Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
5,562
2,000
Matokeo ya yaliyompa ushindi Dr Hussein Mwinyi katika kikao Cha halmashauri k ya chama nec yalikuwa Kama ifuatavyo ,Nahodha 16, Khalid 19 jumla 35 ambazo ndio idadi kamili ya wajumbe wa Zanzibar na kura 129 Za Hussein Mwinyi ambazo na za wajumbe wote wa Tanzania barabara ,haki ya Wazanzibar kuchagua kiongozi wao imeheshimiwa? Mbona kama wamechaguliwa kiongozi au wenzangu mnalionaje hili.Hawana haki ya kulalamika?
IMG_20200712_124921.jpg


Soma Uchaguzi 2020 - Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
15,023
2,000
VIJANA WA CCM TUKAE KWA KUTULIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kila nikiangalia hii picha ya Joshua Nasari, nikikumbuka na swali lililoulizwa na Mjumbe Wa NEC toka Songwe kuhusu wahamiaji kupewa Vyeo badala ya vijana waliopo CCM nacheka Sana.

Definitely tuache Hawa vijana wajinafasi kwa kuwa sioni ndani ya UVCCM mwenye uwezo wa kuwazidi. Nilipokuwa nasema Sana kuhusu hili miaka ya kuanzia 2017 Hakuna waliokuwa wanaunga mkono Hoja hiyo kila mtu alikuwa anaimba litania, Ngonjera,Pambio za Masifu, kupiga Manyanga nk.

Niliwaambia ifikapo 2020 mtakumbuka haya niliyokuwa nawaandikia na niliwaambia CCM Asilia itakuwa imetekwa na kutiwa mfukoni. Ni Dhahiri baada ya chuo Cha kivukoni kushindwa kupika vijana wa CCM Chadema inatusaidia jukumu Hilo.

Huwa nawaambia mnapata wapi ujasiri wa kuwaita Chadema Nyumbu? Hahahahah tutulie infact hatuna vijana wanaofikia viwango vya Hawa watu. Tutulie tuendelee na kujifua.

Ukiona baba yako anawagawia watoto wa Jirani Urithi ujue wewe ni mvuta bangi na mla Unga. Akikupa Urithi utauza upate hela ya kulamba Unga.

Ole Mushi
0712702602
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,054
2,000
Wao CCM wanaamini Muungano ni God's creation na kamwe hauwezi kuvunjwa na nguvu za binadamu ndiyo maana wanaulinda hata kwa damu.
Utavunjwa tu (ni muda tu ndio utaongea), hakuna mzanzibar anayetaka MUUNGANO ,hauna faida kwao zaidi ya kuwanyonya tu!!
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,054
2,000
Kama Wazanzibar wengi hawaridhii muungano ni swala la muda tu, ipo siku tutagawana fito.
Hakuna hata mzanzibar mmoja anayetaka Muungano na ndio maana JMT wanafanya kila njia Rais wa Zanzibar asiwe PURE mzanzibar, Mzanzibar asilia akigombea jina lake lazima likatwe,kina Vuai wamewekwa kama geresha(Rubber stamp) tu!!
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,212
2,000
VIJANA WA CCM TUKAE KWA KUTULIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kila nikiangalia hii picha ya Joshua Nasari, nikikumbuka na swali lililoulizwa na Mjumbe Wa NEC toka Songwe kuhusu wahamiaji kupewa Vyeo badala ya vijana waliopo CCM nacheka Sana.

Definitely tuache Hawa vijana wajinafasi kwa kuwa sioni ndani ya UVCCM mwenye uwezo wa kuwazidi. Nilipokuwa nasema Sana kuhusu hili miaka ya kuanzia 2017 Hakuna waliokuwa wanaunga mkono Hoja hiyo kila mtu alikuwa anaimba litania, Ngonjera,Pambio za Masifu, kupiga Manyanga nk...
Heri ni wao wenye kuuona ukweli huu. UVCCM wamezoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi. Hawaaminiki, hawana hoja zakueleweka hata kuweza kushawishi kwa wale wenye dhamana za uteuzi. Pengine dada zao angalau wataweza hata kupata ubunge wa viti maalum ili waweze kutoa usingizi kwa wazee wenye "stresses".
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
15,023
2,000
Heri ni wao wenye kuuona ukweli huu. UVCCM wamezoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi. Hawaaminiki, hawana hoja zakueleweka hata kuweza kushawishi kwa wale wenye dhamana za uteuzi. Pengine dada zao angalau wataweza hata kupata ubunge wa viti maalum ili waweze kutoa usingizi kwa wazee wenye "stresses".
uvccm kwa sasa wanachojua ni kuteka, kupiga risasi , kutukana mtu mwenye mawazo tofauti......Yaani hawajaandaliwa kuwa viongozi wanafundishwa udikteta kwa vitendo awamu hii.

Ila sasa WHAT GOES AROUND COMES AROUND. Udikteta walioupalilia umekuja ndani mwao wameanza kukanyagana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom