Huyu Jamaa Anakuja Lini?

Huyu Jamaa Anakuja Lini?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
702
Reaction score
1,648
Tangu tukiwa wadogo tukiwa tunapiga kelele, story imekuwa ni moja tu jamaa anakuja! Walimu walikuwa wanatupiga mkwara hadi tunashindwa kulala, tukihisi tukifumba tu macho, jamaa huyo hapa getini.

Lakini miaka imekata, 2030 hiyo hapo inachungulia, na maisha bado ni yaleyale, foleni za daladala, kupambana na kodi, na kupiga misele ya town.

Huyu jamaa hapigi simu, hatumi SMS, wala hatoweza kutoa taarifa lini anakuja.
Mbaya zaidi hata yeye alishasema hajui hiyo ratiba lini atakuja.
Ila kuja tu lazima aje, hata ikifika 2100, maana tumezaliwa tumekuta hii stori kwenye vitabu vya dini....

Atakuja lini? Jibu fupi na la wazi ni SIJUI, NA HAKUNA ANAYEJUA!
Vitabu vyake vimeeleza wazi, ishara za kuja kwake.
Hatari kubwa ni hii Maisha yanavyozidi kuwa ya kawaida, ndivyo watu wanavyozidi kusahau.

Ni kweli, babu alikufa akisubiri, baba naye anazeeka akisubiri, na sisi ndo kwanza tunapambana. Hii inafanya lile tishio la "atakuja kama mwizi lipoteze uzito. Watu washazoea mwizi asiyekuja, maana atokei.

2030, 2050, na hata 2100 huenda atakuwa amesharudi , hakuna anayejua.
Kwa binadamu, miaka 100 ni mingi sana ni maisha ya mtu mzima kabisa.
Lakini kule juu inasemekana siku moja ni kama miaka elfu moja, na miaka elfu moja ni kama siku moja. Hapo ndo hesabu zinapofeli.

Sisi tunapiga kalenda ya 2030, 2040...
Kule juu labda sekunde mbili tu ndo zimepita tangu jamaa aondoke...
Inasemekana baba yake akiyeketi naye mkono wa kuume ndiyo anajua jamaa anakuja lini, kwaiyo kama wewe ni Mkristo na unamuamini kaa ujiandaye, maana anakuja kuhukumu wenye dhambi.
 
Back
Top Bottom