Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Umemjibu vema kabisa. Na anasahau kabisa kuwa ZEC inamtaka mtu kuwa mzanzibar (wao wanaita mkaazi) ili kuwa mpiga kura au mgombea. Kama jamaa alikuwa Mbunge wa Mkuranga - wanamchukulia sio mzanzibar na ndio maana alishinda kwa kura za wabara!! Mimi sielewi ni kwanini wajumbe watofautiane kwa idadi kati ya nchi hizi mbili. Labda ni kwa kuwa siko katika siasa lakini ni dhahiri maamuzi ya wanaCCM Zanzibar yatafanywa na CCM Bara - siku zote!!

Naona njia nyeupe kwa Seif, ziliwemo kura nyingi za wanaCCM hasa baada ya mshindi kusema ataongoza Zanzibar kama JPM anavofanya Bara!
Ni dhahiri Seif atapata

Ila jamaa wamezoea kubaka matokeo

Hata Mwinyi anajua atapata kwa nguvu ya CCM na sio wananchi
 
Matokeo ya yaliyompa ushindi Dr Hussein Mwinyi katika kikao Cha halmashauri k ya chama nec yalikuwa Kama ifuatavyo ,Nahodha 16, Khalid 19 jumla 35 ambazo ndio idadi kamili ya wajumbe wa Zanzibar na kura 129 Za Hussein Mwinyi ambazo na za wajumbe wote wa Tanzania barabara ,haki ya Wazanzibar kuchagua kiongozi wao imeheshimiwa? Mbona kama wamechaguliwa kiongozi au wenzangu mnalionaje hili.Hawana haki ya kulalamika?View attachment 1504475
Hesabu ngumu sana hizi...
Hazitofautiani sana na zile za JMT 1+1=3
 
Kwa uhakika gani kwamba wengine si wajumbe wa Tanzania bara waliompigia kura Nahodha na mwenzie.Hoja ni kwamba pengine Mwinyi halikuwa chaguo la wazanzibari wengi au vinginevyo Ila hii probability yako haiko sawa
 
Vijana wa Znz ndio mnatakiwa mlete ukombozi,wengi mnakimbia nchi yenu mnaenda ulaya kujilipua kama mashoga,ndio mnaona ufahari
Ha ha! Hii ni noma sana. Kuna mmoja kajilipua kwa namna hiyo, si akaingizwa kwenye chama cha mashoga, na anapaswa kuhudhuria vikao na shughuli zao ili kudhiirisha kwamba yeye ni shoga aliyekimbia Zanzibar kwa sababu ya haki za binadamu!! Halafu swala tano kama zote! Maisha haya!!
 
Safari hii asijitangaze, asubiri tume imtangaze 😀😀vinginevyo atawarahisishia tena


Kuna kutangaza kura na kuna kutangaza ushindi, kutangaza kura ni ruksa kwa kila mgombea. Yeye Maalimu atatangaza kura alizopata na sio ushindi.
 
Nao hao wanaokwenda CCM ni waganga njaa. Utaona wasomi lakini maisha yanawapiga chini. Inabidi waende kule wasamehewe madeni waliochukuwa.
 
Ngoja niendelee kunawa mikono kwa maji tiririka tu..siasa nawaachia wenyewe.
 
Matokeo ya yaliyompa ushindi Dr Hussein Mwinyi katika kikao Cha halmashauri k ya chama nec yalikuwa Kama ifuatavyo ,Nahodha 16, Khalid 19 jumla 35 ambazo ndio idadi kamili ya wajumbe wa Zanzibar na kura 129 Za Hussein Mwinyi ambazo na za wajumbe wote wa Tanzania barabara ,haki ya Wazanzibar kuchagua kiongozi wao imeheshimiwa? Mbona kama wamechaguliwa kiongozi au wenzangu mnalionaje hili.Hawana haki ya kulalamika?
View attachment 1504475

Soma Uchaguzi 2020 - Dkt. Mwinyi: Wajumbe wa Zanzibar waliotupigia kura ni 68 hata kama ni kweli wenzangu walipata 35 basi na mimi nilipata 33

 
Back
Top Bottom