Identification zetu JF zinaficha mengi sana

Identification zetu JF zinaficha mengi sana

Nimecheka sana kwahiyo jamaa ni mshua ana anae fake ombaomba au ni kapuku anauefosi ushua hebu nipe ulichokiona kwa mtazamo wako!
Nadhani jamaa niombaomba Promax na pia ana washikaji zake ambao wao wana ukwasi yeye akiwa na 50k akiungana nao basi bata linakuwa si la kawaida hicho ndo naweza kusema maana hata vaa yake si kutilia mashaka kabisa.

Huenda hapa jf alikuwa anaomba hata watu 50 kwa siku sasa mkuu wakitumwa watu 10 elfu5 ana sh ngapi?
 
Mitandaoni humu yaani ni changamoto sana ๐Ÿ˜€
Kuna I'd fulani ilini PM inaniomba hela ya kununulia gesi ya kupikia ghetto kwake ikanitumia mpaka namba ya Simu.

Sikumbuki kama nilimtumia hiyo hela, lakini kuna siku Nilikuwa naifuatilia ile I'd na zile content ambazo huwa anaandika. Nikabaki nashangaa tu hivi kwann Mtu anapenda sifa nyingi za kifahari lakini maisha yake halisi ni ya kuunga?
 
Nimejaribu kutafakari kwa kina juu ya mienendo ya baadhi yetu ndani ya jukwaa hili nikaishia kuwaza;

Ndani ya hili jukwaa Kuna watu wamejipa ukuu ila ni hakika yangu ukikutana nao lazma utapigwa na butwaa.

Kuna watu Wana tabia fulan ndani ya hili jukwaa ila naamin tungepata nafasi ya kujuana tungebaki tunashangaana

Ni Iman yangu kuwa ndani ya hili jukwaa Kuna watu wanakula mlo mmoja ila ndo wanaoongoza kwa kuanzisha nyuzi za kumiliki mpunga mrefu.

Ndani ya hili jukwaa Kuna waume za watu na kwenye jamii wanaheshimika lkn humu kutwa nzima wapo busy kuanzisha nyuzi za kutafuta warembo
Mm identification yangu inaficha nini.. ๐Ÿ˜‚
 
Hiyo ndio duniya sheikh wangu.....bila ivyo vifo vitokanavyo na stress vingekuwa vingi sana
 
Back
Top Bottom