Hutakiwi kuitwa Professor kama hufundishi

Navyojua mimi Professor ni jina la kiwalimu na ndiyo maana huwezi kwenye US au UK ukasikia mwanasiasa full time anaitwa Professor bali wanaitwa Dr au wanaweka PHD mwisho na wanaitwa majina ya kawaida
Heshima Mkuu!

Hivi ni lazima tuwe kama hao uliowaita (US na UK)?.Au ndiyo muendelezo wa Falsafa ya "Tuige kila kitu kutoka nje"?.

Heading ya thread yako na maelezo ni tofauti.Nadhani ungeishia kwenye ku-reason juu ya ufundishaji pekee ingekua poa zaidi kuliko kuingiza masuala ya kisiasa.
 
Navyojua mimi Professor ni jina la kiwalimu na ndiyo maana huwezi kwenye US au UK ukasikia mwanasiasa full time anaitwa Professor bali wanaitwa Dr au wanaweka PHD mwisho na wanaitwa majina ya kawaida
Hiyo ni ya kwako.
Huwezi kuwa Professor bila kufundisha ila ukishapewa haijalishi.
Mwishoni utasema asiitwe mtu doctor kama hatibu.
 
Mkuu nakuunga mkono, obviosly kwa hapa bongo mimi huwa namkubali sana Prop. Shivji, kwanza jamaa anaandika vitabu vya kutosha, pia uchambuzi wake ni wa kiwango cha kimataifa! Kifupi ni kwamba anajua nini anafanya na kwa wakati gani tofauti na hao wengine!
Naomba uedit neno Prop.

Pia naomba list ya majina ya vitabu walau tano (5) vya Prof Issa G Shivji.
 
Mkuu nakuunga mkono, obviosly kwa hapa bongo mimi huwa namkubali sana Prop. Shivji, kwanza jamaa anaandika vitabu vya kutosha, pia uchambuzi wake ni wa kiwango cha kimataifa! Kifupi ni kwamba anajua nini anafanya na kwa wakati gani tofauti na hao wengine!
But kwenye suala la katiba mpya he was just a disappointment and coward! Alicheza chini ya kiwango big time.

Wasomi wengi wa nchi hii tatizo letu kubwa kabisa ni njaa tu, matumbo yetu yanatangulia halafu ndio tunatizama profesaionalism!
 
Navyojua mimi Professor ni jina la kiwalimu na ndiyo maana huwezi kwenye US au UK ukasikia mwanasiasa full time anaitwa Professor bali wanaitwa Dr au wanaweka PHD mwisho na wanaitwa majina ya kawaida
Kwani Tanzania ni US au UK?sio kila kinachofanya US na UK basi nasi tukifuate
 
Mfano Mugabe ana PHD tatu na hajawahi jiita prof..wakina prof wakina lipumba mwenye ofis yake buguruni.
Kwani Uprofesa unajipachika ,sijasikia kama Mugabe amewahi kufundisha chuo kikuu pamoja na kuwa na hizo digrii,kuwa na digrii hakukufanyi tu basi uwe professor ,mambo mengine ni afadhali ukae kimya tu na digrii nyingi za Mugabe alipata kwa distance learning ni kama Elimu kwa Njia ya Posta,huwezi kumfananisha na kichwa Lipumba
 
Jamani bashite anaiharibu hii nchi yani watu wanajitaidi kuanzisha nzuzi zinazo kejeli wasomi wetu ili waonekane Elimu zao hazina maana yaani=bashite.Duh watz hawafai...
 
Unaweza kuwa Prof bila kufundisha. Hata Mwl Nyerere alikuwa Prof japo alikuwa hafundishi. Ila alipendeke zaidi kuitwa Mwl. Mkapa nae alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari (ila hakushadadia kuitwa Dk) tofauti na JK ambaye aliwazidi hata wale waliousomea huo UDr.
Hiyo ni ya kwako.
Huwezi kuwa Professor bila kufundisha ila ukishapewa haijalishi.
Mwishoni utasema asiitwe mtu doctor kama hatibu.
 
Neno Professor Original yake ni Kifaransa, liki maanisha Mwl. Hivi asiye Mwl wa chuo hapaswi kuitwa Prof.

Nashangaa hapa Tz wasiasa ni ma Dr na ni ma Prof wakati hawapublish au hawajawahi hata kupublish article yoyote.

Mf. Prof. J4 Maghembe
Prof. Lipumba
Dr. Mengi
Dr. Kafumu
Dr. Jakaya Kikwete
Dr. John Magufuli
Dr. Nchimbi
Dr. Antony Dialo
Dr. Mahanga nk

Mm nacho fahamu kuna strict Universities hata ukiwa Dr. ikipita miaka kadhaa (mf 10 yrs)bila kupublish any article Senate inaweza kukaa na kukunyang'anya u Dr wako. U Doctor siyo cheo ila ni ngazi ya kufanya tafiti.
 
Navyojua mimi Professor ni jina la kiwalimu na ndiyo maana huwezi kwenye US au UK ukasikia mwanasiasa full time anaitwa Professor bali wanaitwa Dr au wanaweka PHD mwisho na wanaitwa majina ya kawaida
Utumiaji wa jina/cheo professor unategemea nchi na nchi. Ni kweli kama US mara nyingi hutumiwa mtu anapokuwa anafundisha/anatafiti chuoni na mara aachapo ana acha kutumia jina/cheo hicho. Hapa kwetu tumekuwa na hiyo tabia ya kuendelea kuitwa Le Professeri hata kama umeachana na hilo jukumu lakini sijaona mahali popote ambapo imeandikwa ukiacha hiyo kazi basi na cheo hicho unakitema au chuo kina kuruhusu uendelee kutumia jina hilo (kwani ukishatoka chuo huna tena cheo hicho). Tukumbuke pia watanzania tunapenda sana hizi title ndio maana una mabalozi ambao hawajawa mabalozi nao wakiacha bado ni mabalozi. Rafiki zangu engineers waliona kuitwa Mr au Mrs au Miss Fulani haitoshi wakaona watangulize Eng. Hao wanaofanya kazi zahanati na vitu kama hivyo wote hujiita Dr. hata kama sheria hairuhusu. Tuna waheshimiwa ambao sio waheshimiwa. Kwa hiyo bora liende.
 
Kuiga kutatuponza jaman zaman wazungu walitengeneza nguo ili kuvaa mwili mzma kujikinga na baridi ,pia kmaadili sisi tulikua na magome tu ndo kama nguo ( tuliishi safi) wakaleta nguo tukaiga ,,,,leo hii wao wenyewe wnaturudisha kulekule kutembea uchi (vimin)
 
Prof chachage
Mfano Mugabe ana PHD tatu na hajawahi jiita prof..wakina prof wakina lipumba mwenye ofis yake buguruni.
 
Back
Top Bottom