Huyu jamaa aliterend kwa design yake ya nguo

Huyu jamaa aliterend kwa design yake ya nguo

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,039
Reaction score
3,084
Screenshot_20260307-100819_1.jpg


Huyu Jamaa anaitwa Chibu. Chibu alikuwa tayari ameshinda tuzo nyingi sana za muziki, mpaka akawa mshindi wa tuzo za mwimbaji bora Afrika Mashariki. Sasa baada ya mafanikio hayo, akaamua kufanya sherehe kubwa ya kusherehekea ushindi wake.

‎Lakini Chibu hakuwa mtu wa kufanya mambo ya kawaida. Alipenda vitu vya tofauti kabisa. Kwa hiyo akatangaza kitu ambacho kilishtua watu wengi. Alisema kwenye sherehe yake atavaa vazi la kipekee sana, na yeyote atakayebuni dizaini bora zaidi ya nguo yake atajishindia milioni mia mbili.

‎Masharti yalikuwa rahisi: wabunifu wote walitakiwa kutuma mawazo yao ya mavazi ambayo Chibu angevaa siku ya sherehe.

‎Basi wabunifu wengi sana walituma mawazo yao. Kila mmoja akijaribu kuonyesha ubunifu wake. Lakini baada ya Chibu na timu yake kuyapitia yote, waligundua karibu mawazo yote yalikuwa yanafanana au yalikuwa ni mitindo ambayo tayari imewahi kuonekana.

‎Chibu alikuwa anataka kitu ambacho hakijawahi kutokea kabisa.

‎Siku moja wakakutana na jamaa mmoja aitwaye Damiano. Huyu alikuwa stylish na fashionista maarufu. Alikuwa hata amewahi kushinda mashindano ya fashion kule South Africa. Lakini wazo lake lilikuwa la ajabu sana.

‎Kwenye maombi yake aliandika:
‎"Nitakuvisha nguo ya chakula."

‎Chibu aliposoma hilo kwanza alicheka, halafu akabaki anashangaa. Akajiuliza, nguo ya chakula ina maana gani?

‎Damiano alipofika kwenye mahojiano akamweleza wazi:
‎“Nataka nikutengenezee nguo ya chapati.”

‎Chibu alishangaa sana, lakini akasema,
‎“Basi fanya maajabu yako.”

‎Sasa hapo ndipo shughuli ilipoanza. Damiano akaagiza sufuria kubwa sana yenye upana wa mita tatu ili kupikia chapati kubwa kuliko zote. Walitafuta sana wakakosa, mwisho wakaamua kutengeneza sufuria kwa bati zilizogongwa hadi ikawa kama sufuria kubwa.

‎Kisha wakaleta mifuko ishirini ya ngano. Wakaanza kukanda unga kwenye mabeseni makubwa. Baada ya hapo wakaipika chapati kubwa sana ile sufuria maalum.

‎Chapati ilipoiva, Damiano akaanza kazi ya ubunifu. Akaipima kwa vipimo vya mwili wa Chibu, akaanza kukata vipande na kuvishona kama nguo. Mwisho wake akamshonea suruali, shati, hata mkoba—vyote vikiwa vimetengenezwa kwa chapati.

‎Siku ya tukio ilipofika, watu hawakuamini macho yao.

‎Chibu alipotokea mitaani akielekea kwenye sherehe, watu walishangaa sana kumuona mtu amevaa nguo ya chapati. Wengine walimeza mate tu wakitamani hata waguse kidogo.

‎Alipofika kwenye tukio akaanza kupiga show. Watu wakamsogelea, wakampigia picha, wengine wakamgusa kwa mshangao.

‎Lakini kulikuwa na tatizo moja.

‎Kwa sababu ya joto na jasho, ile chapati ilianza kuroa polepole. Kadiri mashabiki walivyomgusa, wengine wakaanza kunyofua vipande vidogo na kuvila kwa utani.

‎Kidogo kidogo ile nguo ikaanza kupungua.

‎Baada ya muda Chibu alishtuka ghafla… akagundua karibu chapati yote imeondoka, baadhi imedondoka chini, baadhi watu wameila!

‎Alibaki amevaa boksa tu.

‎Bila hata kufikiria sana, Chibu akaanza kukimbia mbio kutoka pale kwenye tukio huku watu wakicheka na kupiga kelele.

‎Siku hiyo mitandao ya kijamii ililipuka. Video na picha zikawa zinaenea kila mahali. Kila mtu alikuwa anaizungumzia ile show ya ajabu ya nguo ya chapati.

‎Wengi wakawa Wanasema designer akamatwe
‎Designer yule Damiano Akaanza kutetemeka muda si punde akakimbia alijua labda watu watampiga kwasababu kamuabisha msanii
 
Back
Top Bottom