Huyu ndiye Cedric Kaze, Kocha mpya wa Yanga anayerudisha heshima Yanga

Nimemtazama Kocha Cedric Kaze, nimeitazama tena Yanga ikiwa inacheza kisha nikamtazama tena yeye, nikasafiri mbali sana kupitia makabrasha yake Bwana Kaze

Kaze huyu ana leseni A ya CAF na Leseni A ya Chama cha soka Ujerumani (DFB) ndio leseni ngumu zaidi ya ukocha kupatikana duniani, kifupi jina lake lipo kwenye daftari moja na wakina Jurgen Klopp

Kaze huyu ndie alikuwa Mchambuzi wa viwango kwa timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21, kilichotwaa kombe la dunia 2009, weka nukta hapo! Yaani Ujerumani walimpa majukumu nyeti sana

Kaze huyu alipewa kazi maalum na taifa la Ujerumani kufuatilia viwango vya viungo wao ingali wadogo, Toni Kroos, Sami Khedira na Mesuit Ozil, aliifanya kazi na akaikamilisha kazi

Kwanini namtaja sana Kaze leo?? Naachaje kumtaa kama mnamwona Kibwana Shomari mchezaji kinda amebadilika kabisa anachukua mali eneo lake, anatunza mali kwa kujiamini na anaitoa kwa kujiamini

Naachaje kumtaja Kaze kama ndie amempeleka Fei Toto mgahawani kisha achague Menu anayotaka, alichofanya yeye ni kumlipia bill yake, akamuweka sawa Mukoko, akawaambia Yanga chezeni kwa kumtazama huyu mtoto, nadhani mnamwona

Naachaje kumtaja Kaze kama sio yeye aliemuibua Saido Ntabazonkiza ingali kinda, akacheza michezo ya Rolling stone pale Arusha, akaenda Ulaya na karudi tena kwenye mikono yake, tukionacho kwake ni matokeo ya akili ya Kaze, aliesema mpeni mpira aamue yeye
Natamani sana nimalize kwa kusema nyuma ya ubora wa Yanga Afrika ni huyu Kaze, natamani tumsake yule Mswahili aliesema 'Ngoja ngoja huumiza matumbo' tumuombe atengue kauli
Goli tatu, alama tatu na round ya kwanza imeisha .
Kwa nini asipewe uraia wa tanzania tuanze hulka ya kudakuwa watu mashuhuri na kuwa fanya watanzania nadhani akitumika vyema akapewa na yanga b na akapewa jukumu la kusaka vipaji huenda tukafika mbali sana [[ wana simba mfu sasa hivi wataharibu upepo hapa]]
 
Mbona kuna watu wamenuna sana hapa......Kaze + Morrisson anawaumiza kichwa huko.......mpaka mseme ukweli umri wa Onyango na dhulma ya ubingwa mliochukua
 
Mkichukua ubingwa mtasema yeye ndiye aliye shauri matumizi ya VAR vyura ngoma bado mbichi punguzeni kelele
 
Hizi thread zenu tutakuja kuzifufua mwezi march tu hapo,Mungu akipenda inshallah!
ukweli usemwe,mimi mshabiki wa simba sichelewi kusingiziwa ni utopo kafufue nyuzi zangu utaelewa niko upande gani...KISHINGO KUNA MAWILI ABADILI MFUMO AU AONDOKE...KIUNGO KINAKUWA EXPOSED SANA KISENGESENGE,UTOPOLO TUMEWAZIDI UBORA WA WACHEZAJI SANA TU,WAMETUZIDI UBORA WA KOCHA NA SPIRIT YA TEAM,YAANI TUNACHEZA KAMA KONOKONO NA TEJA HALIJUI CHA KUFANYA MFUMO WAKE WA 4-2-3-1 UKIFELI
 
Hayo ya kufufua nyuzi nimeandika masikhara tu...japo najua soon or later wataangukia pua na nyuzi humu zitakua za kulaumu TFF ambazo kwa sasa zimepungua.

Lakini wana Simba tunahitaji uvumilivu kwa sasa...ni kweli timu ipo down na hatujui tatizo...inaweza kuwa ni wachezaji au ni kocha.
Lakini suala la kumpangia kocha mfumo wa kucheza,tunavuka sana mipaka sababu yule kasomea...na kafanya kazi ana experience kuliko sisi tunaotaka kumfundisha achezeshe mfumo gani...ingekua ni vema labda tungeng'ang'ania Uchebe arudi as mfumo wake tuliuelewa...na pia binafsi naona ni kocha bora kuliko Sven.
 
Tetesi zilizopo ni kwamba nusu ya wachezaji wa simba ni wagonjwa wanafosiwa tu kucheza na ukweli kufichwa ila wengi wameokota corona Nigeria.C.E.O wa zamani yupo hoi kitandani.Ni wakati mgumu kwa simba
 
Hahahaha utopolo sasa mmeona tunavurugana kuhusu kishingo mnapandisha CD siyo,kwendeni hukooo
 
kocha huyu anaujua mpira wa afrika kwani mpira wa afrika na ulaya ni tofauti sana [ ulaya wanatumia akili zaidi na brain intellegence wakati afrika tunatumia mabavu akili ndogo zaidi na uchawi
 
kocha huyu anaujua mpira wa afrika kwani mpira wa afrika na ulaya ni tofauti sana [ ulaya wanatumia akili zaidi na brain intellegence wakati afrika tunatumia mabavu akili ndogo zaidi na uchawi
Sina maama ya kukukejeli lakini bila kulepepesa macho hii ni comment ya kipuuzi mno
 
Tetesi zilizopo ni kwamba nusu ya wachezaji wa simba ni wagonjwa wanafosiwa tu kucheza na ukweli kufichwa ila wengi wameokota corona Nigeria.C.E.O wa zamani yupo hoi kitandani.Ni wakati mgumu kwa simba
Sawa Dada kavae kjora chako. Ukacheze singeli
 
Kishingo ni mweupe,wakati anakuja alikuta bado upepo wa Uchebe unavuma ndani ya timu.
Upepo wa Uchebe umekwisha sasa anaonekana madhaifu yake namna yalivyo.
Kuku kishingo achague moja kati ya haya mambo mawili"aondoke au abaki lakini bundi aamke"
Hil jina la kuku kishingo kwakwel linachekesha sana.sio fare wazee
 
Back
Top Bottom