Kocha Cedric Kaze aitwa kuongeza nguvu Taifa Stars, Yanga yampa baraka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,453
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars, Adel Mrouche amepewa nafasi ya kuchagua wataalamu 4 atakaoambatana nao kwenye timu ya taifa kama sehemu ya benchi lake la ufundi, Kocha huyo amependekeza jina la kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze kuwa chaguo lake la kwanza.

Ikumbukwe Cedric Kaze alifundishwa na kocha Adel Mrouche. Mrouche ni mkufunzi wa shirikisho la soka Ulaya UEFA kwenye kozi ya UEFA pro license.

Tayari Klabu ya Yanga imeshapokea ombi hilo kutoka TFF, kinachosubiriwa kwa sasa ni maamuzi ya muhusika. Klabu imempa baraka zote Cedric Kaze iwapo ataamua kujiunga na timu ya Taifa.

Chanzo: Kitenge
 
Mwalimu Kaze anaongoza duniani kwa kufundisha kukaba , kulinda na kuzuia kufungwa. Ukiifunga Yanga goli moja tu Kaze halali wiki nzima anastudy umeifungaje Yanga mwanya uko wapi, iliwezekanaje basi goli moja tu litamuuma mno! Ukiifunga Yanga goli mbili anaweza kupata homa!

Kifupi Cedric Kaze hataki kufungwa na anajua kulinda asifungwe. Bado Kuna shida Yanga juu ya kucheza krosi , mabeki kuruka na washambuliaji hapa ndo bado Kaze hajafanikiwa.

Wachezaji wa Yanga wameshamuelewa na Sasa kuifunga Yanga kwa mpira wa move ni ngumu sana ni kubahatisha tu.

Kaze ni mtu sahihi. Atasaidia sana Taifa Stars kujifunza kuzuia ila tu iwapo hao wageni Toka Simba sijui Geita kama watafundishika maana Yanga wachezaji Wana morali , wana afya , Wana pumzi na wanakaba kwa pamoja tena kwa spidi muda wote kama ugomvi Sasa sijui huko Kolokoloni na Manungu wanafundishaje wachezaji kuzuia kufungwa!

Yanga hoyeeee!
Kaze hoyeee!
Feitoto hoyeee!
 
Hii timu inaenda kushangiliwa na Yanga tu, mashabiki wa Simba watakaa pembeni.

Ina make sense sasa kwa nini mchezaji kama Kapombe ameachwa, kwa nini Feisal ameitwa, kwa nini makipa wawili wa Simba wameitwa (mtego wa lawama unawasubiria).

Siasa inaendesha mpira, bado hatuna nia ya kweli kukuza mpira wetu.
 
Kwahiyo Kapombe angeitwa ndio mpira wetu ungekua? Kwani kashaitwa mara ngapi wanaishia kubamizwa migoli mingi mingi? Nyinyi kaeni pembeni tutaenda kuishangilia timu ya taifa peke yetu eboo
 
Mwalimu Kaze anaongoza duniani kwa kufundisha kukaba , kulinda na kuzuia kufungwa. Ukiifunga Yanga goli moja tu Kaze halali wiki nzima anastudy umeifungaje Yanga mwanya uko wapi, iliwezekanaje basi goli moja tu litamuuma mno! Ukiifunga Yanga goli mbili anaweza kupata homa!

Kifupi Cedric Kaze hataki kufungwa na anajua kulinda asifungwe. Bado Kuna shida Yanga juu ya kucheza krosi , mabeki kuruka na washambuliaji hapa ndo bado Kaze hajafanikiwa.

Wachezaji wa Yanga wameshamuelewa na Sasa kuifunga Yanga kwa mpira wa move ni ngumu sana ni kubahatisha tu.

Kaze ni mtu sahihi. Atasaidia sana Taifa Stars kujifunza kuzuia ila tu iwapo hao wageni Toka Simba sijui Geita kama watafundishika. Yanga oyeeee!

Akawaulize waarabu wanawafungaje au Geita Juzi
 
Kwahiyo Kapombe angeitwa ndio mpira wetu ungekua? Kwani kashaitwa mara ngapi wanaishia kubamizwa migoli mingi mingi? Nyinyi kaeni pembeni tutaenda kuishangilia timu ya taifa peke yetu eboo
Mbona Manula ameitwa? Unaacha makipa ambao wana game time kwenye timu zao unaenda kumuita Metacha ambaye hata mechi na Mbao huwa hapangwi?
 
Utopolo Hawana Makocha...!

Nabi imebakia kusifiwa Na Wachambuzi Wa Mchongo...!

Historia Yake inaeleweka alikotimuliwa El merrekh baada Ya Kupokea kipigo kutoka kwa Mnyama CL Ya CAF..!

Kaze hamna Kitu pale.!
Mbona kama umevurugwa! Ulichokiandika, na mada iliyopo mezani; ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom