Vodacom nawapa onyo kwa mara ya mwisho kabla sijafuata hatua mpya

MENEMENE TEKERI NA PERESI

JF-Expert Member
Mar 11, 2022
2,539
6,291
Ndugu zangu hamjambo ?
Natumia ukurasa huu kuwaambia watumishi wa Vodacom na wahusika wote wa MGODI kuwa mtamponza mtumishi wenu kwa hizi sarakasi zenu .

Mimi natumia laini ya voda mwaka jana nilijiunga na huduma ya MGODI specifically nilipendelea kuweka kiasi cha akiba kwenye akaunti ya akiba ya MGODI hasa basi wakanipa ofa za kukopa mpaka laki tisa na ushee ila sikuharakisha kukopa nikawa nawachora tu .

Siku nikiwa bar nikaamua kuwakopa hiyo hela nikainywa baada ya muda wakaanza madai yao , Mungu mwema niliwalipa vizuri kabisa bila kuwasumbua ila sikukopa tena kwa huo muda

Mpaka majuma mawili nyuma ndiyo niliamua kuchukua laki tisa tena japo walipandisha kiasi cha kukopa ila kutokana kuwa kuna mambo yalikaa sawa nililipa na pia nikaweka akiba tena kwenye akaunti ya akiba ya kiasi cha laki nane .

Timbwili limeanza wiki hii kila nikitoa hela kwenye hiyo akaunti ya akiba ya MGODI hela haitoki basi nimewasiliana nao majibu ni kuwa nisubiri saa 24 , kila siku jibu ni hilo nikiwapigia na nikochati nao whatsapp .

Sasa nimeshindwa na hapa nimeamua kuwalipa hivi , kuna mtumishi wao sijui ndiyo meneja wao wa huku vijijini nimeshaongea naye hili suala naye anasema niwe mvumilivu ila kwa hapa nilipofika watafihidiana wenyewe kwa wenyewe nimeamua kuwa huyu jamaa ambaye yupo hapa kijijini anafanya mqmbo ya kivodacom najua na nina ushahidi anatoka na demu wangu wa maisha na daily napewa information na wandewa wa kijiji kuwa kademu kangu kanaliwa na jamaa wa vodacom .

Sasa kwa hasara na kunipotezea muda hawa watu wa vodacom nataka nirudishe penzi kwa kasi ya 5G kwa haka kadada ili badae niweze kukamata mawasiliano yake ili nimtie mikononi mgoni wangu .

Maana kwa sheria ya hapa ukimpata mgoni wako malipo ni milioni moja na ushee hivyo chonde chonde Vodacom rejesheni hela yangu kabla mwenzenu sijamtia mikononi .

Wako katika utiisho wa malipo yangu

UPDATE

Picha ya kwanza ni ya malalamiko yangu ila ya pili ni kuwa Vodacom wameelewa kuwa niko serious na wameamua kutatua shida yangu hivyo hela yangu imekubali kutoka .

Nipo kwenye maandamano badae nitakuwa City pub wewe uliyepo mbeya njoo tufurahie , kale kadada sitakarudia tena nimeamua kukaacha na yule ofisa wa vodacom .

Ahsante kwa michango yenu na poleni wenye wivu wa hela zangu hizi ni zangu tu haziwezi kuwa zetu
 

Attachments

  • Screenshot_20240220-131354.jpg
    Screenshot_20240220-131354.jpg
    61.7 KB · Views: 10
  • Screenshot_20240220-145647.jpg
    Screenshot_20240220-145647.jpg
    153.1 KB · Views: 9
Huyu sio popoma kweli?
Mdakuzi
Mkuu hapana siye , mimi ni yule nilisema natamani kumpata mdada anayempenda bwana yake kama wewe ukasema nitampata .

Sasa nilikokapata ndiyo haka bwana wa vodacom anakapitia mimi nikiwa kwenye
Mzee unasolve lipi sasa kwanza?
Mimi nataka nianze na hili la hela kupitia haka kamdada kwa kumuwajibisha huyu bwana vodacom baada ya hapo nakabwaga chini
 
Sijaelewa kabisa! Unawapa onyo voda(kampuni) kisa ofisa wao Kala demu wako, au, onyo kwa vile hujapewa huduma Bora huko mgodini!?
Wewe uta kuwa haujalewa
 
Nilikuwa nawapa onyo kwa kushindwa kuniruhusu nitoe hela yangu MGODI dunduliza kuwa ikiwa wataendelea kunisumbua basi nitamuajibisha ofisa wao anayemla demu wangu kwa faini kubwa ili nisiwe nawadai tena .

Nashukuru wameona post yangu haraka sana nimeweza kuiotoa hela yangu, badae city pub karibu mkuu tujumuike
Sijaelewa kabisa! Unawapa onyo voda(kampuni) kisa ofisa wao Kala demu wako, au, onyo kwa vile hujapewa huduma Bora huko mgodini!?
Wewe uta kuwa haujalewa
 
Back
Top Bottom