Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Huyu ndiye fisadi hatari zaidi

Hata kama wabifu kama Muhongo kaiba ni kaiba tu bifu halibadili wizi!

Tatizo ni kwamba Huyo Mengi anayemkomalia Muhongo naye ni Mwizi number one na hajawahi kutubu, sasa iweje Mwizi mkubwa akomalie wengine huku yeye hajitizami kwanza kabla ya kuendeshea kuwakomalia.
 
Tatizo ni kwamba Huyo Mengi anayemkomalia Muhongo naye ni Mwizi number one na hajawahi kutubu, sasa iweje Mwizi mkubwa akomalie wengine huku yeye hajitizami kwanza kabla ya kuendeshea kuwakomalia.

Hivi wewe upumbavu wako ni kiasi gani?? Mengi ni mfanyabiashara sio mtumishi wa uma. Mengi kaiba nini ambacho mnashindwa kumshtaki?
 
Nyamubi Masatu kama sijakosea, alimaliza la 7 Kwangwa s/m baada ya kufeli shule mojawapo pale Musoma mjini. Alifaulu baadaye kidato cha kwanza pale Mara sec. Sasa ni Prof. Miaka hiyo kurudia darasa 7 hata mara 5 lilikuwa jambo la kawaida sana.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA KUTETEA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:
Kwa miaka mingi kumukuwepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayoyajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali na baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo kwani siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi.
Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Historia inaonyesha amewahi kuanzisha ugomvi na watu wafuatao kwa sababu anazozijua yeye.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

m) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani.

n) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba.
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi na familia yake. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito sasa ni wakati ambao serikali ina bidi ichekue hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

WEWE acha kutulisha pumba!! Mengi ni mtanzania halisi anaipenda nchi yake wote uliowataja ni mafisadi wakubwa nani asiyejua wakina Rostam Aziz, Masha, Muhongo n.k. ni mafisadi wakubwa hapa nchini??
 
Ujasiri anaupata kwa wale wa Mtandao wake ambao kwa sasa hawana nguvu baada ya watanzania wengi kuzinduka ndiyo maana kumung'oa Muhongo imekuwa shughuri pevu, huko nyuma alizoea kuwang'oa mawaziri kwa njia nyepesi tu.

Najua id ya funza na minyoo ni ya mtu mmoja.. Kama unajidanganya muhongo anahitajika na watanzania wewe ni mpumbavu nambari one. Ni rais dhaifu anamlinda sababu na yeye ni mhusika mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mengi ni mwizi,anatumia mgongo wa uzawa kuwaibia watanzania,sasa tumejua janja yake.

Mwaka 1994 aliituhumu serikali kuwanyima viwanja wazawa katikati ya mji,yaani posta na kariakoo kwamba wanapewa wageni wazawa hawapewi,rais mwinyi akaamuru mengi apewe kiwanja,akapewa kiwanja karibu na ilipo hotel ya southern sun au international house[kwa wasiojua maeneo hayo,yako karibu na hospitali ya kansa ya ocean road,chuo cha utalii cha taifa,makumbusho ya taifa.]

Baada ya kupewa,muda mfupi akaliuza eneo hilo kwa wahindi.ambao awali alikua anailaum serikali kuwapendelea na kuwanyima wazawa,alipopewa tu akawauzia hao hao.

Leo anataka vitalu,akipewa kwa kua anajua hawezi kuviendeleza atawauzia wazungu hao hao anaowapinga kila siku.

Unajiuliza kama ana akili sawasawa,alafu anajiita Mengi PhD[pumbavu hana dawa],huu udokta wa kupewa baada ya kushkwa shkwa inye hatari sana.
Mengi ana PhD ya Udalali na Ulalamishi anapiga kila kilichopo mbele, hana aibu hudeka huku akiendelea kupiga. Mfano yale matamasha na zile pati za kula chakula na Vilema ( Walemavu) watu hufikiri Mengi ni Mtu mwema na anawapenda sana Vilema, lakini kumbe Ule ni Mladi wa kuomba pesa Ulaya na kuomba Misamaha ya kodi kupitia Video ambazo huwa amezirekodi wakati anakula nao chakula, Mengi hana cha bure kila kilichopo mbele yake ni Dili, Vitalu vya Gesi tu ndiyo vimemfanya hapati Usingizi Lakini hata leo ukisikia kapata Vitalu atakaa kimya utashangaa.
 
Najua id ya funza na minyoo ni ya mtu mmoja.. Kama unajidanganya muhongo anahitajika na watanzania wewe ni mpumbavu nambari one. Ni rais dhaifu anamlinda sababu na yeye ni mhusika mkuu

Wewe ndiye mpumbavu wa karne! Watanzania wapi? Kwani watanzania wa sasa ni wale wa zamani? Kama wangekuwa wajinga kama wewe kusingekuwa na watu wanaopingana na mbinu za Mengi, woote wangemwamini Mengi pasipo kuhoji kasoro zake kama wewe, acha Kuwalazimisha watanzania waamini fikra zako binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Mengi ana PhD ya Udalali na Ulalamishi anapiga kila kilichopo mbele, hana aibu hudeka huku akiendelea kupiga. Mfano yale matamasha na zile pati za kula chakula na Vilema ( Walemavu) watu hufikiri Mengi ni Mtu mwema na anawapenda sana Vilema, lakini kumbe Ule ni Mladi wa kuomba pesa Ulaya na kuomba Misamaha ya kodi kupitia Video ambazo huwa amezirekodi wakati anakula nao chakula, Mengi hana cha bure kila kilichopo mbele yake ni Dili, Vitalu vya Gesi tu ndiyo vimemfanya hapati Usingizi Lakini hata leo ukisikia kapata Vitalu atakaa kimya utashangaa.

Mengi ni mwizi mkubwa na dalali mkubwa wa karne katika nchi hii.....Mengi hana biashara yenye kumpa utajiri kiasi hicho, zaidi ya makampuni yake ya Ipp ambayo yanaendeshwa kwa hasara, ni nini chanzo kingine cha mapato yake.

Amekuwa dalali katika madini na sasa anataka kuwa dalali katika gesi thanks Muhongo kamgundua na kumkatalia katika hilo
 
Najua id ya funza na minyoo ni ya mtu mmoja.. Kama unajidanganya muhongo anahitajika na watanzania wewe ni mpumbavu nambari one. Ni rais dhaifu anamlinda sababu na yeye ni mhusika mkuu

Wananchi wa sasa wameamka wanajua kubalance pande zote, hawakariri kama zamani ambavyo wengi walikariri Mengi ni MUNGU kila analosema limetoka Mbinguni ndiyo maana alikuwa akiwang'oa mawaziri kirahisi sana, Sasa watu wameshajua kuwa masilahi yake binafsi hutumia huruma za wananchi kupambana na wabaya wake.
 
Last edited by a moderator:
Kwani U Dr. Kikwete kausomea wapi, Mzindakaya naye ni Dr. aliupata wapi?, Aman Abeid Karume naye aliupata wapi U Dr.?, acha ushamba!!
 
Mengi ni mwizi mkubwa na dalali mkubwa wa karne katika nchi hii.....Mengi hana biashara yenye kumpa utajiri kiasi hicho, zaidi ya makampuni yake ya Ipp ambayo yanaendeshwa kwa hasara, ni nini chanzo kingine cha mapato yake.

Amekuwa dalali katika madini na sasa anataka kuwa dalali katika gesi thanks Muhongo kamgundua na kumkatalia katika hilo

Anajuta kuanzisha Ligi na Muhongo kwani mpaka sasa kapoteza Mabilioni na Mhongo bado yupo Ofisini, yupo busy kila dk anabuni mbinu za kufanya ili Mhongo ang'oke, wajanja wa Town sasa wanajilia pesa toka kwa Mengi kwa kisingizio cha kumsaidia kumung'oa Mhongo,kwa kweli tokea Mengi aanze hizo fitna zake za kuwang'oa mawaziri hajawahi kutana na Mziki kama wa Muhongo, hata wana JF nao Safari hii wamegundua kuwa Mengi naye ni Mwizi hafao kumkosoa mtu.
 
Mimi nawashangaa ninyi mnao mjadili mtoa Mada, huyo hawezi jibu chochote kwa kuwa hiyo taarifa amepewa tu aiweke hapa jamvini hana analolijua.

Mada hii imekopiwa toka kwenye hotuba ya fisadi Rostam Aziz aliyokuwa anamjibu Bw. Region and Mengi, kama kuna mtu anaweza kui upload hutuba hiyo anipatie namba yake nimtumie kwa whatsaap.

Nasisitiza mtoa mada hana lolote na inaelekea uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo mno kwa sababu ame copy na ku pest bila kuacha hata neno moja!
 
Anajuta kuanzisha Ligi na Muhongo kwani mpaka sasa kapoteza Mabilioni na Mhongo bado yupo Ofisini, yupo busy kila dk anabuni mbinu za kufanya ili Mhongo ang'oke, wajanja wa Town sasa wanajilia pesa toka kwa Mengi kwa kisingizio cha kumsaidia kumung'oa Mhongo,kwa kweli tokea Mengi aanze hizo fitna zake za kuwang'oa mawaziri hajawahi kutana na Mziki kama wa Muhongo, hata wana JF nao Safari hii wamegundua kuwa Mengi naye ni Mwizi hafao kumkosoa mtu.

Nakubaliana nawe,mengi kwa mhongo amegonga mwamba. Alitegemea muhongo atang'oka kijinga kama alivyokua anawafitini mawaziri wengine.

Hata kama muhongo atakuja kutoka ila mengi hatamsahau. Nakuhakikishia 3-5 years to come hakuna atakaekua anaangalia tv zake,azam anakuja kwa kasi na wengine,ataanzisha vita na hao wengine kwamba wanamhujumu.

Mengi hafai,kila jambo jema nchi hii hataki,akataka tusihamie digitali kwa faida yake mwenyewe na u phd wake.
 
Imeniingia akilini Huyu Mengi si bure amekuwa km mwanamke mjazito kila siku analalama yy tu mara ndimu,mara udongo,mara hichi pumbavu huyu mzee ila some time yes some time no

watz wengi ni wajiNgA sana meNGI AnawapigANia lAkini hamlIoni hilo.
 
watz wengi ni wajiNgA sana meNGI AnawapigANia lAkini hamlIoni hilo.

Acha unafiki,mengi hampiganii mtu,anajipigania mwenyewe.

Mengi angekua na roho nzuri asingekua anadai tax deductions/refund kwa ule msosi anaowalisha walemavu na wazee.

Angekua amewapa mikataba ya kudumu wafanyakazi wake,anawalipa ujira mdogo bila mikataba ya kazi. Wewe mtu anagombana na kina joti unafikiri zinamtosha?

Waswahili husema ukikaa karibu na waridi utanukia vizuri,watu wanaofanya kazi kwa mengi choka mbaya wakat yeye ni bilionea,hakuna uhusiano hapo,fuatilia wanaofanya kazi google,microsoft nk wanavyoishi maisha mazuri maana wanamfanyia kazi tajiri,kwa mengi ni kinyume.
 
acha uongo mdogo wangu anafanya kazi ipp na analipwa vizuri sana.wafanyakazi wa ipp waNA maiSha mazuri sanA.
I
 
Mengi ni tapeli mkubwa.. ametuzulumu ardhi handeni huko. We o.. shamba tunalimiliki kwa neema za mungu tukakuta dhahabu pale. Kwenda kuomba leseni pamoja na kwamba sisi ndo tuliwahi kuomba leseni ile lakini leseni ile akapewa Mengi. Na ni miaka zaidi ya sita sasa leseni anayona hatki fanya chochote alikuja akafanya utafiti bila fidia pamoja na kumfata na kujaribu kuongea nae. Alichoonesha ni kwamba nyie maskini nahamnifanyi kitu. Ameshajaribu kila mahali kututapeli the land lakini anakwama. So ni fisadi mkubwa na tapeli pia. Anyongwe. I have him to ma born marrows..
 
Nashauri urudie tena andiko lako na sources ulizoweka.

Binafsi sion mchango wa moja kwa moja wa hao uliowataja kwa Watanzania dhidi ya Mengi.

IPP ndo media pekee ambayo watanzania tunaiamini ndani na hata nje ya nchi.

Long live Managing director of IPP media , Dkt Reginald Mengi.

Together we stand separate we fall.
 
Back
Top Bottom