Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Habari wakuu,

Baada ya kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda sasa bila ya kuyafikia maisha ya ndoto zangu, pia baada ya kuishi maisha nisiyopendezwa nayo (kukosa uhuru wa kipato) nimekaa na kutafakari kwa kina juu ya hatma ya maisha yangu na kufikia maamuzi yafuatayo.

Mosi, kuna 4.3m PPF, hiki ni kiasi ambacho nilishindwa kukitoa enzi za mwendazake baada ya kupoteza ajira. Sasa niko kwenye kampuni nyingine ambapo michango yangu mpaka sasa ni 5m,so nataka nizihamishie huku na mpaka March mwakani unapoisha mkataba wangu nitakuwa na si chini ya 10m.

Pili,kabla ya December mwaka huu nitaenda Morogoro kufanya ziara maana kuna mshikaji wangu yupo kule naye alikuwa mwajiriwa somewhere akaamua kuacha kazi na kujikita katika kilimo na ufugaji (yuko njema sana), huyu jamaa yangu atakuwa msaada sana kwangu katika kutimiza matarajio yangu.

Tatu,nikishachukua hicho kiasi namfungulia wife mradi wa 2m nyumbani then mimi nasepa zangu porini ambapo nitafanya yafuatayo

. Kufuga nguruwe na kuku
. Kulima nyanya za kumwagilia

Hayo hapo juu nitayafanya kwa 4m na kiasi kilichobaki ambayo itakuwa ni 4m nitaiweka akiba then nitakitumia kununulia mazao kama mahindi nk kipindi cha mavuno.

Karibuni wakuu kwa ushauri zaidi.
 
Kama unauzoefu wa kutosha kwenye sekta ya kilimo&ufugaji basi kila la kheri...

Ila kama huna uzoefu basi usithubutu kuacha kazi...nakushauri kazi usiache na ndoto zako usizipuuze Bali tafuta vijana waandae vzur then waingize Chaka wawe Wana run hizo shughuli hadi pale itakapo enda vizuri ndio uache kazi Sasa..
 
Habar mkuu, hongera kwa kufikiria kutoka katika kuajiriwa ...Ila kabla ya kukushauri zaidi naomba nikuulize

1) Unatemegmea hela yako utakayoipata kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ndio uitumie kuwekeza kwenye huo mradi unaoufikilia?
2) Ulishawahi kufanya kilimo Cha biashara katika scale yoyote ile?

3) Una interest na unaweza kukaa mashambani?

Nijibu tafadhali ili tupeane ushauri
 
risk takers ndio wanafanikiwa sana mara nyingi maana kukaa tuuu eti nikiacha kazi nitakufa hayo ni mawazo ya kizamani sana ,kuna watu walifukuzwa kazi na mwendazake walitetereka kidogo lakini baada ya kukaa vizuri mtaani waligundua kuwa walikua wananyonywa damu tu wala hakukua na cha maana walichokua wakifanya huko makazini
 
Habar mkuu, hongera kwa kufikiria kutoka katika kuajiriwa ...Ila kabla ya kukushauri zaidi naomba nikuulize

1) Unatemegmea hela yako utakayoipata kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ndio uitumie kuwekeza kwenye huo mradi unaoufikilia?
2) Ulishawahi kufanya kilimo Cha biashara katika scale yoyote ile?

3) Una interest na unaweza kukaa mashambani?

Nijibu tafadhali ili tupeane ushauri
1.Ndio mkuu
2.Nilifanya kilimo cha nyanya kama trial hap hapa kwangu,nilifuata taratibu zote za wataalam na wazoefu na matokeo niliyaona mkuu. Pia miaka ya 2003-4 niliwahi kwenda kulima Iringa,nililima maharage karanga na alizeti ila ilikuwa ni kienyeji sana.
3.Interst ninayo tena kubwa sana,naweza kabisa kukaa shamba kwani nimeshahi kufanya hivyo miaka mingi japo sikuwa na mtaji wa kutosha.

Karibu mkuu
 
Kwani fao la kuacha kazi lipo siku hizi?

Usije ukajihesabia una 10m kumbe huruhusiwi kuzipata mpaka ufike uzeeni huko
Sasa wanatoa mkuu.kuna jamaa alifukuzwa kazi mwezi wa 1 kaenda kachukua pesa kanunua Harrier then kaajiriwa kampuni nyingine.
 
Back
Top Bottom