Huyu ndiye Mkullo

STEPHEN JR

Member
May 21, 2011
14
3
Wana JF mmemsikia waziri mchovu wa fedha Tz anasema eti pesa yetu inaposhuka thamani eti serikali yao haina la kufanya kwa sababu ya uchumi huria,kweli ni timamu huyu? Wachumi wenzangu tusaidiane kumuelimisha huyu
 
Kwa kauli hii, inaonekana hajui anachosema kama yule mkubwa aliesema hajui kwa nini waTZ ni maskini!
 
Wana JF mmemsikia waziri mchovu wa fedha Tz anasema eti pesa yetu inaposhuka thamani eti serikali yao haina la kufanya kwa sababu ya uchumi huria,kweli ni timamu huyu? Wachumi wenzangu tusaidiane kumuelimisha huyu

kinachoteremsha thamani ya pesa yetu ni ufisadi kwa sababu gharama za uagizaji huduma mbalimbali kutoka nje haziwezi kuzibwa na makusanyo ya humu ndani kutokana na mirija kibao iliyojengwa na watendaji serikalini.....................hata mkaguzi mkuu wa serikali Ludovick utouh yupo pale kulinda ufisadi tu.........................na ndiyo maana mafisadi wanaendelea kumteua aendelee kwenye nafasi yake.........
 
Yuko sahihi na si kulaumiwa kwa matamshi yake bali Serikali na policy zake za privatization with free market economy.Iwapo katika sera ya soko huria Serikali haikuweka exclusive clause ya Government intervention pale uhuria wa soko unapo athiri watu wake basi hapa maneno ya Mkullo yana prevail.

Nchi makini haiwezi kuruhusu soko huria kutawala uchumi wake na wananchi wake.Hapa kuna njia kuu mbili za kuiwezesha Serikali kumiliki uchumi wake nazo ni ''fiscal policy'' na ''monetary policy'' vyote hivi vinaweza kufanya kazi pindi ''pump priming policy'' imekuwa imposed in good manner.

Watendaji kazi wetu kwa sasa hasa TRA,Wizara ya Fedha na BOT wametupa mbali taaluma zao,wengi wako katika utafutaji wa kujinufaisha kwa kujilimbikizia vipato,hawa ni wapenda safari za nje kwa kigezo cha kujifunza kumbe ni njia ya kufanya biashara zao binafsi na si shule.


Ukweli wa haya yote ni shida zinazoendelea kutukumba huku tukijidai kuwa tunawasomi.Shule usipoiendeleza ni sawa na kutokuwa na shule.
 
Wana JF mmemsikia waziri mchovu wa fedha Tz anasema eti pesa yetu inaposhuka thamani eti serikali yao haina la kufanya kwa sababu ya uchumi huria,kweli ni timamu huyu? Wachumi wenzangu tusaidiane kumuelimisha huyu

Kama BOT ingekuwa na watu makini a substantial amount of our reserves would be in Gold ; ambayo sasa hivi bei yake inapaa kwenye soko la dunia hivyo basi ingekuwa rahisi kuitumia dhahabu hiyo kustabilize shillingi yetu!!
 
WanaJF, hivi mnajua elimu ya Mkullo?? Hakufaa kabiisa kuwa waziri wa fedha. Hajui alisemalo
 
Uchumi huria umeanza awamu ya nne? Mbona awanu ilopita shilingi ilikuwa stable. Mkulo and the whole cabinet are failures.

Awamu ya nne ilipoingia madarakani ilikuta large amount of foreign reserves. Na hii ilitokana na exports, walichokifanya wakaanza kutumia kwa safari za nje na ku-release reserve to local market ili kustabilizing exchange rates bila ya kuwa strong exports ku-replace them. matokeo yake mafisadi waliokuwa na mabilioni ya hela za madafu wamezinunua na kuzihamishia kwenye offshore accounts zao. Nchi imebakia na deficit ya forex while demand is high(to sustain imports, e.g oil etc) what do you expect?, the price of forex going up.

Hapa ni mchanganyiko wa yote, poor economy due to the lack or decrease of exports while import we have increase in import(which needs forex) and poor monetary policies. walipoingiamadarakani wakaona kama vile "John Silver" and treasury island, wakajua hazitaisha, mara mikataba ya umeme wadharura kwa washikaji yote inalipwa by USD, yaani Group la Mtandao liliingia madarakani kwa style ya "Locusts" Nzige wakaanza kutafuna mazao huku wakijisaidia mpaka shamba sasa limebaki jeupe, wanaoathirika ni ordinary citizens.

Tanzania tuna dhahabu na madini ya kila aina, kwa mikataba mibovu, ni kwamba kinachofanyika ni mavuno yasiyokuwa na faida kwa nchi, tungekuwa na policy ya mauzo yote ya madini nje pesa zake lazima zirudi Tanzania as forex na kuhifadhiwa kwenye mabank ya nyumbani, tatizo hili lisingekuwepo Shilingi ingekuwa stable, ila wanauza na pesa inabakia hukohuko walipouza nchi ya ajabu kabisa hii.
 
tatizo la wahamiaji kuongoza nchi tunamalizwa kama russia huyu jamaa hana mipango makini wala hana huruma na mtanzania


true huyu mmalawi na hajawahi kuomba uraia....baba yake alikuja naye morogoro amemshika mkono......,baba yake alikuja kufanya kazi ya umanamba kuvuna mikonge.......baada ya pale hakurudi tena malawi ...akawa amemwandikisha shule mustapha........so huyu kazaliwa malawi ....nashangaaa wanamuonea bashe wakati bashe kazaliwa hapa....au ubaguzi wa rangi?

Mwaka jana wakati wa uchaguzi kuna wazee wa moro walikuja dar kumtaka mkulo asigombee ubunge kwa kuwa sio raia.....kwani wao pia walikuwa na baba yake kwenye kuvuna mkonge hiyo miaka ya 60" na walimuona mkulo ameshikwa mkono na kikaptula chake bila viatu anaingia tanganyika...sijui alimalizana nao vipi!
 
Viongoz wetu hawajui chanjo cha matatzo yetu. Watayatatua vp?
 
Tanzania matatizo sugu ambalo ni udini ambalo limetuletea
1.migawanyiko katika jamii
hakuna tena umoja wa kitaifa imebaki "wao na sisi" raisi anachagua viongozi wakuu wa serkali kwa kuangalia imani za dini kuliko uwezo wao wa utendaji kazi, viongozi wabovu wana support kubwa kutoka kwa wananchi wenye imani moja. Misemo kama "sasa ni zamu yetu" inasikika mitaani ikisemwa na wananchi wa kawaida, wengi wao hawana unafuu wowote kiuchumi.

2. Mamlaka makubwa ya raisi
katiba iliyopo inampa mtu mmoja madaraka kupita kiasi hasa uteuzi wa watumishi wa serkali na idara zake. fikira kila mfanyakazi mwenye cheo cha ukurugenzi na kwenda juu ni mteule wa rais, hii inasababisha viongozi kujipendekeza na kushindwa kufanya kazi kulingana na taaluma zao, hawawajibiki kwa wananchi wanaowatumikia bali kwa bwana wao aliowateua "pangu pakavu phenomenon" katiba mbovu namna hii inampa rais nafasi nzuri tu ya kuweka kila kona watu anaowapenda, hii siyo hali nzuri hasa kipindi hiki ambako jamii inaendelea kupasuka kwa misingi ya dini. rais anaweka madarakani watu wa kundi lake na katiba inamruhusu

3. Udhibiti wa uraia
nchi ambayo haijui nani ni raia au siyo raia wake haiwezi kuendelea hata kidogo, maendeleo huja kwa kazi ngumu na unchungu wa wananchi kuziendeleza na kusimamia raslimali zao. wasimamizi wa raslimali zetu wanatajwa kuwa wamalawi, wasomali, wacongo, wanyarwanda, warundi nk nk huku wamiliki wa biashara kubwa kubwa ni wahindi na waarabu. To be honest tanzania ni nchi pekee duniani ambako watu ambao siyo raia wanamiliki uchumi wa nchi na ni viongozi wa ngazi za juu serkalini. Hii hali inachangiwa sana na udini maana, mmatumbi anamwona mpakistani kuwa ndugu yake wa karibu zaidi kuliko mmatumbi wenzie anaetofautiana nae kiimani.

3. Ujinga wa wananchi
Dini zingine zinachangia kwa kiasi fulani kuwakosesha watanzania elimu bora, sehemu kubwa ya jamii ya kitanzania bado ni mbumbumbu. Ujinga wa watanzania ni mtaji mkubwa kwa wageni na watawala dhalimu na ni hatari kwa raslimali za nchi

UDINI UNAIMALIZA TANZANIA
 
Sio kosa lake, kilaza mkuu ni yule aliyempa hiyo kazi ya kuhesabu njuru za taifa.
 
Wana JF mmemsikia waziri mchovu wa fedha Tz anasema eti pesa yetu inaposhuka thamani eti serikali yao haina la kufanya kwa sababu ya uchumi huria,kweli ni timamu huyu? Wachumi wenzangu tusaidiane kumuelimisha huyu
<br />
<br />
amageuka NDULU,anafanya kazi za BOT,aseme hayo maneno ni idea yake au ameambiwa toka BoT?????
 
Ndio Faida ya kuwa na Serikali ya kishikaji, Tanzania eeeeeeeeehhhhh tanzaniaaaaaaaaaaaaaa
 
Kiwete+Mkulo=Kasungura kadogo=Uchumi unapaa. Aaghh...................... Hawa vilaza wanakera yani ningekuwa na mashine hawa......................
 
Back
Top Bottom