Kudakwashe
Member
- Nov 23, 2014
- 53
- 25
Mtoa mada acha wivu wa kike.
Kwa mikataba inayochongwa na TPDC kwasasa ya kuanzia 60-70% ni mali ya Tanzania plus corporate taxes yeyote atakaye mpa kitalu ataonekana fisadi hata Muhongo akitolewa.Mengi hana hamu na Muhongo! Kwani baada ya Kumpatia Mabilioni Sendeka na wenzake alijua kila kitu kitamalizikia kule kule Dodoma,yaani mpaka sasa amepoteza mapesa kibao kwa Kamati za Ufundi na wajanja wa Town wanachuna kwa kwenda mbele, Mengi hapati Usingizi akisikia jina la Muhongo kaapa atauza hadi tambala la deki ahakikishe Muhongo anang'oka.
Imeniingia akilini Huyu Mengi si bure amekuwa km mwanamke mjazito kila siku analalama yy tu mara ndimu,mara udongo,mara hichi pumbavu huyu mzee ila some time yes some time no
Hadi sasa sijaona kuhusika kwa Mengi kwenye pesa za Escrow zaidi ya watu kuja na shutuma za uzushi.Ebu jiulize iweje Mtu ambaye si Msaafi amunyooshe mwingine vidole? Huyo Mengi yeye si msaafi kabsa tana ana Madhambi kibao iweje awe kinara wa kuwang'oa wengine? Mengi kala Mabilioni ya Rostam na amemsaidia kuuza vyake kisha kutimuka pasipo kulipa kodi, yaani kwa Lugha rahisi kodi alimpatia Mengi badala ya serikali, Huyo babu Mengi kama lilivyo jina lake ana Madhambi Mengi hakuna mfano.
Nchi Hii hakuna asiye na doa wengi wanamwogopa Mengi kwa kuwa wanajua kuwa na wao wamefanya madili wataumbuliwa,Mengi ana mtandao mkubwa unaomwabudu na amezoea kuwang'oa mawaziri kiwepesi japo safari hii kakumbana na kisiki na watu wengi wameamka wapo makini hawataki kuburuzwa ndiyo maana Mengi kapewa vipande vyake, Lakini ingekuwa kama zamani watu wangemhukumu Muhongo pasipo kujua upande wa Mengi.Mengi ni born town.. Hakuna lisisiem lolote linalomweza Mzee Mengi, mabwana zenu akina Rostam na Manji na msululu wa wahindi wote wanaoisaidia sisiem wameshanyoosha mikono. Sisiem mna serikali na dola lakini Born town anawageuza anavyotaka na hamumfanyi chochote. Mnabaki kurojoka tu mara katapeli na kufilisi NBC, mara anakwepa kodi, sasa si mumfilisi kama mnamweza?? Mnasubiria nini?? minyoo anasema eti Rostam kauza shares voda then kamkatia percent Mengi ili asilipe kodi, hii ina maana Mengi ni zaidi ya TRA, Mawaziri husika na Rais mwenyewe.. Kwanini Rostam hakwenda kumwonga Mwigulu au profeseri busha?? Saying that it proves that Mengi is Tanzania ndio maana masisiem kila ligi mnayocheza na Mengi anawapiga chini
Unataka ufisadi wa aina gani au kama ule wa slaa wa kuiba wake za watu.
Mengi kama lilivyo jina lake ana Madhambi Mengi, huyo mzee anazeeka vibaya sana, yeye kaamua kamkomalia Mhongo wakati yeye mwenyewe ni Mtu Hatari ! Sijui alitaka watu wakae kiimya kama Zamani, watanzania wa sasa wameamka hawataki Unafiki, Mengi hana sifa za kuwanyoosha wengine vidole kwani yeye pia ni Mwizi mkubwa.
Hadi sasa sijaona kuhusika kwa Mengi kwenye pesa za Escrow zaidi ya watu kuja na shutuma za uzushi.
Huwezi kumlinganisha Mengi na Muhongo, Mengi ni mfanyabiashara wa siku nyingi na ataendelea kujulikana kwa muda mrefu, Muhongo yeye ni mtumishi wa umma na anashikilia ofisi ya umma kwa muda, muda si mrefu atakuwa mitaani kama mwenzake Werema.
kama Mengi ni "mwizi mkubwa" basi uongozi wote wa nchi ni wa kishetani!
ni shetani tu anayefurahia kuwepo kwa "mwizi mkubwa"
unachofanya ni kumvua boksaa mfalme kuacha machungwa (kama bado yapo) yakining'inia!
Mfalme hana balls za kumkamata "mwizi mkubwa"?
Mengi ni janga katika Taifa. Natamani Rais ajaye awe mkali sana kwa huyu jamaa. Ukiona mtu anabaka mjukuu wake ni dalili tosha kichwani zishatuka....shame on you Mengi
Mkono ndiye aliibua sakata la escrow baada ya kufutwa kazi na Tanesco akaenda kuungana na Mengi ambaye alinyimwa Vitalu vya Gesi, hivyo kama Mkono na Mengi wangefanikiwa juu ya Michongo yao leo hii kusingekuwepo na escrow, hao wazee ni Wanafiki sana waliibua issue baada ya kukosa Dili lakini wangepata wangekaa kimya. Mengi ni mfanyabiashara wa siku nyingi Lakini si biashara halali kwani kuna magumashi kibao si mkweli kwenye jambo lolote ni mjanja Mjanja huku akiwa mwepesi wa kudeka pindi akiona watu wanata kumuumbua.
Nchi Hii hakuna asiye na doa wengi wanamwogopa Mengi kwa kuwa wanajua kuwa na wao wamefanya madili wataumbuliwa,Mengi ana mtandao mkubwa unaomwabudu na amezoea kuwang'oa mawaziri kiwepesi japo safari hii kakumbana na kisiki na watu wengi wameamka wapo makini hawataki kuburuzwa ndiyo maana Mengi kapewa vipande vyake, Lakini ingekuwa kama zamani watu wangemhukumu Muhongo pasipo kujua upande wa Mengi.
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.
c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.
l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.
m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.
n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Mengi ana Madhambi mengi kama lilivyo jina lake, kwanza Wafanyakazi wake Anawaibia sana kwa kuwalipa mishahara Mibovu, Rostam Azizi aliuza hiza zake za Voda kwa dola million 300 akaondoka Nchini pasipo kulipa kodi baada ya kumugawia mengi Mabilioni kwa ajili yakumaliza Ugonvi wao na pia Mengi kamsaida kukwepa kodi.
Mbona unajikanganya mwenyewe?? Kama wote wana doa Mengi anatoa wapi ujasiri wa kuwaumbua waziwazi na kuwapiga chini??