I miss those days

I miss those days

I miss those days bibi harusi anatembea kwa miguu toka nyumbani kwao to Church na from church to husband's home.
I miss those days bibi harusi anakula keki na kushushia na chai ya moto.

I miss those days hakukuwa na michango ya sherehe za harusi. Sherehe zilikuwa zinafanyikia nyumbani na wachache waliokuwa na uwezo walipeleka
ukumbini.
I miss those days hakukuwa na kitchen party zaidi ya bibi harusi kufundwa nyumbani na Shangazi zake.

I miss those days kilikuwa na inner party baada ya sendoff na harusi. I miss those days hakukuwa na catering services wala mc na mziki, vyote hivyo vilikuwa vinapatikana kati ya ndugu wa sherehe kwa kunitolea.

I miss those days bibi harusi anaingiza ukumbini akiwa anaangalia chini na anatembea step za pole pole tap....tap.....tap

I miss those days looh
 
Dah, umenikumbusha tv yenye fomaica. Kuna siku mkanda ulizimikia kwenye deki my brother (RIP, ooh how i miss you. Sijui tungefanya mautundu gani na uzee huu sasa!) akaifungua akahangaika kuchomoa hadi akakata tape. Ukapigwa tape ikaeudishwa library kiroho swaaafi. Komesha dingi alikuwa anagusa tv kama imepata moto anajua wahuni mlishaharibu.

Most of all i miss my family. I dont wanna grow up <sob sob>
Hahahahaaa The Boss you know where we have our lunch lunch and you know where to find me looh.

Umenichekesha na kunifurahisha sana. Let me say this... Hii ni experience ya kwetu......
Mshua wangu alienda nje ya Tanzania miaka hiyo kikazi na aliporudi Tz moja ya vitu alivyorudinavyo ni TV ambayo kwa miaka hiyo ilikuwa ni asset kubwa. Kuangalia TV ilikuwa ni ijumaa jioni jumamosi kuanzia mchana na jumapili kuanzia mchana hadi jioni kisha inarudishwa chumbani kwa baba na mama na inalala huko. Operators wa TV na deck walikuwa kaka zangu very sharp. Sasa itokee mmeiba kuangalia TV katikati ya wiki halafu itokee umeme ukatike na mkanda umekwamia kwenye deck, na mkanda wenyewe wa kuazima......nakwambia kila mtu anaanza kusali ili umeme urudi kabla hamjabambwa maana mtapitishiwa kipondo woote. Hahahaaa
 
enzi za kusoma madeni China badala ya made in China

ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini ulinipa shida kuelewa maana yake mimi nilijua wanabagua rangi za ukutani nikawa najiuliza hizo rangi za ukutani wanabaguaje na kwanini wanazibagua.

Mkuu umenichekesha madeni china naikumbuka Sana hii
 
Dah, umenikumbusha tv yenye fomaica. Kuna siku mkanda ulizimikia kwenye deki my brother (RIP, ooh how i miss you. Sijui tungefanya mautundu gani na uzee huu sasa!) akaifungua akahangaika kuchomoa hadi akakata tape. Ukapigwa tape ikaeudishwa library kiroho swaaafi. Komesha dingi alikuwa anagusa tv kama imepata moto anajua wahuni mlishaharibu.

Most of all i miss my family. I dont wanna grow up <sob sob>

Makabati yenye fomaica enzi hizo mnatisha kitaa hahaa
vyombo vya glass hadi wageni waje....ole wako uvunje chupa ya chai....au glass dah....
 
enzi za kusoma madeni China badala ya made in China

ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini ulinipa shida kuelewa maana yake mimi nilijua wanabagua rangi za ukutani nikawa najiuliza hizo rangi za ukutani wanabaguaje na kwanini wanazibagua.

Nimeipenda saana madeni china maana mi nilikuwa mmoja wapo
 
I miss those days mikanda ya porno maskani walikuwa wanaifunika na cover za mwanamuziki Papa wemba au awilo longomba ili watoto tusijue kilichomo ndani
 
Dah nimekumbuka mashati ya yekeyeke....

yeke yeke hayakuwa mashati mkuu,, ilikuwa ni aina ya muziki nadhani

(sikukuu inanukiaaa aaa, eeee kuwa yekeyeke!! hahahaaaaaaa
 
Jamani hivi kitufe cha like kilishaondolewa???? au ni mimi tu?
 
Zamani Watanzania kila nchi tulijua imetupita kimaendeleo
watu walikuwa wanazamia hata Mozambique ...

mkuu,those days wanaume tulikuwa wanaume hasa!
"Tunachoma meli" tu!..,No Retreat,No Surrender!
 
I miss wali wa zamani ulikuwa na kaharufu kazuri sana , lazima tuoge mapema sana siku hiyo .
I miss those days marehemu baba akija usiku katupia vitu vyake anaweka cassete ya kanda bongoman anatushindanisha kukata mauno watoto wote mshindi anapewa sh.20 mara nyingi nilishinda

hahahahahahaha.....mkuu,yale matando na makoko yalikuwa matamu kuliko ubwabwa wenyewe!
Mi nilipigwa mwiko wa paji la uso na housegirl,hadi leo nna alama ya milele!....surprisingly,ndo akaja kuwa mama wa my first-born!..jembe langu la ukweli sana leo!
 
Makabati yenye fomaica enzi hizo mnatisha kitaa hahaa
vyombo vya glass hadi wageni waje....ole wako uvunje chupa ya chai....au glass dah....

Bwana weeee glass zenyewe zina manundumanundu kama sh tano. Sahani za madeni China maua maua ya kymwaga!
 
Hahaaaaa tena raha ya ko ko ko uivae kanisani...halafu uwe umechelewa misa....

Wakati wa mahubiri yanayogusa moyo watu wanamsikiliza mchungaji na siti zilizo empty ziko mbele....utakomwaje?
 
yeke yeke hayakuwa mashati mkuu,, ilikuwa ni aina ya muziki nadhani

(sikukuu inanukiaaa aaa, eeee kuwa yekeyeke!! hahahaaaaaaa
Kwakusaidia tu kipindi wimbo huo unavuma kuna mashati yalikuja nayo yakapewa jina hilo sijui kama unafahamu hilo!Yaani yalikuwa maarufu hadi watu wakafanya kama sare kwenye mpira!
 
Mkuu umenichekesha madeni china naikumbuka Sana hii
Uchina walikuwa juu sana katika vyombo vya udongo toka dahari,wanasifika kwa hilo....ila kwasasa wamezinduka kuchakachua kumezidi!
 
tena basi ufaulu.....tena ufaulu shule ya bweni nje ya mkoa...daaah! yani ukitembea mtaani unajiona kama unaelea angani. tulipata heshima haswa...leo masikini,wanaofaulu hawajui hata kusoma
those golden days zimebaki simulizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom