TATIZO WANAWAKE TUKIPENDA ,TUMEPENDA ILA KWA SABABU SIO NATURE YETU 'KUTONGOZA' HILO NI JUKUMU LA WANAUME NA LIPO TANGIA ENZI,HUYO DADA KAKUPENDA ILA ANASUBIRI NATURE IENDE KAMA ILIVYOTAKIWA,KAMA UMEMPENDA 'MTONGOZE' LOL
Umeongea fact. Nimewahi kukumbana na kisa cha namna hii, nilikutana na dada mmoja wakati nimeenda kumtembelea rafiki yangu tukastorika weeeee hadi ilipofika mida ya kuondoka nikasepa zangu. Rafiki yangu akanipigia simu kunieleza huyu dada tulikuwa tunapiga nae stori anaomba nimpe namba yako (nimpe?) nikamruhusu mpe. Siku iliyofuata akanitumia ujumbe wa salamu , tukachart kidogo ikapita, ikawa kila siku asubuhi na jioni lazima anijulie hali na stories za hapa na pale kila mtu anashika lake.
Kutokana na uzuri wake na aina ya kazi anayofanya hata sikuwa na wazo kama angeweza hata kuwaza tu kuwa na mimi( kwa muonekano wangu nilivyo nilivyo) yy ni matawi mno ukilinganisha na mimi hali ya mtu watoto wa kijijini wanaita kajamba nani! haahaaa!.
Mara ya kwanza akaniomba tuonane ,bahati nzuri tukakutana pale kwa rafiki yangu kama kawaida stories za hapa na pale ,kila mtu huyoooo na hamsini zake.
Nilikuja kuambiwa na yule rafiki yangu kwamba yule binti anasema anatamani kampani yako lkn anaogopa kukwambia- nikachukulia matani tu ukizingatia alivyo nikijicheki na mimi aaah haiwezekani.
(Kisa kirefu) mwishowe alikuja kunialika kwake kwa chakula cha jioni nikaenda, tumekula tumepiga stories nikaaga nikaondoka zangu huyooooo. Alikata mawasiliano takribani wiki nzima na mimi nikawa sijashtuka wala nini. Siku tumekutana tena pale kwa rafiki yangu ,tumepiga stories kama kawaida mwishoni naaga yule dada akasema huyu jamaa mtu wa ajabu sana! Jamaa kauliza kwanini? Akasema ana roho ngumu sana- yaani anaweza akampa mgonjwa wa jino mahindi yaliyokaangwa. Tukacheka ,nikasepa zangu.
Uliingia ujumbe kwenye simu yangu" hivi mimi nina kasoro gani? usinifanyie hivo" nikampigia kudodosa sms ile, aiseee alifunguka tu, kwanini unanifanyia hivo- tukaongea saana, nikamweleza ukweli maana alinibananisha au labda una tatizo? nikamwambia tatizo ni ww hadhi yako haiendani na yangu hivo sikuwa aware kbs!
Siku niliyokuja kwenda kulala kwake ndio nikaamini kweli mwanamke akimpenda mwanaume atatumia kila mbinu kujiweka karibu nae ili tu kuchukua attention yake.
Namshauri huyo jamaa aondoe hofu na haina haja ya papara mambo yatajipa tu kadiri ya mipangilio itakavokuwa