The whole thing is NONESENSE, kwani aliyekuwa nataka misifa si yeye mwenyewe, sasa anataka kutudanganya kuwa hapendi misifa na sisi tunakubali?
No ni yeye aliyeanzisha kampeni za misifa, mpaka kutajwa tajwa na Twanga pepeta, kuwa mtu wa watu mbona asiseme then kuwa waache kumpa sifa, why now?
Alipokuwa akipewa zile sifa kule mwanzoni alikuwa amfanya kitu gani cha maana, sasa anchokataa ni nini, mimi ningetegemea angekubali publicly kuwa ametuangusha wabongo maana hana sifa za kuwa rais ana angeomba radhi badala ya kutumia ujanja wa kukaripia watu wanaomsifia, wakati ule Mkapa anamsifia kwenye kampeni alikuwa anasifia nini?
Wakati mtandao wanaiponda serikali ya Mkapa mwanzoni na kujifanya wao ni wajuaji walikuwa wakijisifia kitu gani? Wabongo hebu taumke na tuache kukubali huu usaniii, guys litsen hawa mtandao ahwana lolote ni usaniii tu na hii ya Muungwana kujifanya hataki misifa ndio hasa usaniii wenyewe!
Huwezi kuwandanganya wananchi kwa muda mrefu, sasa ukweli umejitokeza wazi for everybody to see kwamba Awamu ya nne ni wasaniiii watupu, mawaziri 60, hawana jibu la kitu kidogo kama umeme, maneno mengiiiiiiii oooh mimi nimeeenda Wall streeet, rais wa kwanza blah blah blah blah, ooh yea sasa hutaki tena misifa, acheni usaniii mmeshindwa kubalini yaishe!
Alichopaswa kusema kwenye huo mkutano ni kuwaomba radhi wabongo na taifa zima, kwa kuishusha hadhi ya urais, na kutokuwa na uwezo wa uongozi mzito kama huo, nigeeelewa, lakini sio kukataa misifa maana ni tabia aliyoianzisha yeye mwenyewe alipokuwa akiwalipa wapiga muziki wa Twanga wamtaje taje bila sababu!
Muungwana JK, tulijua toka wakati wa uchaguzi kuwa yeye na kundi lake la mtandao kisiasa wana tatizo kubwa, maana zile kampeni hazikuwa za kawaida kwa nji yetu masikini. Hela za kampeni zilikuwa nyingi mno, kuharibu majina ya wanasiasa wengine kwa makusudi ili tu wapate power,
Wakaenda mpaka kuiharibu katiba na mwenendo wa uchaguzi wa CCM, wakatishia mpaka kwamba nji haitatawalika iwapo hawatapata, wakawaharibu watu babu kubwa kama kina Salim, maneno mengi, tulijua kuwa ni upepo tu na nguvu ya soda, tuliposema mapema tukatukanwa matusi mazito kule BCS, tulipojaribu kuwasihi wabongo waamuke usingizini, maana they were about to commit the worst political mistake ever, wakatujia juuu, sasa here we are!
One year tayari wananchi wamechoka, tena choka mbaya maana wamepigika ile mbaya na hawana hamu, leo eti Muungwana hataki misiifa, ebo! hataki misifa kwa vipi? Yaani anatuona sisi wabongo wajinga? au? Hebu atuambie zile misifa aliyokuwa akipewa hata kabla ya uchaguzi na kina Kingunge, Tido Mhando mzee wa polls za BBC, watu wa Mlimani, zilikuwa ni sifa za nini? Aliwahi kufanya nini cha maana kabla ya kuwa rais? Hebu kuweni wakweli what didi the man do?
Muungwana toka siku ya kwanza ulipoanza hizi kampeni za urais you were wrong, sina tatizo na Muungwana personally, lakini kiuongozi I do, kwa sababu you just don't have it, kule mwanzoni nilisema kwamba kile tu kitendo cha kuwapa watu 60 uwaziri, mpaka Ikulu viti havikutosha kwenye mkutano wa cabinet, ilikuwa tayari dalili za ku-go home.Mimi ninasema katika awamu nzima ya nne tuliyonayo, ninamuona kiongozi mmoja tu angalau mwenye nafuu naye ni Mama Migiro, wengine wote wanaweza kufunga virago waondoke na taifa letu litakuwa just fine! Yes we will be just fine, I mean what are these people doing? Kuna mliosema tumpe muda, sasa tuambieni tufanye nini sasa?
Eti leo hataki misifa tena? Mzee JK na kundi lako tafuteni njia za kujiondoa kwenye madaraka, kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuwaondoeni, na hatuwezi kusema eti mnaweza kuwa rehabilitated kwa sababu mtu anyekuwa rehabed, ni yule ambaye kabla ya kuwa na tatizo alikuwa sawa, sasa nyinyi hamjawahi kuwa sawa, ndio maana hiyo option haipo, nyinyi ni kuondoka au mkiendelea acheni ngebe ngebe,
nyamazeni kuleni mapesa ya kodi zetu wajinga, hakuna hope maana Chadema nayo ndio hivyo tena taifa zima tutaishia kulazimishwa kula kisusio for breakfast na kusikiliza miziki ya Jimmy Reeves na Dolly Parton!
Mzee ES: Ulimsifu sana JK mwanzoni. Ulikuwa na safu yako inaitwa kitu kama: Kikwete Huyoo! Na alipomsimamisha Mahalu, ulilitoa hilo kama mfano wa uchapaji kazi hodari! Naona alikukatisha tamaa baadaye, lakini kwa uzito wako, ilibidi uweze kuona ukweli tangu mwanzoni.
Maji ukishayavulia nguo, sharti uyaoge. JK ndiye Rais wetu sasa, na cha muhimu sana ni kuangalia taifa lisizorote mno kutokana na ukweli huo. Ili kunusuru uchumi wa taifa letu, napenda kushauri yafuatayo yafanyike:
Augustine Moshi
- Kuwe na badiliko katika Baraza la Mawaziri, na nafasi hiyo itumike kuwapunguza wabaki si zaidi ya 20.
- Arudishwe Dr. Kigoda kwenye ofisi ya Rais kama waziri atakayesimamia uchumi.
- Ateuliwe kiongozi wa hali ya juu kushika wadhifa wa Gavana wa BoT, na azingatie kuhakikisha shilingi haishuki thamani yake kiholela.
- Upelekwe mswada wa fedha (mini budget) bungeni ambao utaongeza kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya Elimu kwa asilimia 100. Fedha hizo zitoke kwenye karibu shilingi trillion moja zilizoachwa Hazina katika bajeti inayotumika sasa.
- Upelekwe mswada bungeni utakaolazimisha mikataba kati ya nchi na wawekezaji kujadiliwa na kupitishwa na bunge kabla haijaweza kuwa sheria.
- Miktaba ya madini iliyopo sasa ipitiwe kwa dhati, na tusikubali ruzuku. Kwa mfano, Barrick Gold wanamiliki aslilimia 75 tu ya hisa za mgodi wao wa dhahabu uliopo Papua New Guinea. Zilizobaki ni mali ya Papua New Guinea. Kwa nini watwae asilimia 97 hapa kwetu?
- Upitishwe mswada wa kukataza matumizi ya fedha zaidi ya shilingi. Malipo yote mahotelini, vyuoni na kwingineko yafanyike kwa fedha zetu. Iendelee kuwa halali kuwa na fedha nyingine, lakini malipo yote hapa nchini yafanyike kwa shilingi ya Tanzania.