KERO Huu mfumo wa Employee Self Service wa Utumishi haufanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,519
86,070
Sioni sababu na nashangaa kwanini UTUMISHI wamekimbilia kutumia ESS na huku ukweli haufanyi kazi, unaingia Online wanakwambia wanashidnwa ku-retrieve taarifa zako, unaomba uhamisho, unajaza kila taarifa then unakuta hakuna kiytu chochote na hakuna mtu wa kukusadiai.

Naupenda sana Mfumo wa NEST (National E-procurement System) wana kitengo cha msaada na mnafanya wote online na mnapata suluhu mara moja, yaani UTUMISHI wanashindwa hata na Customer care wa TANESCO? Mfumo gani ambao hauna msaada? huu ni mwanya wa kukaribisha rushwa na mambo mengine. Mjipange au mtoke humo ofisini. na mnavyojiona Miungu watu sasa.
 
Sioni sababu na nashangaa kwanini UTUMISHI wamekimbilia kutumia ESS na huku ukweli haufanyi kazi, unaingia Online wanakwambia wanashidnwa ku-retrieve taarifa zako...
Mfumo wa ESS ni closed loop Public system,

Kwa sababu Ukihitaji kitu kubadili au kuweka sawa unamcontact IT wako wa wilaya au HR wako...

hUu mfumo unataarifa sensitive za kiutumishi hivyo kushughilka na taarifa sensitive kama hizo kwa online help haitakuwa jambo zuri.

Ndo maana unashauriwa umconsult HR wako kwa sababu ndo.anakujua ila TAMISEMI Wala UTUMISHI hawajui maendeleo yako ofisini.

Ni tofauti na mifumo mingine
 
kwani hao Customer Care si ndio wanaweza kuwa HRs au ITs wenyewe? Mimi nataka ushuhuda hapa wa mtu aliyesaidiwa na HR au IT, ni vimeo na wana viburi balaa.
Shida ni kila Wilaya ina HR wake na IT Wake kuna maswala ambayo kila wilaya inayo ni tofauti na wilaya zingine..

Kwa mfano ni Vigumu kwa Afisa Utumishi wa Tamisemi ni Vigumu kumjua Jackson Abdalla alieajiriwa Tunduma na Jackson abdallah alieajriwa Lushoto..

Ndo maana Kila mtumishi Customer care yake ataipata katika halmashauri yake kuepuka mkanganyiko...

Yes ni kweli kabisa wapo waliosaidiwa na Watu wa TEHAMA na Ma HRs na wapo ambao wanaona kuwa watu hao wako humble na wapo wanaoona hawafanyi kazi..

Ubovu na ubora unategemea na halmashauri
.
 
Sioni sababu na nashangaa kwanini UTUMISHI wamekimbilia kutumia ESS na huku ukweli haufanyi kazi, unaingia Online wanakwambia wanashidnwa ku-retrieve taarifa zako, unaomba uhamisho, unajaza kila taarifa then unakuta hakuna kiytu chochote na hakuna mtu wa kukusadiai.

Naupenda sana Mfumo wa NEST (National E-procurement System) wana kitengo cha msaada na mnafanya wote online na mnapata suluhu mara moja, yaani UTUMISHI wanashindwa hata na Customer care wa TANESCO? Mfumo gani ambao hauna msaada? huu ni mwanya wa kukaribisha rushwa na mambo mengine. Mjipange au mtoke humo ofisini. na mnavyojiona Miungu watu sasa.
Nest ni nzuri ila nachukia sana unapotafuta items ni ushenzi mtupu kwenye ile template ya excel, unaezakaa lisaa unatafuta item moja hauipati, jamamaaa wamanunuzi akaniambia unajichosha zile code akaniambia just pick any copy ila spec ndo uweke za kueleweka
 
Kuweni waangalifu sana ni hiyo mifumo ya IT.
Unaweza shituka unaletewa barua ya Kuachishwa kazi bila kujua.
Unabonyeza bonyeza bila tahadhari utajikuta umeomba kuacha kazi masaa 24.
Kuna watu bila kubonyeza bonyeza kwenye mifumo ya Serikali hawaridhiki kabisa.
 
Mpaka mtu anajiachisha kazi ina maana hajui kusoma ? Maana kila sehemu ya kubofya kuna maandishi yanayomuongoza.
 
Kuweni waangalifu sana ni hiyo mifumo ya IT.
Unaweza shituka unaletewa barua ya Kuachishwa kazi bila kujua.
Unabonyeza bonyeza bila tahadhari utajikuta umeomba kuacha kazi masaa 24.
Kuna watu bila kubonyeza bonyeza kwenye mifumo ya Serikali hawaridhiki kabisa.
🤣🤣🤣Si bora hao washajisajil,sisi wengine tunamsubiri afisa utumishi wizarani dodoma apitishe email address zetu ili tujisajili🙏
Ila maadamu salary inasoma,fresh tu
 
Huu mfumo hauna msaada kwa mtumishi kwenye mambo nyeti mengi.

Umejaa ukiritimba uleule wa awali. Nasikia ukitaka uhamisho lazima uwasiliane na mkuu wako wa idara pamoja na viongozi wengine wa mkoa kama katibu tawala ili waweze ku-approve maombi yako ndo taarifa ziende TAMISEMI kwa ajili ya uidhinishaji wa mwisho wa maombi.

Mfumo umeongeza usumbufu uleule tuliokuwa tunaulalamikia. Ila ninasikia kwenye suala la mikopo ya benki kwa watumishi kupitia e-loan wako faster ukitumia mfumo kuliko kujaza form.
 
Back
Top Bottom