Huyu mgeni wangu mbona kama simsomi?

Huyu mgeni wangu mbona kama simsomi?

Kuna jamaa yangu katoka bush kuja kufuatilia masuala yao ya mirathi hapa mjini,sasa kwa sababu ni mtu wa kijijini na tunafahamiana nikamuambia hakuna haja ya kufikia lodge hapa kwangu kuna chumba cha wageni aje tu ili apunguze gharama.
Jamaa kafika tumepiga story za hapa na pale tukaagana kila mmoja akaingia chumbani kwake kulala.sasa chumba nilichomuandalia ndiko mimi huwa napatumia kunyoosha nguo zangu,nikakumbuka umeme unasumbua nikisema ninyooshe nguo asubuhi naweza nikaamka nikakuta umeme umekatika tayari.so ile naingia chumbani kwake nikamkuta jamaa kavua nguo zote afu kalala kifudifudi,nikatoka kwanza chumbani nikiwa namuwaza ,jamaa inakuaje analala hivyo,kashindwa kulala hata na boxer kweli?
Nimeshindwa kumsoma
Siyo wote wenye boxer mnunulie tena mbili
 
Acha viungo vipumue, mbona mwamba amejiamini kulala hivyo? Inamaana ndio mazoea yake ingawa umekosa ustaarabu ilikupasa ugonge hodi japo unayo mamlaka kwenye nyumba yako, pia kumsaidia mtu isiwe sababu ya kumtangazia madhaifu yake,, kitu kinachofanya usimuelewe ni nini? Hujui uchi upoje?
 
Dar sasa hivi hamna joto mkuu
Hilp joto la dar unaloona ni dogo linawrza kuwa kubwa kwa mimi ninayetokea mafinga, pia kulala uchi si kosa kisheria, kikanuni, kiimani, wala kimaadili, wewe tu ulitaka kumu undermine mgeni wako ili ajue kwamba wewe ni tajiri, chumba anacholala yeye kwako ni kisehemu tu cha kupigia pasi,, na hizo tabia mnazo sana watu mliotokea kwenye ufukara uliopotiliza, huwa mkifika mjini na kufanikiwa kupata kijinyumba cha room 2 basi ndugu zenu waliobaki kijijini huwa mnawaona kama takataka,pmbv kabisa
 
Kuna jamaa yangu katoka bush kuja kufuatilia masuala yao ya mirathi hapa mjini,sasa kwa sababu ni mtu wa kijijini na tunafahamiana nikamuambia hakuna haja ya kufikia lodge hapa kwangu kuna chumba cha wageni aje tu ili apunguze gharama.
Jamaa kafika tumepiga story za hapa na pale tukaagana kila mmoja akaingia chumbani kwake kulala.sasa chumba nilichomuandalia ndiko mimi huwa napatumia kunyoosha nguo zangu,nikakumbuka umeme unasumbua nikisema ninyooshe nguo asubuhi naweza nikaamka nikakuta umeme umekatika tayari.so ile naingia chumbani kwake nikamkuta jamaa kavua nguo zote afu kalala kifudifudi,nikatoka kwanza chumbani nikiwa namuwaza ,jamaa inakuaje analala hivyo,kashindwa kulala hata na boxer kweli?
Nimeshindwa kumsoma
Usalama wa taifa huyo ...tena ni level ya wolf kuwa makini
 
Ww ni mjinga na huna akili kwanza ni lini mtu kulala akiwa uchi kikawa kitu cha ajabu?au kama ww hutaki mtu alale uchi ndani ya nyumba yako ulimtaarifu kuhusu hilo ili alizongatie?

Pili kwanini uingie kwenye chumba ambacho unajua kuna mtu mzima bila kugonga hodi ili akuruhusu kuingia?
Nyinyi watu kama nyie ndo huwa mnafikia hatua ya kuwalala mabinti zenu kwa sababu ya ukosefu wa adabu.
 
Alikuja fundi home kufanya kazi za ujenzi ,katokea huko kusini ...Umeme ulikatika akiwa amelala basi katoka kwenye chumba chake na amelala kwenye sakafu hapo sebuleni...

Jamaa kafanya hivyo siku mbili kwa vile umeme ulikatika tena muda ule ule ...Ilikuwa mwaka jana nakumbuka..Kingine, jamaa akishaamka Asubuhi anafagia uwanja 🤣🤣mida hiyo mimi narudi masjid nakuta anafagia uwanja ...Tumekaa naye kama wiki 2 anafanya hivyo hivyo.

Kazi anapiga balaa we acha tu ,pia alitusaidia karibia nusu gharama ..
 
Kwa nini huyo jamaa analala bila kufunga mlango??
 
Back
Top Bottom