IGHONDO NI SINGIDA KASKAZINI, SINGIDA KASKAZINI NI FURAHA.

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
216
229
Anaandika Mo Mlimwengu.

Penye nia pana njia na subira huvuta heri. Hii subira ndio imepelekea wakapata mbunge ambaye hata akiwa Dodoma moyo wake uko singida ila mwili wake uko Dodoma. Mh Ramadhan Ighondo ni mtu ambaye vitendo vyake vinazidi maneno. What a Mp?

Jiimbo la Singida Kaskazini limempata mwenyewe na si walisema mzigo mzito apewe mnyamwezi sasa la Singida kaskazini kapewa Ighondo. Wote tunajua kilimo ni uti wa mgongo lakini asilimia 70 ya watanzania wote tunategemea kilimo. Haya matukio huwa ni nadra sana kutokea ila leo historia imefanyika na imetokea.

Tunashuhudia mtu wa maana kabisa Mh Ighondo Ramadhan akiwa makini kuangalia mkataba mkubwa wa mradi wa umwagiliaji skimu ya Msange mbele ya Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo Mh Hussein Bashe ukisainiwa.

Kwa jimbo la Singida Kaskazini hii ni heshima kwao na upendeleo wa hali ya juu. Sijui watoe shukrani ya aina gani kwa Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan. Huu ni upendo wa hali ya juu kwa wana Singida. Na kwao wanyaturu desturi yao upendo hulipwa kwa upendo.

Siku ya leo nyaraka wamebadilishana kati ya Mkandarasi Kagwa Eng Co na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji ndugu Raymond Mndolwa. Kilimo ni maisha na maisha yetu ni kilimo. Wema hulipwa kwa wema.

Mh Ighondo Ramadhan umeandika historia kwa kuhakikisha serikali ya Dr Samia inafuta machozi ya kilio chako ambacho umekuwa ukipigania siku zote ukiwa bungeni.

#Ighondokazini
#kilimoutiwamgongo
#Singidayetu
 

Attachments

  • IMG-20240430-WA0092.jpg
    IMG-20240430-WA0092.jpg
    48.4 KB · Views: 3
Ni hilo tu alilolifanya huko singida?kushuhudia mradi ukisainiwa? Mko nyuma ya wakati ndugu zangu, kiufupi kabisa,Singida bado haijapata chochote cha kujivunia ama kushukuru kwa sasa,labda baadaye sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom