wataanza kuropoka kuwa wameanza kazi ya kuwasaka hao majangili kwa lengo la kupata fedha hizo matokeo yake wataambulia kuuawa.
Cha msingi ni kuweka intelijensia ya uhakika hata ya kununua na kuwalipa kimya kimya kwa mikataba maalum kama wanavyofanya CIA na FBI.
Kwani wanaouwawa ni dini gani?? Nadhani hapo hakuna swala la dini hii ni siasa tu,wameuwawa wenye viti na sasa ni migambo ukichunguza huenda hawa migambo walikuwa wanafanya kazi na hiyo serikali ya kijiji kwa hiyo uchunguzi ufanyike hapo

Lakini viongozi wakubwa wanadharau hii bila kujua lengo halisi ni nini wameanzia na hawa wa chini labda ni kupima tu upepo

Baadae huenda ukasikia mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa, kamanda fulani kauwawa ndio akili zitakaa sawa na wakati huo huenda washachelewa sababu maadui watakuwa wamejiimarisha na kusoma vizur aina ya ulinz wa jeshi letu
 
A Simplified Guide To
Firearms Examination
How It’s Done
Firearms Evidence that May be Found
The range of evidence in firearms-related cases can be as small as a piece of a bullet fragment which has rifling marks or as large as hundreds of bullets and cartridge cases and numerous firearms. Even from small samples, information can be developed to indicate the type of firearm used and possibly identify the actual firearm that was used.
Other firearms evidence that could be found at a shooting scene includes shotshell wads and shot pellets; these can indicate the gauge of the shotgun. Wads and pellets can be gathered and preserved in the same manner as bullets and cartridge cases.
By examining wadding materials, the examiner may be able to determine
the gauge of the shotgun
the manufacturer or marketer
a range of possible shot sizes based on impressions in the shotshell wad
individual characteristics (in some cases)
Gunshot residues fall into two categories. The first type is gathered from the suspected shooter’s hands with a collection kit. The purpose of the examination is to determine if a person has recently handled or fired a weapon. Since it doesn’t determine which firearm was fired or when, this testing has limited value, and many laboratories have stopped performing these examinations. The second type looks for residues on items such as a victim’s clothing in an effort to determine the muzzle-to-target distance. Many times this type of evidence is not visible to the naked eye and requires microscopic examination and chemical testing to develop. The victim’s clothing must be handled with care, air dried and stored in paper containers in order to provide useful evidence.
Propellants and other gunshot residues expelled during the firing process. (Courtesy of Jack Dillon)
How the Samples are Collected
Firearms evidence can be recovered in a number of ways and areas. Firearms themselves can be recovered at shooting scenes by crime scene investigators and sent to the laboratory. Bullets, bullet fragments, cartridge cases, shotshell wadding, etc., are normally collected individually after proper documentation/photography and sent to the laboratory. Bullet evidence can also be obtained at autopsy or in an emergency room setting. In these cases the sample should be marked as a biohazard and then sent to the laboratory. Each laboratory has written procedures for packaging and submitting evidence.
Bullets/slugs that do not strike a person are often imbedded into a nearby surface such as wood/drywall. This evidence is best gathered by cutting out a section of the material and submitting it to the laboratory to allow a firearms examiner to carefully extract it. This prevents adding or destroying any markings that could be crucial to identifying or matching the suspected firearm.
Who Conducts the Analysis
A well-trained firearms examiner should perform the evaluation and comparison of this evidence. These examiners will have received extensive training on all matter of firearms and ammunition manufacturing; evidence detection, recovery, handling and examination procedures; comparison microscope equipment and procedures; courtroom testimony and legal issues; and casework.
 
Inshu ya kibiti ni ngumu sana maana hata kama wewe ni mpepelezi ukiingia kule lazima utajulikana na mwisho wa siku utauawa sio rahisi kama mnavyodhani shida inaanzia kwenye jamii kwa maoni yangu jamii ya pale inasapoti hivi vitendo ndo maana inakuwa ngumu mno kwa intelejensia kuingia na kufanya kazi
 
Serikali iliwahi kutangaza kuwa wahusika wa mauaji huko wamekamatwa. Sasa sijui wanatoka wapi tena!!????
Hivi vikundi inabidi vidhibitiwe mapema kabla ya kuota mizizi, lasivyo kutazuka Boko Haramu na Al-shabab wa Tz.
IGP kazi kwako kamanda wetu.
Intelijensia inahitajika kujiingiza katikati ya Jamii na kujiingiza katikati ya Jeshi letu husika.
 
Typical of alshaabab and boko haram...

Where were they trained!?
Kunasadikika kuwa kuna kundi la vijana wengi wa kitanzania wanaopatiwa mafunzo ya kigaidi na makundi ya alshabab somalia.
Hata wakenya walishatushtua kuhusu hilo.
Yawezekana wengi wao wameshamaliza mafunzo na kurejea kimya kimya na sasa wanasubiri kipyenga tu.
 
Inshu ya kibiti ni ngumu sana maana hata kama wewe ni mpepelezi ukiingia kule lazima utajulikana na mwisho wa siku utauawa sio rahisi kama mnavyodhani shida inaanzia kwenye jamii kwa maoni yangu jamii ya pale inasapoti hivi vitendo ndo maana inakuwa ngumu mno kwa intelejensia kuingia na kufanya kazi
sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom