Ifahamu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Majukumu yake

Nov 15, 2022
25
142
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 29(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 (iliyorejewa 2019) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma na kuanzishwa rasmi tarehe 1 Machi, 2010.

Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni;
  • Kutafuta wataalamu wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuhifadhi taarifa (kanzidata) za wataalamu hao ili kurahisisha utaratibu wa kuwaajiri pindi wanapohitajika;
  • Kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo Vikuu na wataalamu wenye weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea na ujazaji wa nafasi wazi za ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma;
  • Kuhusisha wataalamu maalum kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji;
  • Kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na ajira; na
  • Kufanya kazi nyingine yoyote inayoendana na majukumu yake kadri itakavyoelekezwa na Waziri.
 
Back
Top Bottom