I don’t wanna marry him, what should I do?

Hehehe nawashangaa wanaume wanavyomwaga povu kwenye huu uzi yaani nawashangaa sana aisee
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hata mimi mwenza siwaelewi ujue[emoji1745][emoji1745][emoji1745]
 
Wanawake ni watu wa ajabu mno...! Hamueleweki mnataka nini maishani, ushamtumia wee leo waona hakufai, mwambie ukweli lakini ujue kuwa wakati utapofika wa wewe kumtaka umpendae haitakuwa rahisi sana kwako, na utamuita huyo unayetaka kumuacha na wala hatogeuka kuusikiliza wito wako.
 
Dunia haiko fair huyo anayekupenda unamuona sio wa maana unayempenda wewe anakuona wewe sio wa maana kuna siku na saa utakuja kumjutia huyo kaka... natamani nikushauri kwa namna ambayo ungeweza kunielewa ila utakuja kuelewa siku yatakapokukuta
 
Dah ,aiseee....
 
Nimejitahidi sana kwa kipindi chote hicho ila sikuwahi na sidhani kama nitaweza. Imefikia hatua i just hate everything about him. Kumbuka hata hii ya kuishi pamoja sikuwahi kuifurahia.
Kama ni hivyo hakuna sababu ya kuwa sijui na huruma, au kushindwa kumwambia,tell him unajisikia, hata Mungu atakusimamia, na pia Mungu atajua huyo mwanaume amletee mwanamke yupi wa kufanana nae.. Umefanya vibaya sana kukaa kimya muda wote. " Baba hapendi".
 
Hao ndio wanawake bwana

Sifa yao kubwa ni kwamba ---hata wao wenyewe hawakijui wanachokitaka
Acha tu mkuu.Ni vile baai hatuwez kujizuia kupenda ila mapenzi ni upumbavu uliotukuka sanaa
 
Mwanaume usiyempenda kweli anaweza kufanya hivyo na ukamwachia tu ukaendelea kuishi naye kwa miaka miwili na nusu anakukula na kukuhudumia we umeuchuna tu? Khantwe siamini !!!
Two years an a half ..man.!!!!?,asije kuuwawa huyu dada, mapenzi ni jambo la hatari sana
 
Kabisa,hasara ya jamuhuri inajulikanaga kabisa,hasa kwenye suala la mapenzi.
 
Hahaha Soo True

Mazee hii kweli kabisa. Hata dem awe mpole mkarimu mtaratibu vp...unavyozidi kumtukuza tu ndio unazidi kuharibu.

Ishanikuta sanaa hii.

Na zile tongoza za kubembeleza ndio kabisaaa
Kweli kabisa,wanasema mwanamke kwa kadri unavyotaka kumuweka karibu ndio unavyopoteza uwezekano wa kuwa nae,hawa viumbe aisee,..
 
Hahaha kwa hiyo mtu kusema biashara zangu ni kosa? Katika eneo hilo alitakiwa asemeje eti, biashara zetu? Wanaume watu wa ajabu sana ninyi
Neno zangu,mimi ,yangu, ni sumu sana kwenye mahusiano,mtu mwenye u- mimi ..hata huwa salamu simpi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…