Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Mkuu naona hapo pa Muhongo ndio hasa ambapo umepalenga, huko kote kwingine ni hadithi tu. Hongera kwa kumtetea bosi wako Muhongo. Mkuu uelewe kitumbua kimeisha ingia mchanga, sisi watanazania sio wajinga wala wapumbavu, tunajua mbichi na mbivu, kuendelea kutetea mafisadi wenu mnajivua nguo wenyewe. Uzi wako mzima unatetea mafisadi papa, mkuu shame on you.
 
Huyu huyu ndiye aliyemshambulia sana Ben Mkapa kupitia magazeti yake akidai kwamba eti alimfanyia roho mbaya wakati akiwa madarakani. Msisahau pia aliwahi kulianzisha na Dk Fenella Mkangara, lakini huyu mama msomi akampuuza tu. Pia hupenda kujitambulisha kama rafiki mkubwa wa JK, halafu anamshambulia kupitia magazeti mengine.
 
mmmmh kumbe ndio maana yuko mweupe mweupe hivi
Dada yangu hebu ingia link ya BMT hajajaziwa chochote hata umri wa kuzaliwa yaani huyu jamaa ni magumashiwa kutupwa
vijanwa wake wametupiwa vi-bundle wamsafishe
http://www.parliament.go.tz/index.php/members/mpcvs/1778/2010-2015
Member of Parliament CV


[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 3, align: left"]GENERAL[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Salutation[/TD]
[TD]Honourable[/TD]
[TD="width: 42%"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]First Name: [/TD]
[TD]Prof. Sospeter[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Middle Name:[/TD]
[TD]M.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Last Name:[/TD]
[TD]Muhongo[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 20%"]Member Type:[/TD]
[TD="width: 38%"]Nominated by the President[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Constituent:[/TD]
[TD]No consituency[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Political Party:[/TD]
[TD]CCM[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Location:[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Phone: [/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ext.: [/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Fax: [/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office E-mail: [/TD]
[TD]smuhongo@parliament.go.tz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Member Status: [/TD]
[TD]Current Member[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Date of Birth[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Huyu huyu ndiye aliyemshambulia sana Ben Mkapa kupitia magazeti yake akidai kwamba eti alimfanyia roho mbaya wakati akiwa madarakani. Msisahau pia aliwahi kulianzisha na Dk Fenella Mkangara, lakini huyu mama msomi akampuuza tu. Pia hupenda kujitambulisha kama rafiki mkubwa wa JK, halafu anamshambulia kupitia magazeti mengine.

Mengi ni born town.. Hakuna lisisiem lolote linalomweza Mzee Mengi, mabwana zenu akina Rostam na Manji na msululu wa wahindi wote wanaoisaidia sisiem wameshanyoosha mikono. Sisiem mna serikali na dola lakini Born town anawageuza anavyotaka na hamumfanyi chochote. Mnabaki kurojoka tu mara katapeli na kufilisi NBC, mara anakwepa kodi, sasa si mumfilisi kama mnamweza?? Mnasubiria nini?? minyoo anasema eti Rostam kauza shares voda then kamkatia percent Mengi ili asilipe kodi, hii ina maana Mengi ni zaidi ya TRA, Mawaziri husika na Rais mwenyewe.. Kwanini Rostam hakwenda kumwonga Mwigulu au profeseri busha?? Saying that it proves that Mengi is Tanzania ndio maana masisiem kila ligi mnayocheza na Mengi anawapiga chini
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: WCM
kweli jamaa hawa takataka ya watz kujifanya wanatumwa ujinga ipo siku wakiwekwa kati watatamani waolewe yaishe

Tatizo vijana wengi wa lumumba wamekaririshwa kwamba wanaikosoa serikali yao ya ccm na watendaji wake ni adui kwa taifa lao hvyo kupelekea kuzushiwa mambo yasiyo na ukweli.
 
Mengi ni Mnafki sana akipata kitu huwa kiimya na Laiti angepata Vitalu vya Gesi leo hii watanzania wasingekuwa wanamjua Muhongo, si umeona Rostam kauza hisa zako voda kwa dola million 300 akamugawia Mabilioni Mengi ili kumalizana Ugonvi wao na Mengi akamsaidia kuondoka na Hayo Mabilioni pasipo kulipa kodi kutokana na Uzoefu wake wa Ukwepaji kodi, tatizo Mengi kasahau kuwa watanzania wa sasa si wale wa zamani ambao waliokariri kuwa Mengi ni MUNGU hawezi kuwa na doa wala Dhambi.

Hivi Rostam si ndie alikuwa mbunge igunga kwa tiketi ya CCM,unataka kuniambia Mengi ana mjua Rostam kuliko CCM waliompa dhamana ya kugombea ubunge Igunga,ikumbukwe sera ya kujivua gamba ilitokana na kashfa zilizo anzia kwa Rostam,nahisi hata Kufungiwa kwa gazeti kuna uhusiano wa habari iliyo anika uchafu wa Rostam iliyokuwa na kichwa cha habari ROSTAM ANACHEZA KAMA PELE MIPANGO KAMA KANISA KATOLIKI.
 
SERGIO Viongozi wenyewe unaowasema ndio hawa kina Muhongo au? Kama ndio hao basi hao ni wachafu tu. Unamuonea bure mzee Mengi

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Last edited by a moderator:
The way people are arguing here is very strange. Prof Muhongo is guilty, and this has no doubt. The conflict between Muhongo and Mengi is another issue. Inawezekana kweli Mengi ana self intrest hapa lakini hii haisafishi makosa aliyotenda Prof Muhongo. Hebu shirikisheni akili kidogo nyie Watanzania
 
Azimio lipi? Hilo Azimio si ni la Shinikizo la Mengi baada ya kutembeza mkwanja kupitia kwa Sendeka.
We hukupata huo mkwanja. Acheni kumbwela mbwela watu wamekula hela unakuja kutetea humu jamii forum ufala huo
Yaani watu bwana hata huu wizi wa wazi bado mnatetea hivi mmelishwa nini watanzania jamaniii
 
Kweli njaa nikitu kibaya sana yaani unaweza kununuliwa hata kwa sahani ya chips kavu?Ninani ndani ya nchi hii asiejua uzalendo wa mzee Mengi?nani anawajali nakuwathamini watoto wamaskini wa nchi hii kama Mzee Mengi? Mungu Akulinde na Kukubariki Kwakila Unachokifanya Mzee Mengi Kwani Jasho Lako Linakomboa Watoto Wengi Maskini Wa Taifa hili..! Mzee Mengi Wasamehe Hawa Vijana Waliokubali Kutumika Bila Kujua Wajibu Wao Wakulinda Rasilimari Za Taifa Ndio Maana Wako Kwenye Mitandao Wanachafua Watu Wakati Baba Zao Wameshikiliwa Kwenye Ofisi Zakata Na Vituo Vya Polisi Kwakukosa Michango Ya Ujenzi Maabara..!
 
mhuhongo+saada mkuya x mcc nimesha saini na mimi ndiye waziri-tumbili=kafulila tumbili ndiye mkweli
 
Back
Top Bottom