Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Matokeo ya yaliyompa ushindi Dr Hussein Mwinyi katika kikao Cha halmashauri k ya chama nec yalikuwa Kama ifuatavyo, Nahodha 16, Khalid 19 jumla 35 ambazo ndio idadi kamili ya wajumbe wa Zanzibar na kura 129 Za Hussein Mwinyi ambazo na za wajumbe wote wa Tanzania barabara ,haki ya Wazanzibar kuchagua kiongozi wao imeheshimiwa? Mbona kama wamechaguliwa kiongozi au wenzangu mnalionaje hili.Hawana haki ya kulalamika?View attachment 1504475
Mambo ya Wazanzibar, wewe mtanganyika yanakuhusu nini ?
 
VIJANA WA CCM TUKAE KWA KUTULIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kila nikiangalia hii picha ya Joshua Nasari, nikikumbuka na swali lililoulizwa na Mjumbe Wa NEC toka Songwe kuhusu wahamiaji kupewa Vyeo badala ya vijana waliopo CCM nacheka Sana...
Ndio maana utaona Mh.Rais hizi teuzi za hivi karibuni kaamua kuteua walioko ofisini sio vijana wa uvccm hiyo inaonyesha vijana wengi wa ccm hawana uwezo wa kiuongozi
 
Hapa panahitaji maelezo toka kwa Dr. Bashiru Ally katibu Mkuu CCM juu ya uvumi huu ambao bado haujathibitishwa lakini CCM zote mbili yaani CCM Zanzibar na CCM Mpya hawajajitokeza kutuambia hali ilikuwaje.

Bila maelezo toka Dodoma, hesabu hizi za kali 129 + 19 + 16 = 164 zinatoa jibu la jumla kubwa linalotaka tamko toka kwa chama hiki kikongwe nini kilitokea mjini Dodoma. Je kuna mpasuko ndani ya CCM yaani CCM bara na CCM Zanzibar ? Kwako ndugu Humphrey Polepole ufikishe ujumbe.
 
Lete ushahidi kwa sababu kura zilikuwa za siri!
Wee kilaza kweli alete ushahidi gani tena wakati matokeo yalitangazwa na kwamba wajumbe wa bara wanaopiga kura ni 129 Zanzibar ni wajumbe 35 shamsi alipata kura 16. DK alipata kura 19 umeelewa hapo
 
uvccm kwa sasa wanachojua ni kuteka, kupiga risasi , kutukana mtu mwenye mawazo tofauti......Yaani hawajaandaliwa kuwa viongozi wanafundishwa udikteta kwa vitendo awamu hii.

Ila sasa.....WHAT GOES AROUND COMES AROUND.....Udikteta walioupalilia umekuja ndani mwao wameanza kukanyagana
Wajinga sana hawa vijana
 
Wee kilaza kweli alete ushahidi gani tena wakati matokeo yalitangazwa na kwamba wajumbe wa bara wanaopiga kura ni 129 Zanzibar ni wajumbe 35 shamsi alipata kura 16. DK alipata kura 19 umeelewa hapo
Wewe kweli mbwiga.

Kwani hao wazanzibar kura zao zilihesabiwa peke yao?!
 
CCM wamerahisisha ushindi wa Maalim Seif Zanzibar
Ndugu Sky Eclat, sijui ukweli unamipita wapi, ndugu mmejipifua sana kwa kukataa kuyaona maovu ndani ya chama chenu, hadi linefanya kuwa macho yenu hayaoni ukweli.

Sky uchaguzi kwa Maalim umezidi kuwa mgumu na ushaguzi wa halali umetoweka kabisa. Msitegemee ACT kutangazwa mshindi hata siku moja, kama Mbowe atakovyo kosa kiti chake cha ubunge hata akipata 70% ya kura, kama atagombea ubunge badala ya Uraisi
 
Umejuaje kama hao 35 hawakumpigia kura Dr Mwinyi?!

Ata hili unataka ufafanuzi ama limurikwe tochi? unaambiwa wajumbe kutoka Zanzibar ni 35 na zile kura za shamsi na Khalid ni 35, lakini idadi ya wajumbe kutoka Tanganyika ni iliyobaki kwenye Idadi ukitoa 35, Kwa akili yako yakawaida tu bila ya akili ya darasani ivi kweli Mizengopinda anaweza kumpigia kura Dr. Khalid ama Shamsi?

Haya mambo yapo miaka nenda miaka rudi, Wazanzibari na maalim seif wamepiga kelele mpaka vifua vimewakauka lakini ccm wa zanzibar bado walikuwa na tamaa watampata rais wao wamtakae.

Sasa matokeo yake pressure imeanza kuwakumba huko huko Dodoma, na kama mwinyi ndo atafuata nyayo za mkuu ccm zanzibar wategemee anguko kubwa la wale waliokuwa wakijifanya wana hati miliki kwenye chama cha Mapinduzi Zanzibar.
 
Ata hili unataka ufafanuzi ama limurikwe tochi? unaambiwa wajumbe kutoka Zanzibar ni 35 na zile kura za shamsi na Khalid ni 35, lakini idadi ya wajumbe kutoka Tanganyika ni iliyobaki kwenye Idadi ukitoa 35, Kwa akili yako yakawaida tu bila ya akili ya darasani ivi kweli Mizengopinda anaweza kumpigia kura Dr. Khalid ama Shamsi?

Haya mambo yapo miaka nenda miaka rudi, Wazanzibari na maalim seif wamepiga kelele mpaka vifua vimewakauka lakini ccm wa zanzibar bado walikuwa na tamaa watampata rais wao wamtakae. Sasa matokeo yake pressure imeanza kuwakumba huko huko Dodoma, na kama mwinyi ndo atafuata nyayo za mkuu ccm zanzibar wategemee anguko kubwa la wale waliokuwa wakijifanya wana hati miliki kwenye chama cha Mapinduzi Zanzibar.
Uko kihisia zaidi siyo Uhalisia.

Kura ya Pinda wewe uliiona?
 
Wazanzibari wenyewe hawajitambui, wameuza nchi yao kwa Tanganyika. Wacha Watanganyika wawateulie rais
Usitukane wazanzibari , wazanzibari wanajitambua kuliko mnavojitambua(watanganyika) tatizo CCM Zanzibar wachache wameisaliti Zanzibar kwa masilahi binafsi. Binafsi nadhani hatimaye adui amejulikana kilichobakia is to bury the little differences among Zanzibaris and bury the hatchet in head of common enemy.
 
Back
Top Bottom