Huyu Pogba wetu ni hasara tu

 
Naweza kufikiri haya siyo makosa ya POGBA, tumlaumu zaidi Aliyemkataa yule mchezaji wa zamani mwenye uzoefu na kumkimbilia POGBA. Mashabiki wote walisikika wakiimba wanaimani na yule mchezaji wa zamani lakini Mkataji aliona HAPANA...POGBA atatufaa tu.

Kila siku Pogba amekuwa na visasi vya ajabu ajabu, anatoa pasi akitaka, anakuondoa hata kwenye team akitaka. anapendekeza nani awe kipa nani au mlinzi wa kati...anachagua team. usipomsifia akifanya madudu uwanjani ujue una hatihati ya kutolewa kwa mkopo..

Kuna yule mchezaji toka jiji mashuhuri ameweza kudumu kwenye number baada ya kuonyesha ushabiki wa makosa ya POGBA uwanjani...

Kelele za mashabiki hazimzuii POGBA kucheza FYONGO... ngoja tusuburi dirisha dogo tumsajili mbadala wa POGBA toka team Pinzani...
 
duh!!!pogba anatuchomesha sana!yan team imepotean kabsa cjui tutumie mfumo gan ili aperfom vingnenevyo mpk mkataba wake unaisha timu itashuka daraja.
 
Nadhani POGBA ana tatizo sio kama wachezaji wenzake waliowahi kununuliwa kwa bei kubwa. wenzake waliacha mbwembwe . lanini pogba bado anamajisifu na kujiona yeye ndio manyuuu, anabadili mikato na rangi za nywele.

ila najiuliza mbona haitaji ile rangi ya team yake? hivi huyu ni manyuu kweli? Kweli POGBA anatuharibia team,....
 
`bonge la fowadi` Pogba sio fowadi,,, nenda kwa Edo kumwembe akufundishe uchambuzi
Siku nyingine soma Kwanzaa uelewe ndio ujibu leo tupo na Paul pogba kule team coach sizonje hatari hatari
 
Pogba nasikia anajiapiza kuzinyoosha timu kwa kufunga magoli mengi huku kumbe anatoa kitu kidogo kwa makipa....kama vile 10m ili apewe magoli ya chee
ETI APIGE PENATI BILA KIPA KUWEPO!
 
Siku nyingine soma Kwanzaa uelewe ndio ujibu leo tupo na Paul pogba kule team coach sizonje hatari hatari
Qwi Qwi Qwi.... Huyu jamaa ni Div V kabisa!! Eti nenda kwa Edo Kumwembe akuelezee kuhusu Pogba wa Man U!!! Fasihi kidogo tu inamshinda?
 
Tatizo yeye ni ni kiungo....

Wakati huo anataka kuwa forward.....


Wakati huo anataka kuwa beki........

Sometime anataka awe Goalkeeper...
Mtu mmoja huyo huyo? Kwa mechi moja ama mechi anuwai?
 
Na Baadae mtasema miaka miwili ni michache sana kama awali mlivyo sema Siku mia ni chache.
Pogba ameishiwa mbinu kila siku ni ugomvi na wachezaji wenzie. Na mbaya zaidi ni kwamba Kila akikutana Na washabiki anaomba Wamuombee hirizi yake ili iwe na nguvu zaidi!!
 
Nasikia pogba analalamika hakujua kama hii kazi ya uchezaji ni ngumu,ange-sign mkataba wa miaka miwili tu na siyo mitano
Kila Mtu Man U anatamani Van Persie asingeuzwa. Van Persie alikua mtu wa majeraha ila alikua akifunga Magoli na hasa magoli Muhimu.
 
Acha Uchochezi bana!! Sisi tunamzungumzia Pogba na Man U. Qwi Qwi Qwi...
 
Teh teh teh.... huu uzi umewapiga Chenga watu wengi sana, hasa wale wasomaji wa magazeti ya Ijumaa na kiu bila kuwasahau waangaliaji wa Bongo Muvie.
 
Pogba bana alivyo kuja alisema Man U ya Pogba itakua Man U ya magoli yaani atafunga magoli akiwa kwenye kona yoyote uwanjani. Sasa Msimu umeisha hatuoni magoli!! Mbaya zaidi mpambe wake anasema Pogba kashafunga Magoli 3800, sasa sijui alikua ajiyafunga akiwa mazoezinii au alikua akiyafungia bafuni!? Qwi Qwi Qwi
 
Ndo kwanza dakika ya 20 kipindi cha kwanza Pogba kakata moto.....pumzi ndogo route ndefu
 


Hongera mkuu unatisha kwakweli[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…