Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Chonde chonde Usiache ajira kizembee hivo master

Kama unataka kufuga na kufanya kilimo , Tafuta wafanyakazi wakufanya hizo Kazi kwanza huku wewe ukiwa msimamizi mkuu au mkeo akawa msimamizi mkuu kwa hizo Kazi

Hayo mafanikio ya rafiki Yako yatumie Kama darasa kwanza na usikurupuke kisa eti umeona una m10 , Maisha yana hatua zake ndogondogo Sana na za Muhimu Sana zingine zinahitaji subira
 
Habari wakuu,

Baada ya kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda sasa bila ya kuyafikia maisha ya ndoto zangu, pia baada ya kuishi maisha nisiyopendezwa nayo (kukosa uhuru wa kipato) nimekaa na kutafakari kwa kina juu ya hatma ya maisha yangu na kufikia maamuzi yafuatayo.

Mosi, kuna 4.3m PPF, hiki ni kiasi ambacho nilishindwa kukitoa enzi za mwendazake baada ya kupoteza ajira. Sasa niko kwenye kampuni nyingine ambapo michango yangu mpaka sasa ni 5m,so nataka nizihamishie huku na mpaka March mwakani unapoisha mkataba wangu nitakuwa na si chini ya 10m.

Pili,kabla ya December mwaka huu nitaenda Morogoro kufanya ziara maana kuna mshikaji wangu yupo kule naye alikuwa mwajiriwa somewhere akaamua kuacha kazi na kujikita katika kilimo na ufugaji (yuko njema sana), huyu jamaa yangu atakuwa msaada sana kwangu katika kutimiza matarajio yangu.

Tatu,nikishachukua hicho kiasi namfungulia wife mradi wa 2m nyumbani then mimi nasepa zangu porini ambapo nitafanya yafuatayo

. Kufuga nguruwe na kuku
. Kulima nyanya za kumwagilia

Hayo hapo juu nitayafanya kwa 4m na kiasi kilichobaki ambayo itakuwa ni 4m nitaiweka akiba then nitakitumia kununulia mazao kama mahindi nk kipindi cha mavuno.

Karibuni wakuu kwa ushauri zaidi.
Feedback tafadhali
 
Kampuni ninayofanyia kazi haijatuwekea mazingira mazuri ya kukopa mkuu,ila pamoja na hayo nimepata suluhisho ambalo ni kuwapeleka watoto shule za kawaida ili niweze kupata mtaji.
Ualimu ni KAMPUNI kumbe? Vipi umefikia wapi na harakati zako? Njoo Mwanza tufuge samaki kwa vizimba, kuna pesa ndefu imetolewa na wafadhili MABEBERU kupitia serikali ya CCM.
 
Back
Top Bottom