Ufunguzi wa shule mpya ya sekondari ya sekouture - jimbo la Singida kaskazini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,079
1,002
UFUNGUZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA SEKOUTURE - JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI

UGUNGUZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI, MBUNGE IGHONDO ATAJWA KINARA WA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA ELIMU JIMBONI.

Mnamo mwezi Januari 09 2022 Wananchi wa Kijiji cha Sekouture wakiongozwa na Viongozi wao Walifanya hafla ya Ufunguzi wa Shule mpya ya Sekondari iliyojengwa kwa fedha nyingi kutoka serikalini . Wananchi hao kipekee kabisa wamemshukuru Mungu kwa kufanikisha wa ujenzi huo kwani kwao ilikuwa Ni ndoto , shule hii itapunguza kero ya umbali mrefu, na kata tano zitanufaika na Shule hio.

Katika Ufunguzi huo Wananchi hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kuwapatia fedha nyingi za mradi huo, huku pia kipekee wakimpongeza mbunge wao Mhe. Ramadhan Ighondo kufuatia juhudi zake za kuwasemea wananchi, ufuatiliji mzuri na nguvu ya uhamasishaji Hali inayopekea kutatuliwa kwa changamoto jimboni hapo.

Wananchi hao wamemmiminia zawadi nyingi Sana Mbunge Ighondo, huku Uongozi wa Kata, na chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ilongero pia kumtunuku cheti Cha Pongezi kwa juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo.

Wananchi wamewapa Viongozi wengine pia zawadi akiwemo Diwani wa kata Hiyo Mhe. Issa Mwiru, Diwani wa viti maalum, Mhe. Mwanamoshi Bakari na wote walioshiriki katika Ujenzi huo.
Diwani wa kata Ya Ilongero pia amempongeza Sana Mbunge Ighondo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Ilongero kwa kazi nzuri anayoifanya.

Huku Mkuu wa Shule Hiyo mpya na Wanafunzi wote walioripoti Shuleni hapo wakifurahi Sana uzuri wa mandhari ya Shule Hiyo.

Mara tuu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 Mbunge Jimbo la Singida Kaskazini Mhe. Ramadhan Ighondo alifanya ziara yake mapema kabisa jimboni ya kuwashukuru wananchi kufuatia kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo Hilo.

Katika ziara yake Hiyo wananchi walimwelezea changamoto mbalimbali ambapo katika sekta ya Elimu ilikuwa Ni upungufu wa miundombinu ya elimu ikiwa Ni madawati, Vyumba vya madarasa pia wanafunzi kutoka Umbali mrefu kusaka elimu,

Sehemu zote alizopita mbunge huyo katika jimbo lake kero kubwa ya sekta ya elimu ilikuwa Ni hiyohiyo.

Katika shule ya Msingi mwakiti Mbunge alijionea mwenyewe wanafunzi wengi wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati.

Mbunge huyo aliamua kuchukua changamoto hizo mara moja na kuzifikisha mahali husika huku akianza na mfuko wa jimbo katika kipindi chote uliopelekea kutengenezwa kwa madawati ya kutosha , ujenzi wa vyumba vya madarasa, ukamilishwaji wa nyumba za walimu, katika sehemu zote zenye changamoto.

Kwa upande wa Serikalini Ighondo amekuwa akiwasemea vyema wananchi wake na Hali iliyopelekea serikali kuliona jimbo la Singida Kaskazini kwa Jicho la umakini zaidi na Hadi Sasa Vyumba vingi vya madarasa vimejengwa na kukamilika pamoja na madawati yake kufuatia ufuatiliji na juhudi kubwa za mbunge Ighondo katika kutatua changamoto hizo.

Mpaka Sasa Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Mkimbii na Sekouture umekamilika kwa kiwango kikubwa kwani Mbunge huyo alifika maeneo hayo kuwahamasisha wananchi kupokea miradi hiyo na kuepuka kuihujumu.
 
Back
Top Bottom