Ifike sehemu Lema ajue kifo ni cha kila mtu. Aache kutishia watu vifo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,239
22,318
Ni aibu kwa kiongozi mkubwa wa chama kikuu cha watoa taarifa, CHADEMA, kukosa hoja na kutumia neno KIFO kutishia watu walio kinyume na itikadi yake. Huyu akishika dola si ataua watu wengi sana? Hakika kiongozi kama Lema ni hatari sana kwa usalama wa raia. Yaani ukiwa naye tofauti lazima akuambie UTAKUFA. Inashangaza sana. Lema jipe muda usome biblia Mwanzo 3 na Mhubiri 9 ili ujue kuwa kifo ni lazima kwa kila mmoja wetu ukiwemo wewe unayetishia watu kuwa WATAKUFA.

Pia elewa KKKT sio tawi la CHADEMA. Kama Askofu Shoo alikuwa mshirika wenu basi huenda Malasusa hataki kuchanganya siasa kwenye majukumu yake. Unachokifanya ni kuzidi kukididimiza chama chako na kuonekana ni chama cha kikristo. Epuka kushambulia kanisa kwasababu hata wapiga kura wenu hawawezi kuheshimu CHADEMA kama wanavyoheshimu kanisa. Kuendelea kumshambulia Askofu Malasusa ni kuzidi kupoteza kura zenu chache mlizo nazo.

Kwa kauli za Lema itoshe kusema kwamba CHADEMA imejaa madikteta wanaotamani kuona watu wenye maoni tofauti wanapoteza maisha.


View: https://www.instagram.com/p/C2WJylpNHY_/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==
 
Back
Top Bottom