I miss those days

I miss those days

umenikumbusha zamani simu mpaka ipite kwa operator,waweza ukapiga weeeee unasubiri uunganishwe na operator. operator aliweza kusikiliza kila mnachoongea.
kulikuwa pia na simu zile za reverse call(tuliziita RIVASKOO).Unapiga kwa operator kisha yeye anakuunganisha na simu unayotaka kupiga kisha makato yanakuwa sio kwako ila kule ulikopiga...hii ilikuwa maarufu sana kwa wanafunzi wa sekondari wa shule za bweni.....
Ahhh...enzi za benki ya posta na vile vitabu vya posta haha utadhani pasipoti ya kusafiria.

Ninacho hicho kitabu cha bank ya posta na Picha yangu nimebana ufagio
 
Nimesoma humu nimebaki na tabasamu kimya kimya tu. Boarding school 🏫 enzi hizo ukipata money 💰 telegram (tulikuwa tunaita kitele) na mda wa kufunga shule umekaribia unakuwa mfalme wiki nzima washkaj wanakuzunguka kila kona usije ukabadilisha list ya kuwakopesha ukafanya ufisadi.. Nikiwatizama washkaj tukiwa kijiwe tunakula bata siku hizi kama watu na familia zetu nabaki nacheka tu
 
Mkuu umenichekesha madeni china naikumbuka Sana hii

Kila ikifika saba saba tunakwenda kiwanjani nilikuwa napenda kusoma bendera za mataifa mbali mbali ya Afrika, baba mmoja akaniambia nimsomee bendera ya Gine (Guinea) sasa mimi nasoma Guinea ilivyoandikwa kila akinirekebisha sikubali ikabidi anisifie tu kwamba najua kusoma
 
Song: Maiko Jakson njoo sitaki tucheze break dansi, maiko Jakson njoo sitaki kama hutaki nenda na ule wa Kuku kapanda basi kenda(kwenda) ferry bata kavaa raison hata maana ya hizo nyimbo hatuzijui la hazirudi hizo, mijukuu sasa hivi inalilia katuni ktk tv
 
Hahaha naona Kasinde umeamua kutupunguzia machungu ya kulazimishiwa watawala na kakikundi cha watu fulani.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha naona Kasinde umeamua kutupunguzia machungu ya kulazimishiwa watawala na kakikundi cha watu fulani.

Umeona eeh, wacha tuburudike mambo ya zamani ilikuwa rahaa, najua we enzi hizo ulikuwa bado uko bustani ya Eden.
 
Last edited by a moderator:
Kasinde ndio maana shikamoo jazz wakitia timu kwa mabinti hawachomoi siku hizi.
Ni kweli maana wana art ya kipindi kile so unique and romantic looh. Hata sie jazz band hatuchomoi, sio mvulana sasa hv a nakwambia. .. mi najua kuchinja viazi hadi maji ya natoka. Unabaki khaa hapo ndo kamaliza kutongoza hehee
 
those days tunarusha mawe juu ya bati ili utoke...au tunapita na kurudi uonekane.....
 
I miss those days, kombolela na vyakula vya asili. Thread kama hii vitoto kama Evelyn Salt havikanyagi
Those days nimechapwa sana Kisa kombolela, nimechapwa sana Kisa vibarua vya mapenzi nmekula chunvi ujue teh
 
Last edited by a moderator:
Kioo kiooo alikivunja naniii

Sijui sijui, wa mwisho akamatwe atiwe gezerani

Huu mti gani,; wa mchongoma
Nikiukata, haukatiki
Hata kwa panga; haukatiki
Hata kwa shoka; haukatiki

Bilingo bayoyo Bilingo bayooo
Tunamuomba dada heaven aingie kati tumuone maringo yake
Bingili bingili mpaka chini
 
Those days mtoto wa mwalimu unapendwa na kila mtu. Mbaya zaidi mnakaa kota alafu kidume ndio wewe tu. Dah lotima napakumbuka sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom