Kile kinachoendelea huko Pwani hususani Kibiti,ni mambo ya hovyo sana, ni aibu, ni ukosefu wa utu, ni ukosefu wa ueledi kwa serikali haswa jeshi la polisi
Wana wakamata viongozi wa CUF, wanawatesa, wanapigwa risasi, wanaweka vizuizini, eti wana watafuta wauaji wa raia hususani viongozi wa ccm wanaouawa kila mara.
Haya ni mambo ya ovyo, yanachochea mpasuko ktk jamii, hakuna tena kutumia akili, kilichobaki ni ubabe, nguvu na utendaji wa kujilisha tuu.
Waziri wa mambo ya ndani ameshindwa kazi atuachie nchi ikiwa salama, huu ni wakati muafaka kwake kujiuzulu.