Rais Samia karibu Singida

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
KARIBU SINGIDA "IYUU" SAMIA.

Rais Dkt Samia ana ziara ya siku 3 Mkoa niliyozaliwa wa Singida. Hii ni ziara yake ya kwanza Singida tangu awe Rais ambapo pamoja na mambo mengine ataadhimisha BIRTHDAY ya Mkoa wetu wa Singida kwa kufikisha miaka 60 tangu uundwe Octoba 15, 1963.

RATIBA:

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba, Mhe. Rais Samia atakuwa na ratiba katika Mkoa wa Singida kama ifuatavyo;

15/10/2023:

Asubuhi tutampokea Sagara akitokea Mkoa wa Manyara na kwenda eneo la Minga kuzindua Shule 12 za Singida zilizojengwa kisasa kwa mradi wa "boost".

Kuzindua barabara ya Itigi - Mbeya kilomita 56

Mkutano wa Hadhara Wilaya ya Manyoni utakaofanyika Itigi

Ataenda Wilaya ya Ikungi Kufungua Vituo viwili vya Polisi vya Kisasa vya Ikungi na Mkalama

Atasalimia wananchi Kata ya Puma iliyopo Wilaya ya Ikungi.

16/10/2023

Asubuhi Kuzindua Daraja kubwa Wilaya ya Mkalama

Mkutano mkubwa wa Hadhara Uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini ambapo ataadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa Mkoa wa Singida kwa kuoneshwa Makala maalumu tulipotoka, tulipo na tutapotarajia kufika kimaendeleo kama Mkoa. Baada ya hapo ataongea na wananchi.

17/10/2023

Ataenda mji mdogo wa Shelui Kukagua maendeleo ya Umeme vijijini ambapo hadi sasa vijiji 129 kati ya 180 vya Mkoa wa Singida vimewashwa umeme.

Kuzindua Mradi wa Maji Shelui- Ziwa Victoria.

Kama Mzaliwa wa Singida nina furaha mno kuwakaribisha watanzania kutoka pande zote nchini tukamlaki RAIS wetu mkoani Singida ambaye kwa muda mfupi amefanya Mapinduzi makubwa ya kimaendeleo mkoani Singida na Taifa kwa ujumla. Na ndio maana Singida ndio Mkoa unaoongoza nchini kwa kuwa na mahaba mazito kwa Rais Dkt Samia, na CCM.

Karibu "Iyu winthu" Samia.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
KAZI IENDELEE
SINGIDA GUNTOO!!

Suphian Juma Nkuwi
Kada - CCM
Mzaliwa wa Singidap
Simu: 0717027973
Octoba 13, 2023
IMG_20231013_131055_682.jpg
IMG_20231013_131055_694.jpg
 

Attachments

  • IMG_20231013_131055_694.jpg
    IMG_20231013_131055_694.jpg
    73.4 KB · Views: 3
Mwandishi nguli na Mwanadiplomasia Bollen Ngetti jana aliwapiga madongo ya matumizi ya hovyo ya fedha za umma kuchonga mabango ya Mama yenu vipi na nyie mmeyabandika?
 
Ah ah Mkuu sio wavivu bali wanalidhika mapema Yani mtu anaweza kwenda kibaruani Kisha akipata 10k apo kesho umuoni lakini nyuma yake watoto kama kumi ivi wanamuangalia kazi kuwatuma mchana jua Kali kutafuta zile nyanya poli kwenye mashamba ya watu na kuchuma mlenda (limbe) kwenye vumbi
Ni wajinga sn, lakini wana ardhi nzuri inakubali mahindi, alzeti, mtama, korosho, mbaazi n.k, MO kaiba kawaachia nyumba za tembe, Mwigulu anaiba kwa kasi then asepe zake wamelala tu hawa wajinga
 
Back
Top Bottom