I miss those days

I miss those days

Ebana eeeh hiyo ni kweli kabisa.

Nakumbuka kuna watu walikuwaga wanaenda Zaire kununua viatu na kuja kuviuza Dar.

Basi wengine tulikuwa tunaona Zaire imeendelea sana.

Mi nakumbuka kuna mjomba'angu mmoja hivi mjeda...aliendaga Msumbiji akarudi na nyanya za kwenye kopo [tomato paste] na corned beef za huko.

Basi nilikuwa naona jamaa wameendelea sana hadi wanatengeneza nyanya za kopo.

Hahahaa ujinga kitu kibaya sana.

Manake kigezo cha maendeleo tulichokuwa tunakitumia ni cha vitu na si watu.

Wakati maendeleo ya kweli ni ya watu na si vitu.


Na watu wakitoka Nairobi tunaenda kuwasalimia ha ha haa
haki ya Mungu hii nchi ilikuwa burudani...
Mtu akienda Ulaya ukoo wote mnaenda airport kumuaga...

Halafu kuna maeneo kupiga picha mnakamatwa na polisi....ha haa
 
Hahahaaa umenikumbusha mchezo ya zamani looh, kombolela, kibaba baba na kimama mama, mate ka, kula mbakshie baba, kiskio poo, rede, vichupa daah.
Ila hapo kwenye kombolela kujificha watu ndo tulijifunzia mechi za mchangani. Unakuta umejificha na mvulana ambaye unampenda na mko wawili tuu mlipojifichia .......

Hahahaha dah brilliant
 
I miss those days hapakuwa na wapambe. .. .. .

I miss those days ukumbi wa harusi unapambwa kwa toilet papers za pink na light blue.

Haahaahaa! Hapo umeuaa! mbafu sangu mie! Dah! Kweli tunatoka mbali
 
enzi za kusoma madeni China badala ya made in China

ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini ulinipa shida kuelewa maana yake mimi nilijua wanabagua rangi za ukutani nikawa najiuliza hizo rangi za ukutani wanabaguaje na kwanini wanazibagua.

Hahahahahaha mie hoi we jamaa ulikua kiboko
 
I miss those days...wakati mbalamwezi inawaka usiku mnacheza sana
 
I miss those days mikanda ya porno maskani walikuwa wanaifunika na cover za mwanamuziki Papa wemba au awilo longomba ili watoto tusijue kilichomo ndani

Hahahahahaha mbavu zangu weee utoto kaaazi kweli kweli
 
Umenikumbusha mbali sana
Sketi ya charanga kwa mara ya kwanza nililetewa na demu wake na broo
 
I miss wali wa zamani ulikuwa na kaharufu kazuri sana , lazima tuoge mapema sana siku hiyo .
I miss those days marehemu baba akija usiku katupia vitu vyake anaweka cassete ya kanda bongoman anatushindanisha kukata mauno watoto wote mshindi anapewa sh.20 mara nyingi nilishinda

Tena uwe wali maharage nyama ilikua sio dili, ila now watu wanapenda nyama sana sijui ilibadilikaje
 
I miss those days unachagua demu badoo unasomesha next day you meet una...
 
Du...umenikumbusha mwanzo ngoma ilikuwa inaitwa Juliana...

Na sababu ilikuwa hayo mashati yalikuwa yakijumuliwa huko Uganda na wafanyabiashara wengi walikuwa wakirudi na ngoma...
 
Kwenda shuleni na kiti cha jikoni na ufagio mkononi
 
wakati wa mbalamwezi usiku mnakaa chini ya mwembe mkisubiri maembe yadondoke baada ya popo kutingisha akitaka kulala,, likidondoka ni kugombaniana acha kabisa!!
 
enzi za kusoma madeni China badala ya made in China

ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini ulinipa shida kuelewa maana yake mimi nilijua wanabagua rangi za ukutani nikawa najiuliza hizo rangi za ukutani wanabaguaje na kwanini wanazibagua.

Hahahaa mkuu nimecheka sana hiyo madeni china...ndo zilikuwa zangu kumbe tulikuwa wengi lol.... Heaven Sent we ulikuwa unasomaje kwa mfano
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom