Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,569
- 19,442
Ni kweli kuwa kuna mambo mengi tu ya kiuchumu ambayo Nyerere alikuwa too utopian kwa kuchanganya sana siasa za kimataifa na uchumi wa nchi changa kama Tanzania. Alitakiwa awe makini sana. Vita siyo lelemama, hata leo Marekani wanajutia kujihusiha na vita ya Iraki. Tanzania ilijihusiha na vita nyingi sana katika eneo hilo la afrika kuanzia mwaka 1968 hadi 1980.Jizaledo said:Kichuguu,
Katika kuthamini ubinadamu Mwalim alikuwa msitari wa mbele sana lakini kamwe hakujali tahadhari yakujihusisha katika mambo ya watu wengine kwa uchumi wetu.
A Brief Background:
(a) Baada ya uhuru, effort ya viongozi wa kwanza wa afrika ilikuwa ni kuungansiha bara la afrika ili taifa moja kubwa (USAfrica).
(b) Tanzania, Zambia na Zaire zilikuwa ni nchi pekee za Afrika mabazo zilikuwa zinapakana na makoloni, na kulikuwa na kero zake hasa kuhudumia wakimbizi na mambo kama hayo; kwa mfano mwishoni mwa miaka ya sitini tulikuwa tunapigwa mabomu na Wareno kule Ruvuma mara kwa mara.
(c) Baada ya mapinduzi Zanzibar ilijenga na uhusiano na Ujerumani ya Mashariki wakati bara ilikuwa ikisaidiwa na Ujerumani Magharibu kujenga barabara, hospitali ya ocean road na sikumbuki sawasawa kama ilikuwa ni pamoja na nkurumah hall ile ya chuo kikuu. Ulipofika wakati wa Muungano, ambao kuna maandiko yanayoonyesha kuwa ulikuwa umetengezwa zaidi na mataifa ya magharibi ili kupunguza kasi ya ukominist kuingia sehemu hiyo ya dunia, nchi za Magharibi zilimuambia Nyerere kuwa fukuza ujerumani mashariki ama sivyo sisi hatutakusaidia. Hii ilikuwa ni dharau ambayo mchonga hakuivumilia; akawaambia kuwa chukueni mali zenu muondoke. Wajerumani wale walibomoa sehemu ya barabara lami ambayo walikuwa wameshweka na kuna taarifa kuwa Nkurmah hall haikumalizika.
Sasa basi mchanganyiko wa mambo haya ulisababisha Nyerere (a) kuthamini sana africanism (b) kupunguza imani kwa mataifa ya nje na ndiyo maana akaja na sera za kujitegemea; huu ndio ulikuwa mwazo wa siasa za Ujamaa na Kujitegemea:- Nyerere aliyesomea Uingereza hakuwa na background yoyote ya Ujamaa kabla ya hapo, (c) kuyachukia mataifa ya magharibi ambayo yalikuwa yanashirikiana na makaburu na wareno against Africanism, na hivyo kupigana nayo.
Inawezekana kabisa mazingira yalimlazimisha kufanya hivyo, ilia yeye alizidi sana. Waswahili wanasema wema usizidi uwezo. Niliwahi kuishi na watu kutoka Zimbabwe ambako Nyerere aliwahi kupeleka batallion nzima kupigana na smith; wala hawakumbuki kuwa kuna askari wa Tanzania waliwahi kupoteza masiha yao kwa ajili ya uhuru wao. In fact wanacheka sana kuwa Tanzania pamoja na kupata uhuru miaka mingi bado haijafanya lolote la maendeleao. Jamaa wa afrika ya kusini ndiyo wacha kabisa. wanasema Tanzani ni "third world." wengi wao hawajui kama Tanzania ilisadia chochote katika uhuru wao. Kwa hiyo investament yetu kwa uhuru wao haikuleta faida yoyote kwetu sisi.
In general, Nyerere hakuwa na restraint ya kuhakikisha kuwa hamalizi resources za nchi katika vita zake za ukombozi ingawa vita hizo zilikuwa za halali
Hebu jaribu kufanya uchunguzi kwa Wananchi wa kawaida, ambao ndio wanaomatter hapa wakuambie ni awamu ya Raisi yupi maisha yao yalikuwa na nafuu; na ninakuhakikishia Mzee Ruksa chati yake utaiona iko juu kiasi gani.
Mimi siyo mmoja "mwananchi wa kawaida" kwa sababu naangalia maendeleo kwa maana halisi siyo kwa maana artificial. Watu alimwita Mwinyi ruksa kwa vile alipopata pesa za mkopo akazitupa mitaani bila uangalizi wowote hivyo kutoa ruksa kuzitumia; hivyo kila mtu alaweza kujipatia kwa namna moja au nyingine. Nilikuwa nakutana na watu kwenye baa wakiwa na shiling milioni kumi mfukoni kwa ajili ya kulewea wakijua kuwa kesho yake wangepata nyingine.
Hata akipatikana mwendwazimu asiye kuwa na plani yoyote ya wapi anataka kuipeleka nchi, lakini akawa anagawa hela hovyo hovyo kwa kila mtu, utashangaa kuwa kuna waswahili wengi watampenda.
Hicho huwezi kukitumia kuwa ni kipimo cha uongozi mzuri. Ametelemsha sana hadhi ya Tanzania. Wakati Mwinyi anapokea nchi Tanzania ilikuwa ya 18 kutoka chini. Wakati yeye anaondoka madarakani aliiacha Tanzania ikiwa ya 8 kutoka chini, yaani kila mwaka ilikuwa ikishuka daraja. Mkapa amepokea ikiwa ya 8 na kuiacha ikiwa ya 4; alipinguza kidogo sipidi ya kuporomka labda kwa vile nchi ilishafika bondeni tayari.